Mume wangu na x-gf wake

Mom...charuka mapema...hakunaga mazoea ya kawaida ya watu waliokwishakuwa wapenzi....(ni wachache sana tena sana)utakuja ambiwa shetani alinipitia...mie nilifanya kabisa kumpigia cm, na nikamwambia kabisa cku nikikuta msg au calls zako humu nitakufungia safari, walianzaga hivi hivi, mara vi sms mara vi calls, mara cjui wanaagizia nini ukija huku uniletee mana huko ndio original,cjaonaga sms wala calls zake tena, ni wakati wa kila mtu kushika lake, ameolewa/ameoa sasa nini tena....

ni kweli nyamayao hata mi nimetel mr kwanza sifurahii na amwambie mom hataki tuzoeane tunapeana pressure zisizo na maana!
 
Jamani hii imenikumbusha maumivu niliyonayo mpaka sasa hivi, mume wangu anawasiliana kwa karibu sana na hawara yake na hata akigombana na mwenza wake mshauri wake ni mume wangu. inauma sana msisikie tafadhali ficheni wenza wenu wasijue! kama humpendi mwenzako ni bora umwambie aanze mbele kuliko kujifanya huwasiliani nae kumbe raha zenu kwa kwenda mbele! God forbid. Mungu awalaani wote na wafumaniwe siku moja laivu bila zengwe!
 
kibongo bongo ckubaliani nayo, inategemea mmeachanaje...

Hapa ofisini nina mabosi wangu wawili walikuwaga wapenzi huko chuo tena na mtoto wakazaa. Sasa hivi kila mmoja ana ndoa na mtu tofauti, lakini naona wako poa tu, huyu mama ndiye bosi mkuu akisafiri anamwachia X wake ofisi anakaimu. Na sijawahi kusikia hata tetesi za mapenzi baina yao, wanapiga kazi tu. Na wanayo maelewano mazuri ya kikazi. Mdogo wa bosi mkuu (mama) alifanyiwa send-off majuzi, na huyu x-wake alikuwa very active kwenye kamati. Ukosefu wa ustaarabu ni tabia binafsi, sio kila mtu yuko hivyo.
 
Jamani hii imenikumbusha maumivu niliyonayo mpaka sasa hivi, mume wangu anawasiliana kwa karibu sana na hawara yake na hata akigombana na mwenza wake mshauri wake ni mume wangu. inauma sana msisikie tafadhali ficheni wenza wenu wasijue! kama humpendi mwenzako ni bora umwambie aanze mbele kuliko kujifanya huwasiliani nae kumbe raha zenu kwa kwenda mbele! God forbid. Mungu awalaani wote na wafumaniwe siku moja laivu bila zengwe!

huo muda wanaupatia wapi kukaa na kushauriana yote hayo, wakimalizana kushauriana watataka kufarijiana....pweeehhh mie ctaki kabisa.
 
Hapa ofisini nina mabosi wangu wawili walikuwaga wapenzi huko chuo tena na mtoto wakazaa. Sasa hivi kila mmoja ana ndoa na mtu tofauti, lakini naona wako poa tu, huyu mama ndiye bosi mkuu akisafiri anamwachia X wake ofisi anakaimu. Na sijawahi kusikia hata tetesi za mapenzi baina yao, wanapiga kazi tu. Na wanayo maelewano mazuri ya kikazi. Mdogo wa bosi mkuu (mama) alifanyiwa send-off majuzi, na huyu x-wake alikuwa very active kwenye kamati. Ukosefu wa ustaarabu ni tabia binafsi, sio kila mtu yuko hivyo.

ebu nijaribu kuamini hayo yawezekana. sikatai wapo wachache waaminifu hivyo.
 
Hapa ofisini nina mabosi wangu wawili walikuwaga wapenzi huko chuo tena na mtoto wakazaa. Sasa hivi kila mmoja ana ndoa na mtu tofauti, lakini naona wako poa tu, huyu mama ndiye bosi mkuu akisafiri anamwachia X wake ofisi anakaimu. Na sijawahi kusikia hata tetesi za mapenzi baina yao, wanapiga kazi tu. Na wanayo maelewano mazuri ya kikazi. Mdogo wa bosi mkuu (mama) alifanyiwa send-off majuzi, na huyu x-wake alikuwa very active kwenye kamati. Ukosefu wa ustaarabu ni tabia binafsi, sio kila mtu yuko hivyo.

Mtu b nakuelewa....lakini ni wachache sana kwenye jamii yetu wanaiweza hiyo, wachache sana,nina mifao kama mi3....tahadhari ni muhimu.
 
huo muda wanaupatia wapi kukaa na kushauriana yote hayo, wakimalizana kushauriana watataka kufarijiana....pweeehhh mie ctaki kabisa.

Nyamayao unatuhukumu vibaya. Si kila mwanaume yuko hivyo. Mi japo sijaoa, nimewahi kuwa na girlfriends, wengine sasa wameolewa. Kiukweli akiniomba ushauri nitampa vizuri tu na nakuhakikishia sitamtaka naniliu yake maana kiukweli hata sijisikii, yaani atakuwa kama dada yangu tu.
 
Mumeo anakosea kabisa. Kwa nini unaendekeza udhalilishwaji wa namna hiyo? Hivi wewe huna wako wa zamani? Kama huna tafuta na wewe rafiki mpya atakayekuwa anakushauri, kukusikiliza ukitaka sikio la kukusikiliza, na bega la kuinamia endapo utalihitaji. Au huwezi kufanya hivyo?

Kwa mengine zaidi niPM

hapana hapana, hapo ndio unaharibu kabisa
 
Mtu b nakuelewa....lakini ni wachache sana kwenye jamii yetu wanaiweza hiyo, wachache sana,nina mifao kama mi3....tahadhari ni muhimu.

Hawa mabosi wangu kwa kweli huwa nawachukulia kama role models wangu maana licha ya kuwa nao katika profession moja, nimepitia pia maisha hayo ya kupata girlfriends na kuachana nao na ningependa wawe marafiki zangu wa kawaida, sitaki kuishi maisha ya hofu kuwa nikionekana nasalimiana na x wangu watu waanze kunifikiria kuwa nataka kukumbushia na mambo kama hayo. Hawa walipata hadi mtoto lakini hawakumbushii. Kwa nini hutaki kuamini kuwa inawezekana kutokumbushia?
 
ahh nyamayao bwana ni haya matatizo tu MPAKA YANAMFANYAGA BUBU KUONGEA....!!!!

mie nasemaje, kama mr kutaka kucheza rafu achezee hukoo mbali, ishu za kutaka kupasha kiporo hamnaga, kusanifiana tu huko !...cku hizi ananiogopa kidogo, wakati ule akituma vi sms vyake nikampandia hewani nikamwambia ujue mie nakujua wewe vizuri, cku nikikufungia safari ujue nakuharibia kabisa kwa mumeo soooo plz tulia kabisa na ndoa yako, tukaja kukutana supermarket nilijishtukia tu nimemkata jicho la ki naija....hakurudia tena...nani anataka kusanifika hadharani?
 
Mom...charuka mapema...hakunaga mazoea ya kawaida ya watu waliokwishakuwa wapenzi....(ni wachache sana tena sana)utakuja ambiwa shetani alinipitia...mie nilifanya kabisa kumpigia cm, na nikamwambia kabisa cku nikikuta msg au calls zako humu nitakufungia safari, walianzaga hivi hivi, mara vi sms mara vi calls, mara cjui wanaagizia nini ukija huku uniletee mana huko ndio original,cjaonaga sms wala calls zake tena, ni wakati wa kila mtu kushika lake, ameolewa/ameoa sasa nini tena....

Hapo ndio huwa nakuheshimu sana Da Nyamayao,

You ara a no nonsense soldier! Kwa nini watu walete mzaha kwenye mambo yanayogusa hisia na uhai wa wenzao. Mie sitaki kusikia hata siku moja. Ila ukweli uko pale pale, a phone call of your X is so sweet! La muhimu ni kukinga mapema kuliko kuja kuhangaika na tiba!

Retired Maj Gen DC (1947)
 
Hawa mabosi wangu kwa kweli huwa nawachukulia kama role models wangu maana licha ya kuwa nao katika profession moja, nimepitia pia maisha hayo ya kupata girlfriends na kuachana nao na ningependa wawe marafiki zangu wa kawaida, sitaki kuishi maisha ya hofu kuwa nikionekana nasalimiana na x wangu watu waanze kunifikiria kuwa nataka kukumbushia na mambo kama hayo. Hawa walipata hadi mtoto lakini hawakumbushii. Kwa nini hutaki kuamini kuwa inawezekana kutokumbushia?

naamini lakini kwangu tahadhati muhimu kwani pia ya kupasha kiporo nimeyaona mengi sana kuliko hayo ya ma boc zako...na mie mwenyewe nina X ambae ameoa/nimeolewa lakini hachoki kuataka kukumbushia...soo kwangu tahadhari ni muhimu.
 
Huyu wa kwako sio mstaarabu, kumbe basi ndiye amesababisha wote tuhukumiwe vibaya. Wengine hatuko hivyo, nakuhakikishia Nyamayao.
 
sihitaji msaada wa x wangu maana yupo available sana kama ningemhitaji. ni hivi najisikia wivu x wa mume wangu anavyomganda kwa sababu binafsi nisingependa kuzoeana na x wangu kihivyo, nikihitaji ushauri mume wangu ni mshauri wangu wa kwanza!

