Mkuu,
Tupo matabaka mengi, hasa bongo hii. Kuna wanaweza kufanya bajeti ya mwezi na kuweka kila kitu mezani, mama atajua mwenyewe(kina nyie).
Kuna wanafanya bajeti, baba ananunua vitu kila mara na kumletea mama, haiachwi mia home.(kina wao).
Kuna wanaonunua kila siku kwa kuacha kodi ya mezani kutokana na kilichpatikana jana, kama nilipiga dei nikapata 15k, nampa mama 10k nabaki na 5k kibaruani(kina sie).
Kwa ground mambo sio rahisi namna hiyo.
Nakua

Mkuu nakuelewa, na ni kweli Maisha yana tabaka , ila Sasa Mkuu, ndio kwamba Ndani ya nyumba kikosekane kitu mpaka Usipoacha Hela , Basi wanafamilia walalamike ??
Mimi nakua, Mzee wetu alikua anahakikisha Amenunua Mchele kilo za kutosha , Unga wakutosha ( Ule wa kusaga wenyewe ) , Maharage, na mazaga yote yote ambayo hayaharibiki mafuta ya kupikia alinunua Ndoo ndoo , atanunua Chumvi pakiti za kutosha mwezi, atanunua Sukari ya kutosha ,Unga wa ngano , n.k
Atahakikisha kwenye Friza Kuna Nyama kilo Kadhaa, Samaki wabichi sato Kila Kadhaa n.k
Alafu Masuala ya Hela Kwa ajili ya Mengineyo anamalizana na Mke wake ...hapo ndo kama Leo mnataka Mle Ndizi, Sijui Tambi, na kubadilisha badilisha .
Hii kitu nimeibeba Mwenyewe, maana hata utokee umekwama, mambo yameingiliana, unakua na uhakika wa Chakula Ndani hata kama umetembelewa na Ndugu, Rafiki, jamaa.
Na Wife anajua, Nilishamwambiaa, Sitaki kwenye Chakula ulete Bajeti za kichoyo,in fact Moja ya Sababu Kumuacha mwanamke ,kwangu Mimi ni Suala la Chakula.
Nitoe Rai tu, Pamoja kwamba Maisha yetu yanahitaji utoe ulichopata Jana kwaajili ya Leo, Ni vema Kuhakikisha Ndani una Akiba ya Chakula, kuanzia Mafuta mpaka Dona.