Mungu anataka aabudiwe kupitia Masanamu?

Ni halali kuwepo masanamu katika nyumba za ibada,ambayo hayasikii wala hayana msaada wowote ule katika kumuomba Mwenyezi Mungu?
Hakuna sanamu ya Mungu wala yenye mfanano wake
 
Nimesha elezea maana ya imani ila,pia nimekusoma sana humu unapinga uwepo wa Mungu bila wewe kuthibitisha kua Mungu hayupo,

Hoja zako hua unajichanganya wewe mwenyewe,sasa huo mfano wa kipindupindu unahusikaje? Watu wakiamini Mungu na kufuata amri zake Dunia inakua ni sehemu salama,sasa kipindupindu kinahusikaje hapo?

Acha kuteseka,waache watu waamini wanachokiamini na wewe endelea na maisha yako,huwezi kuwapangia watu jinsi ya kuishi.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Uwepo wa Mungu huyo unapingwa na dunia tunayoiona inayoruhusu mabaya.

Mungu huyo angekuwepo, kusingewezekana kuwepo na baya lolote. Magonjwa, njaa, majanga ya asili yasingeweza kuwepo.

Ni hivi, kama Mungu huyo yupo, dunia inayoruhusu mabaya haiwezi kuwepo.

Dunia inayoruhusu mabaya ipo, hivyo, Mungu huyo hayupo.

Wewe una tatizo la kuelewa mifano na kufikiri kidhahania.

Kuamini Mungu yupo na ni jibu la matatizo ya watu ni imani potofu sawa na kuamini mavi ni dawa ya Covid-19.

Sasa wewe umeniuliza, watu baki wakiamini Mungu yupo, mimi napungukiwa nini?

Na mimi nakujibu.

Hao watu wanaoamini Mungu wananitungia mimi sheria za maisha yangu kutokana na imani yao potofu.

Unakwenda sehemu, unataka kula, unaambiwa hapa usile kwa sababu mwezi wa Ramadhani.

Unataka kunywa kinywaji unachotaka, unaambiwa huruhusiwi kunywa kinywaji ni haram.

Unataka kupumzika bila kelele, unapigiwa kelele kutoka msikitini na kanisani.

Unataka kuishi kwenye Jamhuri isiyofuata dini, kila kitu kinaongozwa na dini ya Mungu wa uongo.

Sasa hapo utasemaje kwamba watu wakiamini Mungu mimi inanipunguzia nini?

Hawa ni watu wanaokula mavi na kuamini ni dawa ya Covid-19.

Wanasambaza ujinga wao na maradhi dunia nzima.

Halafu unasema mimi hilo linanipunguzia nini wakati wakila mavi wao kipindupindu kinaenea mpaka kwangu?
 
Kukataa kuwa Mungu hayupo ni kuamini kivipi?

Unaelewa hapa ni kama umesema kunyoa nywele ubaki na upara ni mtindo wa kusuka nywele pia?

Thibitisha Mungu yupo.
Mungqau ni roho,Mungu anafanana na mwanadamu mme ni mfano wa Mungu.
Roho huwezi uthibisha kwa elimu ya macho ya nyama.Mtu Ili akamalike ana sehemu tatu mwili,roho na nafsi.Nafsi na roho vikitoweka kwa mtu uhai unakoma,mtu Ili anakufa baada ya roho kuacha mwili.Roho ukaa ndani ya mwili, uthibisho wa roho ni uhai, Hakuna uhai Hakuna roho. So Mungu ndie chanzo cha uhai, kama uhai upo na Mungu ndie chanzo kwann usiamini yupo
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Uwepo wa Mungu huyo unapingwa na dunia tunayoiona inayoruhusu mabaya.

Mungu huyo angekuwepo, kusingewezekana kuwepo na baya lolote. Magonjwa, njaa, majanga ya asili yasingeweza kuwepo.

Ni hivi, kama Mungu huyo yupo, dunia inayoruhusu mabaya haiwezi kuwepo.

Dunia inayoruhusu mabaya ipo, hivyo, Mungu huyo hayupo.

Wewe una tatizo la kuelewa mifano na kufikiri kidhahania.

Kuamini Mungu yupo na ni jibu la matatizo ya watu ni imani potofu sawa na kuamini mavi ni dawa ya Covid-19.

Sasa wewe umeniuliza, watu baki wakiamini Mungu yupo, mimi napungukiwa nini?

Na mimi nakujibu.

Hao watu wanaoamini Mungu wananitungia mimi sheria za maisha yangu kutokana na imani yao potofu.

Unakwenda sehemu, unataka kula, unaambiwa hapa usile kwa sababu mwezi wa Ramadhani.

Unataka kunywa kinywaji unachotaka, unaambiwa huruhusiwi kunywa kinywaji ni haram.

Unataka kupumzika bila kelele, unapigiwa kelele kutoka msikitini na kanisani.

Unataka kuishi kwenye Jamhuri isiyofuata dini, kila kitu kinaongozwa na dini ya Mungu wa uongo.

Sasa hapo utasemaje kwamba watu wakiamini Mungu mimi inanipunguzia nini?

Hawa ni watu wanaokula mavi na kuamini ni dawa ya Covid-19.

Wanasambaza ujinga wao na maradhi dunia nzima.

Halafu unasema mimi hilo linanipunguzia nini wakati wakila mavi wao kipindupindu kinaenea mpaka kwangu?
Bila matatizo na changamoto Hakuna maendeleo. Hio dunia isiyo na shida na matatizo yote hayo uliyoyasema ipo ni zawadi kwa watakatifu siku za mwisho baada ya hukumu. Uamuzi ni wako uende kuzimu au peponi.
 