Umeona Mom,

Kwa mwenzio mume wako ndiye mshauri wake wa kwanza. Kama hamjagawana kihampa hapo mmmmmhhhhh, sikubali kuitwa Tomaso!

Retired Maj Gen DC (1947)
 
Hapo ndio huwa nakuheshimu sana Da Nyamayao,

You ara a no nonsense soldier! Kwa nini watu walete mzaha kwenye mambo yanayogusa hisia na uhai wa wenzao. Mie sitaki kusikia hata siku moja. Ila ukweli uko pale pale, a phone call of your X is so sweet! La muhimu ni kukinga mapema kuliko kuja kuhangaika na tiba!

Retired Maj Gen DC (1947)

hayo mambo ndio nicyoyataka sasa/cyapendi kabisa....cku nilipom call huyo X nilim call kupitia cm ya mr, unajua alivyochekelea?.."hallow sweet, nilikumiss sana" alopockia namwambia huongei na sweet wako unaongea na mama mtoto alikata cm kwa shock, nilimtumia sms nikamwambia nakucall na plz pokea cm yangu tuongee kiutu uzima na ucjaribu kukata call yangu....sweet my foot...Mom gangamala.
 
Jamani najisikia wivu sana huyu x anavyozoeana na mume wangu, ameolewa ana mtoto, akihitaji ushauri lazima amconsult mr kwanza, hata kuapply kazi mr amsaidie kuandika barua. Ni wivu tu unanisumbua jamani

MOM,
Kwani haumwamini Mwenza wako? Inawezekana ukawa uhusiano wa kawaida, japo napata shida sana ilikuwaje mkafahamiana na x wake?, kwani mnaishi jirani? Hapa kuna kitu kimoja ambacho kinaendelea nacho ni kuwa, Hawa watu bado wana very Strong Tie, Kuna wakati niliwahi kuwa na wakati mgumu sana nilivyoendekeza ukaribu na X wangu,Kwangu sikuona taabu , na kwasababu nilishakuwa mtumishi nilimfahamisha na mwanzoni alinielewa, Lakini baadaye ilikuwa vigumu sana kukubali hali halisi,nilikuwa namfanyia vitu vingi sana, likitokea tatizo lolote nilikuwa wa kwanza kufahamishwa, Nilipoona mambo yanataka kuvuka mpaka niliacha kumwendekeza, mpaka sasa nimeshasau kabisa, hata nikiona Call yake au SMS sihipi umuhimu kiviiile.Mwambie Mwenzio kuwa hiyo hali uhipendi , ataacha tu.
 
Mtafute huyo X wa mumeo na uongee naye kujua ukweli kuliko kuumia moyoni!
 
Nyamayao unatuhukumu vibaya. Si kila mwanaume yuko hivyo. Mi japo sijaoa, nimewahi kuwa na girlfriends, wengine sasa wameolewa. Kiukweli akiniomba ushauri nitampa vizuri tu na nakuhakikishia sitamtaka naniliu yake maana kiukweli hata sijisikii, yaani atakuwa kama dada yangu tu.

Kumbe hujaoa???

Basi ngoja nikueleze.....Kwetu sisi tuliooa, Ex GF ni mtu wa kukaa naye mbali sana kwani ukitaka bailojia unajikulia tu kama soda kwenye friji. Kwa hiyo inabidi kukaa mbali ili mume wake asije kukuchinja. Uzoefu wangu na wenzangu uko hivyo.

Ndo maana nikasema huko nyuma kuwa kuna wakati EX GF akikupgia simu tu, akili inavurugika mpaka unatamani kwenda home kulala. Dawa ni kumwomba atulie na mume wake hata kama hampendi na wewe kujizuia kuanzisha tamthiliya ya aina yoyote. Ni mambo mazito sana. Kama wapo wachache waliomudu basi tuwaache. Ila wengi wetu lazima tuchukue tahadhari.
 
hiyo anayofanya mme wake ni dharau sana huwezi kuwa unamweka karibu mtu ambaye alikuwa nae zamani kimapenzi kama mshauri wako ktk maisha wanakuonea tu wewe mdada kwa kuwa naona wamekuona hushtuki kirahisi. Huwezi kufanya kitu kama hiki kwa mwenza wako kwa kuwa na wewe mfano ukifanya hivyo kama anavyofanya kwa X wako atajisikia vp. Jaribu kufanya kama alivyofanya Nyamayao inaweza kukomesha hiyo kitu milele daima
 
Back
Top Bottom