Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Austronomy

Member
Jun 27, 2024
14
45
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
 
Unaposema MUNGU aliona wapi mfano wa dunia ndipo akaumba, hivi unamfananisha BWANA MUNGU na Mwanadamu?

Umekosa akili, umekosa adabu kwa MUUMBA wako kiasi unaona hawezi kufanya chochote mpaka kwanza awe ameona?

Na kama mpaka aone kwanza, unataka kusema yupo mwingine aliye mkuu kumzidi YEYE?

Kijana kuwa na adabu kwa MUUMBA wako. Usifikie hatua ya kumdharau MUNGU kuwa hawezi kutenda, hawezi kuumba mpaka awe ameona kwanza.
 
Ndiyo maana anaitwa MUNGU ni cheo Cha ngazi ya juu kuliko vyote kwenye muundo wa maisha na uhai kabla na baada ya maisha haya.

Uwezo wa fikra zetu na utambuzi haviwezi kueleza bayana kuhusu sifa, uwezo na hali ya MUNGU.

Kumjua MUNGU linabaki fumbo asilia linalohitaji mlango wa Imani pekee Ili uwezakano huo uwepo.

Yeyote anayetumia ishara bayana kutaka kumjua MUNGU hataweza kwa maana MUNGU hayupo katika ulimwengu wa macho haya bali kiroho.

Tunapaswa kujali matokeo Bora ya MUNGU wetu katika maisha yetu kuliko kumpima uwezo wake ambao kamwe hauwezi kubainika kwa akili zetu finyu
🙏🙏🙏🙏🙏
 
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Ilimpendeza hivyo
 
Kutaka kujua mfano kautoa wapi huko ni mbali unajikomaza.

Unachotakika kujua hilo neno au Concept "MFANO" yeye ndio aliliumba na kuliwekea huo utaratibu ambao wewe Leo unauzungumia hapa.

Angeamua Concept ya MFANO isiwepo pia wala usingekua hata na Idea kwamba kuna kitu kinaitwa kugelezea mfano.

IN SHORT: MUNGU NI YUPO VERY COMPLEX UNAFOSI KUMJUA KWA SIMPLE INTELLIGENCE AMBAZO AMEKUWEKEA YEYE MWENYEWE.

NISAWA NA MFUMO MZIMA WA INTERNET UNAOSHIKILIA MAELFU YA WEBS, APPS, SAAS, SOFTWARES then itokee kama Web kamoja kama Jamiiforums kianze kuhoji HOW INTERNET INA WORK LIKE BUTTONS ZAKE ZIKO WAPI, INA SEHEMU YA KUSHEA UZI....kwamba JF inajiuliza maswali kuhusu Internet kwa uwelewa wake wa kujijua yeye JF alive hatojua iyo Internet inauwezo wa kutuma pesa na kupokea wala haiwezi jua hio pesa nini nini.

Uelewa tulionao ni sawa na hako kaduara kadogo hapo ambao uwelewa wenyewe umejifunga kujua yaliyo ndani ya hako Kaduara, unachofanya unataka kutumia uwelewa huo mdogo tena uliojufunga kujua kitu ambacho kikubwa kuliko huo mduara mkubwa hapo lazima uwe CONFUSED.
images (1).jpeg
 
Hata kwa upande wetu wanadamu kama kila kitu kingetokana na mfano wa ambacho kipo basi kusingekuwako mageuzi ya aina yoyote. Nani aliona mfano wa hivi vitu kisha akavitengeza; electric bulb, nuclear bombs, transistor au hata LLMs kama ChatGPT.
Kama kwa ngazi ya wanadamu ipo hivyo, basi kwa ngazi ya juu ni zaidi
 
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Yasiyowezekana kwa Mwanadamu (Mtu), kwa Mungu yanawezekana!
 
Swali lako halina mashiko, labda uwe unamtizamo/ufahamu tofauti kuhusu Mungu.

Hata hizi ramani tunazotumia nani amezisanifu? Sasa kama mwanadamu anazisanifu Mungu ndio wakumtilia mashaka,

Uumbaji ulikua ni udhihilisho wa kile kilichokuepo tayari, kuto kuonekana kwa kitu haimaanishi kua hiko kitu hakipo.

Mungu ni mwingi wa maono, na kila kitu kilianza kama maono katika fikra za mtu... Kwanza mtu anakua na maono => baadae linakua wazo=>ndipo inapatikana taswira halisi ya kitu => kazi inabakia katika utekelezaji kuunda kitu hicho.

Yote ya yote
🔘Mungu ni Mjuzi wa yote (omniscient),

🔘Mungu ni yupo mahali popote ulimwenguni (Omnipresent)

🔘Mungu ni mwenye (nguvu) UWEZA mkuu wakati wote (Omnipotent).
 
Samahan,labda sikuwa specific.

Hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, na siyo wasio amini.
Hapa ni open forum jukwaa la wote.

Ukishaweka mada yako hapa ujue kwamba kila mtu yupo huru kuchangia.

