Ombi kwa Rais Samia Hassan kuhusu HESLB kuondoa fedha za kujikimu wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field)

P Accountant

JF-Expert Member
Sep 26, 2020
369
169
Kwako Mheshimiwa:-

Lengo kubwa la ujumbe huu ni kukufahamisha juu ya HESLB kuondoa allocations za field kwa wanafunzi wa mwaka wa pili ambao hawakuwa na field mwaka wa kwanza. PASIPO KUTOA TAMKO LOLOTE HADI SASA.

Mheshimiwa,
Nikupe historia juu ya upangaji wa mkopo kwa wanafunzi wa chuo kikuu mnamo mwaka wa masomo 2020/2021. Bodi ya mkopo iliwapangia wanafunzi fedha za kujikimu wakati wa masomo yao kwa kuzingatia mahitaji ya kila mwaka wa masomo. Wakati huo wewe ukiwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Kwa wanafunzi ambao hawakuwa na mafunzo kwa vitendo (field) hawakupangiwa fedha za field kwa mwaka husika 2020/2021. Bali walipangiwa kwa mwaka wa masomo 2021/2022 kuwa watalipiwa fedha hizo wakati wa mafunzo kwa vitendo.

Mambo yamekuwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali, kwani allocations zimebadilika pasipo kutoa TAMKO LA MSINGI JUU YA MABADILIKO HAYO. Hadi napo andika hapa, wanafunzi wamefutiwa allocations za fedha za field na hawafahamu hatima yao juu ya fedha hizo wakati huu mwaka wa masomo ukiendea ukingoni kwa vyuo kama UDSM na UDOM.

Kwanini kuna mashaka zaidi?
Ikumbukwe kuwa sambamba na kutoa fedha za field, Bodi ya mkopo ilipunguza allocations za fedha za Ada ya masomo ambazo zilipaswa ziwekwe kwa mwaka wa pili wa masomo, LAKINI PIA HAKUKUWA NA TAMKO LOLOTE JUU YA JAMBO HILI. Kitendo kilichopelekea wanafunzi kuongezea fedha katika ada.

Mheshimiwa,
Kwa heshima sana, tunaomba TAMKO lako juu ya mabadiliko haya ambayo hayaleti taswira nzuri juu ya utendaji wa HESLB. Kwani wameshindwa kutoa maelezo ya msingi kwa wanufaika wa mikopo.

Tanzania yetu sote. Usawa na uwazi ni njia ya amani katika kuendesha taasisi.
 
Back
Top Bottom