Mungu Haishi. Maana Si Kiumbe

Una uthibitisho gani kwa haya uyasemayo? Leta ushahidi au kaa kimya
wewe uliyesema juu kuna mbingu ndio ulete ushahidi .kila siku vyombo vya Nasa na makampuni mengine yanaenda huko anga za mbali ushasikia kuna chombo kimeona au kukuta mbingu.kuna galaxy zip mabilioni ya miaka ya mwanga s zingegonga mbingu.kwa kuwa umeshakuwa brainwashed tangu utoto wako lazima uamini ile anga ya blue ni mbingu
 
Umejuaje mkuu kama Mungu ameumba viumbe? isije ikawa unamsingizia tu
 
Babu zetu walio ishi na kufa kabla ya hivi vitabu havijaja,walimjua Mungu ?
Sidhani kama kuna jamii ambayo haina neno Mungu kwahiyo suala la vitabu ni utofauti tu wa mafundisho ambayo huwa yanabadilika badilika, kwahiyo naweza kusema hata hao mababu zetu nao walikuwa na mafundisho ya Mungu ambayo walikuwa wakiyafuata kwa wakati uliyopo na mazingira yao ila Mungu ni huyohuyo tu.
 
Shida inakuja miungu haujawahi sema chochote kile. Zaidi ya wakoloni kutuletea vitabu wakidai miungu inataka nini. Lakini miungu yenyewe haijawahi kusema kitu.
Kwanini sasa haisemi kitu ni mabubu au vp?
 
Unadhani Mungu huyo huyo leo angekuwa na Makundi haya Yaliyopo. Huku Waislamu.. Huku wakristo.. Huku Wa Hindi n.k n.k

Huyo Mungu hapendi umoja na Muongozo mmoja
 
Kwanini sasa haisemi kitu ni mababu au vp?

Kwanini sasa haisemi kitu ni mababu au vp?
Swali lako zuri.
Kwanini haisemi kitu?
Haisemi chochote na haijioneshi kama ipo. Tutajuaje kama ipo sasa.
Ukweli ni kwamba, hakuna wa kuthibitisha chochote kile zaidi ya kila mtu kuja na nadharia zake au tu imani zake. Lakini miungu yenyewe haijawahi kusema chochote.
 
Mungu anajulikana kwako kadri unavyoweza kumuelewa, hakuna maelezo ya kutosha ya kibinadamu yanayoweza kujitosheleza. Waache watu wamjue kadri anavyojifunua kwao.
 
Unadhani Mungu huyo huyo leo angekuwa na Makundi haya Yaliyopo. Huku Waislamu.. Huku wakristo.. Huku Wa Hindi n.k n.k

Huyo Mungu hapendi umoja na Muongozo mmoja
Suala la hizo dini linahitaji mjadala wake ila hapo mie nimejaribu tu kueleza kuwa si kwamba huyo Mungu wa kwenye vitabu hakujifunua kwenye jamii zengine tofauti na hizo jamii zilizomo kwenye hivyo vitabu. Ni vile hatujaelezwa ama tuseme historia zao hazikuandikwa kama zimevyoandikwa jamii za kwenye hivyo vitabu.
 
Nimekuuliza hivyo kwa sababu hata wewe unaposema miungu haisemi chochote inakuwa ni nadharia yako pia na ndio maana nikakuuliza kwani hiyo miungu ni mabubu? Maana mabubu wapo tunawaona ila hawawezi kusema.

Au ufafanue unaposema miungu haisemi chochote una maana gani?
 
Shida ya mtoa mada ni kukosa uelewa wa elimu ya kiroho. Elimu ya kiroho ni pana zaidi ya DINI, Japo kwa kiasi kidogo dini zimeelezea elimu hii. Hauwezi kukamilisha na ukaelewa au ukaeleweka kwa source na material ya DINI tu.
In short, Mungu aliye HAI ni kuwa Mungu yupo active mda wote,viumbe vyote kuna kipindi vinakuwa vimelala na hivyo kwa namna fulani wanapoteza sifa za kiumbe hai.
Tafsiri sahihi ya elimu ya kiroho,Kiumbe ni mwili ambao una roho ndani yake hivyo kinachoishi ni roho na sio mwili. Mwili unaweza ukaukatakata na bado ukaishi,why kwa sababu roho bado inaishi.
Viumbe vyote vitakufa au miiliyote itakufa na kurudishiwa miili hiyo(kufufuliwa) baadae.
Roho haifi na inaishi kwakuwa ihai.
Napumzika kiaina nitaendelea kwa mwenye uhitaji
 
Miungu kutosema chochote wala sio nadharia. Ni jambo halisi lenye uthibitisho. Maana ya "miungu haisemi chochote" ni kwamba miungu haijawahi kutujulisha kama ipo na mtu akitaka kuijua haimuoneshi kama ipo. Wala haituongozi tufanye nini hapa duniani na haitupi sababu yoyote ya kuishi.
 
Je hiyo miungu ipo au haipo?
 
Sawa kabisa..Mungu ni zaidi ya uhai....Mtu anapotaja uhai maana yake kuna kifo..Mungu hayuko kabisa kwenye hizo level za uhai ma kifo....Mwanadamu kumuelewa Mungu ni nini...haiwezekani.....tinajitutumua tu..lkn Mungu ni juu sana ya hizi akili zetu....Mungu ni yupo, aliyekuwepo na atakayekuwepo....Mungu ndo kaumba huo uhai....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…