Hapa sio kanisani wala msikitini kwamba unataka kusikia majibu ya imani yako ilivyo kuaminisha.

Vinginevyo imani yako ya huyo Mungu ungebaki nayo moyoni mwako na sio kuileta hapa.
 
HIvi unajua maana ya swali kuwa specific ?

Kumbe nikupe mfano wa pili : Tanzania ni nchi ya ulimwengu wa tatu, nataka kujua kwanini tanzani ni masikini.

Wewe unakuja kwanza kukanusha kuwa tanzania siyo nchi ya ulimwengu wa tatu, hapa swali lazima kwanza lijibiwe na watu walio na mtazamo kuwa tanzania ni nchi ya ulimwengu wa tatu ndiyo watatoa sababu za kwanini ni maskini.

Ila wewe ambae hujakubali kuwa tanzani iko kundi la nchi za ulimwengu wa tatu huwezi kujibu swali hili maana utakosa sifa za kujibu.
 
Umeuliza swali gumuu!
Ila linaweza kuwa na majibu labda mkuu.

Kumbuka kauli hii ya kwenye biblia "na tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu, kwa mfano wake Mungu aliwaumba mwanamke na mwanamke"

Hii huenda Mungu alijiangalia yeye alivyo ndiyo akatuumba sisi (wanadamu) kwa kujiangalia yeye kama mfano.

Je, kwenye universe aliangalia wapi akaona aumbe universe ikiwa na umbo hili.
 
HIvi unajua maana ya swali kuwa specific ?

Kumbe nikupe mfano wa pili : Tanzania ni nchi ya ulimwengu wa tatu, nataka kujua kwanini tanzani ni masikini.

Wewe unakuja kwanza kukanusha kuwa tanzania siyo nchi ya ulimwengu wa tatu, hapa swali lazima kwanza lijibiwe na watu walio na mtazamo kuwa tanzania ni nchi ya ulimwengu wa tatu ndiyo watatoa sababu za kwanini ni maskini.

Ila wewe ambae hujakubali kuwa tanzani iko kundi la nchi za ulimwengu wa tatu huwezi kujibu swali hili maana utakosa sifa za kujibu.
Utajibuje swali ilhali huyo Mungu anayesemwa yupo kiuhalisia hayupo?

Inabidi kwanza huyo Mungu anayedaiwa kwamba yupo, athibitishike kwanza yupo kisha ndiyo maswali mengine ya namna gani aliumba dunia yafuate.

Vinginevyo, Kama huwezi kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu huwezi kusema kwamba Mungu huyo ndio aliumba dunia.

Yani unarukia maswali ya mbele ilhali uwepo wa huyo Mungu ni imani tu zisizo na uthibitisho wowote ule!!
 
Unaposema MUNGU aliona wapi mfano wa dunia ndipo akaumba, hivi unamfananisha BWANA MUNGU na Mwanadamu?

Umekosa akili, umekosa adabu kwa MUUMBA wako kiasi unaona hawezi kufanya chochote mpaka kwanza awe ameona?

Na kama mpaka aone kwanza, unataka kusema yupo mwingine aliye mkuu kumzidi YEYE?

Kijana kuwa na adabu kwa MUUMBA wako. Usifikie hatua ya kumdharau MUNGU kuwa hawezi kutenda, hawezi kuumba mpaka awe ameona kwanza.
SIkuwa na maana hiyo uliyo itafsiri wewe.

Biblia inasema "na tumfanye mtu kwa sura yetu na kwa mfano wetu, kwa mfano wa Mungu aliwaumba mwanamke na mwanamume"

Kuna uwezekano Mungu kutuumba binadamu hivi tunavyoonekana leo ni kwa sababu alijiangalia yeye akaona a-design kitu cha kufanana na yeye.

Sasa ulimwengu mzima na vingine aliona mahali labda ndiyo maana akaamua kuu-design hivi ulivyo leo.
 
Utajibuje swali ilhali huyo Mungu anayesemwa yupo kiuhalisia hayupo?

Inabidi kwanza huyo Mungu anayedaiwa kwamba yupo, athibitishike kwanza yupo kisha ndiyo maswali mengine ya namna gani aliumba dunia yafuate.

Vinginevyo, Kama huwezi kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu huwezi kusema kwamba Mungu huyo ndio aliumba dunia.

Yani unarukia maswali ya mbele ilhali uwepo wa huyo Mungu ni imani tu zisizo na uthibitisho wowote ule!!
Ndiyo maana sijaamua kulenga wasio amini Mungu kama wewe.
Ningeamua kuwa lengo wote ningekuja na thread hapa "Mungu hayupo au yupo" na wewe ungepata side ya kusimama na uthibitisho wako.

Nakushauri tu : Kuingiza logic and reasoning kwenye mambo ya imani/kiroho/yasiyoonekana kimwili lazima utoke mtupu.

Ndiyo wewe hapo.
 
Back
Top Bottom