Mungqau ni roho,Mungu anafanana na mwanadamu mme ni mfano wa Mungu.
Roho huwezi uthibisha kwa elimu ya macho ya nyama.Mtu Ili akamalike ana sehemu tatu mwili,roho na nafsi.Nafsi na roho vikitoweka kwa mtu uhai unakoma,mtu Ili anakufa baada ya roho kuacha mwili.Roho ukaa ndani ya mwili, uthibisho wa roho ni uhai, Hakuna uhai Hakuna roho. So Mungu ndie chanzo cha uhai, kama uhai upo na Mungu ndie chanzo kwann usiamini yupo

Roho yenyewe nayo ni uongo tu.

Unatumia uongo mmoja kutetea uongo mwingine.

Na mimi sijakutaka uthibitishe kwa elimu ya macho na nyama.

Sasa umejizidishia maswali.

1. Thibitisha roho ipo na habari za uwepo wake si uongo tu.

2. Thibitisha Mungu yupo na habari za uwepo wake si uongo tu.
 
Ibrahimu ni baba wa manabii kwani kizazi chake ndicho kilichotoa mitume yote iliyobaki,tokea utoto wake alikuwa akiyachukia hayo Masanamu kwani alishangaa vipi wanaabudu mawe ambayo wanayachonga wenyewe na ambayo hayawezi kumdhuru au kumfaa mtu na chochote
 
Bila matatizo na changamoto Hakuna maendeleo. Hio dunia isiyo na shida na matatizo yote hayo uliyoyasema ipo ni zawadi kwa watakatifu siku za mwisho baada ya hukumu. Uamuzi ni wako uende kuzimu au peponi.
Mungu alishindwa kuumba dunia hii iwe ambayo ina changamoto lakini haina matatizo?

Mbona watu wametengeneza video games zina changamoto lakini haziui watu, hazileti matetemeko ya ardhi etc?

Hiyo dunia ambayo unasema ipo ni zawadi unaweza kuthibitisha ipo kweli na si hadithi za uongo tu?
 
Roho yenyewe nayo ni uongo tu.

Unatumia uongo mmoja kutetea uongo mwingine.

Na mimi sijakutaka uthibitishe kwa elimu ya macho na nyama.

Sasa umejizidishia maswali.

1. Thibitisha roho ipo na habari za uwepo wake si uongo tu.

2. Thibitisha Mungu yupo na habari za uwepo wake si uongo tu.
Unajua kuhusu ndoto, mawimbi ya radio, umeme, ukiweza vijua hivi hata nikukupa shule Roho,Mungu huwezi elewa.Mungu sio physical object
 
Ukute mwandishi ndo huwa anakesha kwenye mbio za mwenge
 
Nisaidieni kale Kadubwana kanakowekwa mbele wakati wa Sala za jumuia ni Sanamu au laa!!! Total hua sikaelew
 
Ibrahimu ni baba wa manabii kwani kizazi chake ndicho kilichotoa mitume yote iliyobaki,tokea utoto wake alikuwa akiyachukia hayo Masanamu kwani alishangaa vipi wanaabudu mawe ambayo wanayachonga wenyewe na ambayo hayawezi kumdhuru au kumfaa mtu na chochote
Acha kuabudu mwenge kipindi cha mbio za mwenge.
 
Kutoka 20:4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
Kutoka 20:5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

Hapa ndipo penye majibu ya swali lako

Hakuna umuhimu wa kuto kuwepo maana hayana msaada wowote katika kuwasiliana na Mungu kwasababu

Mungu anaabudiwa katika Roho na kweli
Unayajua makerubi wewe? Umewasikia malaika wewe? Wote hao kwa namna moja au nyingine Mungu alitoa maagizo sanamu zao ziwepo. Walikuwepo pia katika sanduku la Agano
 
Nisaidieni kale Kadubwana kanakowekwa mbele wakati wa Sala za jumuia ni Sanamu au laa!!! Total hua sikaelew
Mafuta ya Mwamposa unayaelewa? Sanamu ya mwezi kwenye msikiti unaielewa? Sanamu ya mwenge wa uhuru je? Sanamu ya nyoka kwenye nembo za hospitali?
 
Mungu alishindwa kuumba dunia hii iwe ambayo ina changamoto lakini haina matatizo?

Mbona watu wametengeneza video games zina changamoto lakini haziui watu, hazileti matetemeko ya ardhi etc?

Hiyo dunia ambayo unasema ipo ni zawadi unaweza kuthibitisha ipo kweli na si hadithi za uongo tu?
Sayansi haina uwezo wa kuthibitisha uwepo wa Mungu.Bali elimu ya mambo ya kiroho
 
Roho nayo huwezi kuthibitisha ipo.

Ni uongo kama uwepo wa Mungu.

Kimsingi unatumia uongo mmoja (uwepo wa roho) kama kichaka cha kufichia uongo mwingine (uwepo wa Mungu).

Badala ya kujibu swali moja, umejiongezea maswali na kuyafanya yawe mawili.

1. Thibitisha roho ipo.

2. Thibitisha Mungu yupo.
 
Unajua kuhusu ndoto, mawimbi ya radio, umeme, ukiweza vijua hivi hata nikukupa shule Roho,Mungu huwezi elewa.Mungu sio physical object
Kwani nani kasema Mungu ni physical object?

Ndoto, mawimbi ya radio, umeme, vyote hivi vinapimika.

Roho na Mungu ni hadithi tu. Ndiyo maana havipimiki.
 
Ni halali kuwepo masanamu katika nyumba za ibada,ambayo hayasikii wala hayana msaada wowote ule katika kumuomba Mwenyezi Mungu?

Acha uvivu wa kusoma biblia ! Mambo mengine mpaka utakufa, hutokaa uyajue simamia imani yako unayoamini.
 
Back
Top Bottom