Mume bora mwenye hekima na busara ni huyu hapa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
51,636
23,072
CHRISTINA SHUSHO AMEMKOSEA MUMEWE, ATUBU

Kitendo cha Christina Shusho kusema kwamba aliozeshwa akiwa mdogo bila idhini yake ni kumdhalilisha huyo aliyekuwa mume wake kwamba alikuwa mkubwa sana kwake (mzee) na alimuoa kimabavu, kwanini hakuachana nae kipindi hicho hicho au kwenda kushtaki? Au kuna kitu alikuwa anapata hakipo tena ndio anaamua kumchafua? Maswali ni mengi yenye mashaka.

Nimeona video anahojiwa hata pete ya ndoa hajavaa anaulizwa kwanini anasema ni suala la makubaliano aliamua kumuacha mumewe kwenda kutimiza ndoto zake na ilikuwa kwa amani anasema habari za mume na mke kuwa mwili mmoja kwake siku hizi hazipo. Kule kwa mumewe alipokuwa anasema akiamua anaenda kutembelea tu. Hii sio sahihi ndugu zangu.

Imefika hatua anasema kwamba hapendi kuitwa pastor Christina Shusho anasema yeye sio mchungaji ila ana watu wa karibu wachungaji yeye hajiskii vizuri kuitwa pastor, kweli? Muimbaji wa nyimbo za Injili unaehubiri kupitia nyimbo hutaki kuitwa mchungaji??? Unaogopa nini? Ni mambo gani hasa yanakupa aibu kuitwa pastor?

Binafsi nasimama na huyo mume, naona suala la ndoa la Christina Shusho limekaa upande mmoja yeye tu ndio anaongea kwenye media na majukwaa mbalimbali kwamba alifosiwa kuolewa mara alijitoa kwenye ndoa kutimiza maono yake nk ukweli unabaki kwa mume huenda nae ana mengi ya kuzungumza ila ana kifua, sio ropo ropo.

Nadhani siku huyo mzee (ambaye Christina anadai aliozeshwa kwake akiwa mdogo kwamba ni mkubwa sana kwake) akiongea huenda tukakosa pa kuficha sura zetu yanaweza kuwa mambo mazito mno

Nadhani mume ameamua kutumia busara kukaa kimya kuepusha taharuki kubwa zaidi

Sioni kama kulikuwa na haja ya Christina Shusho kuongelea haya mambo hadharani yalipaswa kuwa binafsi

Wanawake jifunzeni, mambo ya ndoa sio ya kuweka hadharani.
 
Past shushooo chr...
 

Attachments

  • 1714663466367.jpg
    1714663466367.jpg
    203.1 KB · Views: 4
Nlichogundua ni kwamba kuna ukweli flani kwamba ile ndoa yao ilikuwa ya kulazimishwa. Umri na kila kitu ni tofauti. Makanisa mengi ya kipentekoste wana tabia ya kuwaozesha mabinti wanaume wasiowahitaji, nao hukubali sababu wanawatii watumishi
Sad
 
We badala ya kuangalia maisha yako unafuatilia na ku judge ya watu.

Wachungaji wengi tu wanakula kondoo kwa kificho, wachafu tu, hata kama anaimba injili ni mtu kama sisi, kukataa kuitwa mchungaji kuna ubaya gani? Kukataa ndoa we inakuuma nini?

Anayekuwa ndoani ni yeye anafahamu changamoto anazokutana nazo, inawezekana hampendi huyo mume, ana kosa?

Nyie ndio wale wazazi wajinga mnalazimisha watoto wa kike kuolewa na mtu fulani kisa mihemko ya kidini na tamaa.

Hata akiamua kuimba bongo flavor kuna shida? Si maisha yake kachagua havunji sheria...
 
Nlichogundua ni kwamba kuna ukweli flani kwamba ile ndoa yao ilikuwa ya kulazimishwa. Umri na kila kitu ni tofauti. Makanisa mengi ya kipentekoste wana tabia ya kuwaozesha mabinti wanaume wasiowahitaji, nao hukubali sababu wanawatii watumishi
Naam kuna hili jambo la kulazimishiwa ambalo wazee huwa hawaliangalii, na ndoa nyingi za hivi huwa hazidumu
 
We badala ya kuangalia maisha yako unafuatilia na ku judge ya watu.

Wachungaji wengi tu wanakula kondoo kwa kificho, wachafu tu, hata kama anaimba injili ni mtu kama sisi, kukataa kuitwa mchungaji kuna ubaya gani? Kukataa ndoa we inakuuma nini?

Anayekuwa ndoani ni yeye anafahamu changamoto anazokutana nazo, inawezekama hamoendi huyo mume, ana kosa?

Nyie ndio wale wazazi wajinga mnalazinisha watoto wa kike na mtu fulani kisa mihemko ya kidini na tamaa.

Hata akiamua kuimba bongo flavor kuna shida? Si maisha yake kachagua havunji sheria...
Muheshimiwa hatugombani.Mama Samia ataongeza mishahara tu.Keep it calm!
 
Watu huwa wanasahau hili. Ni bonge la point
Tunaingia tu kichwakichwa…mambo inabidi yabalance…unampenda sawa je yeye anakupenda? Siyo umeona mali tayari unaolewa au kuoa…mali ni mali na upendo ni upendo….afu unachokikimbilia ni mwonekano tu wa nje ila upendo daima moyoni
 
Muheshimiwa hatugombani.Mama Samia ataongeza mishahara tu.Keep it calm!
Mambo mengine ni ujinga.
Inasikitisha kuona bado kuna wa Tanzania wapuuzi kiasi hiki.

Kwamba mtu akiimba injili aitwe mchungaji.
What's so special about uchungaji wakati wengine ni wazinzi na walevi wakubwa?

Mimi naishi kwa shemeji yangu ni bora hata ningalikuwa nimeajiriwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom