Mungu awe nanyi vigogo wa HESLB

Mungu awe nanyi vigogo wa HESLB

Majina ya waliopata mkopo kwa wanafunzi wanaondelea namaanisha mwaka wa pili na watatu bado hayajatoka kwa vyuo vyote .kwahiyo uwasiliane na loan officer wa hapo udom ili ujue hayo majina yakiwasili chuoni kwako
 
Pole sana. Ww fanya kila unaloweza ili imfikie Magufuli utapewa double
 
Bonge la ushauri mkuu ila nasikia pale bodi wanamajibu ya kunya sana hawa watu da Mungu anisaidie

Kama unaogopa kwenda bodi utakuwa huna shida.Shida huwa zinaleta ujasiri,unashangaa mtu umefika ofisi ambayo hukutegemeq
 
pole sana...ila usikate tamaa subiri majina ya mwaka wa pili yatoke unaweza ukawepo
 
Ni rahisi kumpata Magufuli kuliko Mkurugenzi wa bodi!!
 
Majina ya waliopata mkopo kwa wanafunzi wanaondelea namaanisha mwaka wa pili na watatu bado hayajatoka kwa vyuo vyote .kwahiyo uwasiliane na loan officer wa hapo udom ili ujue hayo majina yakiwasili chuoni kwako

Nimekuelewa mkuu nafurahi sana kwa ushauri mzuri nitaufanyia kazi endelea kunipa ujuzi zaidi.
 
Nenda Bodi,omba kukutana na Mkurugenz wa Loans alocation and disbursements anaitwa RAIZAR.. ukifika gateni..mwambie Raiza kaniambia nije..jifanye unafahamiana nae Tu..jamaa akikupa nafasi kukusikiliza..unapata mkopo,yupo floor 1..ofisi yake iko pembeni kulee katika kona
 
Mimi nataka kufa jamani nina miaka mitatu sasa nakosa boom, nahisi bora ningezaliwa nyani ulaya kuliko kuwa mtu Tanzania lnchi iliyojaa undugunization na rushwa hasa samaki wakubwa kama wafanyakazi wa HESLB mimi kama mwanafunzi ninayeendelea na masomo mwaka wa pili sasa na chuo wameshafungua(UDOM) ndugu zangu wanajukwaa ikumbukwe kuwa nilikuwa nasomesha na serikali toka kote nilikopita kwani me ni yatima na sina uwezo wa aina yoyote ile mwaka 2013 nilihitimu kidato cha sita na kufauru hivyo nikaaplay chuo mkopo nikakosa ikanilazim kuahirisha chuo mwaka uliofata nikaaplay tena nikapata chuo mkopo nikakosa tena education UDOM hivyo nilikuwa napiga tempo nikapata hela kidogo kwa ushauri nikaona nitazeheka nikaenda kuripoti chuoni nimeteseka sana ikafika sehemu nikaishiwa hadi chupi kwa maisha ya udom yalivyo magumu nimejikomba hadi mwaka ukaisha nimeomba mkopo tena jamani ndiyo hivo nashindwa nifanyeje jamani naomba ushauri wenu sina pakushika ndugu zangu na chuo ndiyo wanaendelea

pole ndugu
 
Inatia uchungu sana, ila mi nna wasiwasi kuna sehemu uli-mistaken wakati wa ku-apply mi siamini kama una sifa zote tajwa huwezi kosa mkopo.

Angalia je, vyeti vyako ulivyoambatanisha mwanzoni na kwa mara ya pili vyote vilikamilika? je, vilikuwa certified na wakili na kugongwa muhuri wa wakili? Uliweka picha? ya kwako na ya mzazi kote kwa mara zote ulivyo apply? Je, ulisign panapo stahili? Uliwasilisha form kwa wakati?Je kipindi walipotoa majina ya wanafunzi waliokosea ku-apply either kwa kutoweka kiambatanishi chochote uliyaangalia majina? je, jina lako halikuwepo kwa waombaji waliokosea? jiulize maswali mengi mengi mengi ni lazima kuna sehemu ulikosea tu. iwe kwa bahati mbaya au kwa uzembe.

Tofauti na hapo pole sana Mwenyezi Mungu akutangulie.
 
. Mkuu hayo yote nilizingatia tena kwa umakin zaid
 
Back
Top Bottom