Mungu haijui kesho yako

Kwa hiyo jinsi moyo wangu unavyokuwa na matamanio yake mimi ndio naamua huo moyo uwe hivyo ama mungu ndio huamua moyo wako uwe hivi ama vile?
 
Kwahiyo wale panya roads hawakulelewa vizuri na wazazi wao?

Usilolijua ni usiku wa giza.
 
Kwa hiyo jinsi moyo wangu unavyokuwa na matamanio yake mimi ndio naamua huo moyo uwe hivyo ama mungu ndio huamua moyo wako uwe hivi ama vile?
Ni training yako mwenyewe. Kama vile unavyotaka mwili wako uwe na misuli wenye afya au ujae sumu za sigara, shisha bangi. Ts all about you. Ni mwili wako, moyo wako, roho yako.
 
Na kama uwezo wa kutuzuia anao ila anaamua kutuacha maana yake anafanya uovu, kitaalam tunaita ‘Sadism’, yaani ni Sadist, ana-enjoy kuona mateso ya wengine, otherwise why uruhusu na unao uwezo wa kuzuia?
Acheni upumbavu, mbona hukanyagi moto ukuunguze mguu ilihali uwezo wa kuukanyaga unao?

Au mbona hujipeleki huko vitani Ukraine ukafe nakati uwezo wa kwenda unao?

Au kwanini hujilazi kwenye reli ili treni ikija ipite nawe ufe nakati una uwezo huo?
 
Ni training yako mwenyewe. Kama vile unavyotaka mwili wako uwe na misuli wenye afya au ujae sumu za sigara, shisha bangi. Ts all about you. Ni mwili wako, moyo wako, roho yako.
Ok kwa hiyo mimi ndio nikaamua moyo wangu uwe vipi kutokana na training yangu, so sio mungu anayeamua moyo wangu uwe na tamaa fulani, na sio mungu anayeamua wala kujua future yangu iwe vipi, sio?
 
Mimi kuna issue flani nimezinote watu wenye roho mbaya, makatili na washenzi ndio naona wanafanikiwa huku duniani kuliko watu wema sijui hizi hesabu zimekaaje
mwenye uelewa afafanue. Mimi ni mtu wa dini pia naamini Mungu yupo
 
Changamoto za maisha zinawafanya watu wakufuru
 
Ok kwa hiyo mimi ndio nikaamua moyo wangu uwe vipi kutokana na training yangu, so sio mungu anayeamua moyo wangu uwe na tamaa fulani, na sio mungu anayeamua wala kujua future yangu iwe vipi, sio?
Sasa unachanganya. Kuna tofauti ya kujua future yako na kuamua future yako. Anayeamua future yako ni wewe ila iyo future MUNGU anaijua kutokana na maamuzi yako na mambo yanayoumba matamanio yako ndani yako.

Kama wewe binadamu ukimuona binti anatamani kutembea na kila mwanaume unajua kabisa huyu ataishia kupata mimba na ukimwi yeye MUNGU ambaye anawatazama binadamu vizazi na vizazi atashindwaje kujua matokeo ya maamuzi yako? Kuna jambo gani jipya utakalofanya asijue litakapokupeleka? Kama anauwezo wa kuona ndani mawazo ya matamanio yako anashindwa vipi kujua huyu kutokana na hii tamaa atafanya nn?
 
Kwa hiyo kama hiyo future yangu naamua mimi, so Mungu anajua nitakachoamua kabla hata sijaamua?
 
maisha baada ya kifo unayatengenezaje wakati nayo pia yashapangwa
 
Mbona mnatumia nguvu nyingi kutuaminisha Mungu hayupo? Kama shetani yupo basi MUNGU YUPO! kama umeamua Mungu hayupo sio lazima utushirikishe.

Kumb 30:19 ''Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;''
 
Mimi kuna issue flani nimezinote watu wenye roho mbaya, makatili na washenzi ndio naona wanafanikiwa huku duniani kuliko watu wema sijui hizi hesabu zimekaaje
mwenye uelewa afafanue. Mimi ni mtu wa dini pia naamini Mungu yupo
Kwa mimi mafanikio ni kuwa na amani ya roho, tena sihitaji mijumba ya kifahari, mali wala mipesa mingi maana naona karibu asimilia kubwa ya vyanzo vya uovu ni ukwasi, kama ilivyokuwa kwa Mfalme Suleiman alipoomba hekima akazidishiwa na utajiri.

Matokeo yake uliyaona hadi mwishowe Mfalme Suleiman alikuwa na Michepuko tele, alimwasi Mungu na alikiri kuwa "yote ni ubatili mtupu bila ya kumcha Mungu"
 
Kwa hiyo kama hiyo future yangu naamua mimi, so Mungu anajua nitakachoamua kabla hata sijaamua?
Ni kama wewe unavyojua hili gari litakula mafuta kiasi fulani hata kabla hujaliendesha kwa sababu unafahamu mfumo wa cc zake na matokeo ya kuendesha gari lenye hizo cc.

MUNGU nae anaangalia matamanio yako anajua utakapoelekea. Hakunaga suprice katika maamuzi, lolote utakalolifanya palikuwa na maandalizi, yale maandalizi ndiyo MUNGU huyaona, ukijiandaa kughairi au kubadilika anaona unavyojiandaa kabla hata hujabadilika.
 
Lakini hilo gari linakua limeundwa hivyo ili kula hizo CC kwa umbali kadhaa, kwa hiyo unasema hata moyo wa mtu kuwa na matamanio fulani ni mungu anakua ameumba hivyo tangia mwanzo?
 
Lakini hilo gari linakua limeundwa hivyo ili kula hizo CC kwa umbali kadhaa, kwa hiyo unasema hata moyo wa mtu kuwa na matamanio fulani ni mungu anakua ameumba hivyo tangia mwanzo?
Hilo gari limeundwa ni mashine halina utambuzi, nimelitumia tu kama mfano uone katika kipengele cha kufahamu jambo kutokana na sifa za hilo jambo. Sifa za cc kubwa ni kula mafuta sijaongelea uhusika wa uumbaji wake.

Binadamu ana uhuru wa kuchagua ila chaguzi zina maandalizi. MUNGU anayaona maandalizi ndipo anajua utakachokifanya.
 
Uwezo wa mungu usiulinganishe na WA Binadamu.
 
Reactions: Tsh

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…