Mungu hakupi vyote, wala hakunyimi vyote

Mungu hakupi vyote, wala hakunyimi vyote

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,007
Reaction score
168,596
Hapo mwanzo Mungu alipoumba dunia akaitengeneza Ulaya na milima na barafu kali kila mwaka,
Kisha akatengeneza Marikani nako akawatupia hali hiyo ya hewa ya kila mwaka kuwa katika msimu wa barafu.

Halafu akatengeneza Afrika, milima na mabonde yenye rutuba,mito yenye samaki tele, hali ya hewa safi, madini kibao Tanzanite, dhahabu, almasi,shaba, chuma, wanyama wa kila aina na mali asili kibao, pakalingana sana na paradizo.

Wazungu wakaja juu,'Jamani umetuonea, mbona hao umewapendelea?" Mungu akawambia "Acheni kiherehere ngojeni muone viongozi ntakaowapa"
 
Akaumba na JF, halafu alipoiona ni njema akamuumba watu8.
Siku zilivyokua zinaenda, akaona ya kwamba watu8 yu mpweke. Basi akajisemesha, "Nitamfanyia watu8 msaidizi wa kufanana naye, nyama katika nyama zake na mifupa katika mifupa yake".
Siku moja watu8 akiwa ameamka kutoka kwenye usingizi mzito, pembeni yake kulikua na kiumbe chenye uzuri usio kifani, chapendeza kwa macho na umbo pia. watu8 akavutiwa naye na jina lake akamwita measkron, huyo ndiye mkewe hata sasa.
Haleluya!!
 
Last edited by a moderator:
Buji umetisha, maneno yote haya huwa unayafikiria mida gani? Yako sence na yanachekesha
 
Nijuavyo ni kuwa Mungu ni hakimu wa haki, na akiamua yeye hamna mahali pengine popote unapoweza kwenda kukata rufaa
 
Umewahi kujiuliza ni kwa nini Matornado yanatokea Amerika na sio sehemu nyingine yoyote ..??
 
Ni bahati sana kwani Mungu huyu huyu alimuumba mk..we...rrr!! Bwana Mungu nashangaa kabisa nikitazama jinsi vilivyo, milima maji na vitv vyote pia viumbwavyo kwa uwezo wako.
 
Back
Top Bottom