Mume wangu nimemchoka mpaka akinisogelea nasikia harufu ya chatu

Wanajamvi nin miaka 3 tu kwenye ndoa lkn nimemchoka mume wangu hatari. Akisogea karibu yangu nasikia harufu ya chatu na siyo ya binadamu.

Usiku huwa kuna muda nakosa usingizi kwa mawazo juu ya hili dubwana. Najutia kuwa na hili dubwana ktk maisha yangu.

The man is really caring. Juzi juzi nilikosa usingizi nikaamka nikawa nimekaa kitandani, namuangalia anavyo jigeuza geuza kitandani hadi nikaanza kulia kwa majuto. Alipoamka nikavunga kuwa tumbo linaniuma. Nikamuomba aniadalie uji.

Basi kwa haraka sana akaenda jikoni akaandaa uji na kuniletea.

Jamani nilipofikia naweza hata nikamlambisha sumu usingizini maana kwa kuwa ahajanikosea nikimuacha kutakuwa na drama nyingi sana toka kwa wazazi ndugu na majirani.

Kwa ufupi hajanikosea chochote lkn ni akili yangu tu ndiyo imemchoka mpk namsikia ananuka chatu.
Duh kama umerogwa vile ila pabaya patakua panakuita
 
Mkataa pema pabaya panamuita.Kuna kitu unakitafuta na hakika utakipata na hilo dubwana utakuja kulitafuta usilione.Huwa tunataka sana mapenzi ambayo tunayaona kwa wengine au kwenye sinema au maigizo alafu tunajifananisha nayo.Mapenzi huwa ukiwa na huyu unatamani ungekuwa na yule.Kuna wimbo upo youtube unaitwa MOYO HAUSEMEZEKI-SADIQ TAARAB PLIZ USIKILIZE.
Don't compare your life to others,comparison is the thief of joy.Tafakari mkuu.
 
Siku nyingine wa Kike, siku nyingine wa kiume


Hapa kabla hujawa wa kike
 
Umeolewa lini mpaka kufikia hatua kumchoka mumeo kiasi hicho wakati juzi tu ulikuwa unataka kughairi kuolewa sababu ya best man.
 
Kama huna mimba, basi wewe hufai na utakuwa na wanaume wengine kwahiyo uache uzinzi ijali ndoa baadaye utakuja kuikumbuka na kuililia
Asante kwa kauli. Ninao ushuhuda wa namna hii kwa jirani. Kwa sasa kila siku mke analia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom