Mume wangu hataki kuacha hela ya matumizi

miss chuga

JF-Expert Member
Dec 25, 2019
303
651
Habari zenu?

Poleni na majukumu ya kila siku, swali langu ni kwamba je ni sahihi mwanaume kutokuacha hela ya matumizi nyumbani? Binafsi nina miezi miwili toka nifungue biashara ya mgahawa hata bado haijachangamka ila toka nifungue Mume wangu hataki kuacha hela ya matumizi kama mwanzo wakati mtaji wenyewe alikataa kunipa, nimekopa sahivi nina kazi ya kulipa madeni na kulisha familia, tuna mtoto mmoja.

Kwakweli hili swala linaniumiza sana akili, nikimuuliza anadai hali ni ngumu hana hela wakati kabla sijaanza hii biashara alikuwa kila asubuhi anaacha elfu 10 mezani. Naombeni msaada wenu vipi hili Jambo ni sahihi au siyo sahihi?
 
habari zenu? poleni na majukumu ya kila siku, swali langu ni kwamba je ni sahihi mwanaume kutokuacha ela ya matumizi nyumbani? binafsi nina miezi miwili toka nifungue biashara ya mgahawa hata bado haijachangamka ila toka nifungue Mume wangu hataki kuacha...
Njoo nkupe
 
habari zenu? poleni na majukumu ya kila siku, swali langu ni kwamba je ni sahihi mwanaume kutokuacha ela ya matumizi nyumbani? binafsi nina miezi miwili toka nifungue biashara ya mgahawa hata bado haijachangamka ila toka nifungue Mume wangu hataki kuacha ela ya matumizi kama mwanzo wakati mtaji wenyewe alikataa kunipa nimekopa sahivi nina kazi ya kulipa maden na kulisha familia tuna mtoto mmoja, kwakweli hili swala linaniumiza Sana akili nikimuuliza anadai hali ni ngumu hana ela wakati kabla sijaanza hii biashara alikuwa kila asubuhi anaacha elfu 10 mezani. Naombeni msaada wenu vipi hili Jambo ni sahihi au siyo sahihi?
Thread 'USHAURI: Simuelewi mume wangu' USHAURI: Simuelewi mume wangu
 
Pambana, nyie wanawake pesa zenu chungu sana, maadamu una kazi ya kukuingizia kipato jitahidi kuhudumia familia yako.

Nb. Mimi sio femist hata kidogo
 
Hivi wenzangu nyie Ndoani kwenu, Hela ni Kila siku inaachwa Asubuhi mezani ?.

Mimi Bajeti ya Chakula naifanya Kwa mwezi, na nikitoa naitoa jumla , sitoi Kwa mafungu mafungu .

Nachotaka Chakula kisikosekane Wala kelele za Sijui Hela vile Mara vile

Yes kama Mwanaume , Kuna Hela zile za hapa napale ambazo pia hunifanya Kila siku nikiwa narudi home niwe na kitu mkononi.

Siku Nikikuta Chakula hamna, au wagen wangu au Ndugu wangu hawajala,, itakua ndio tiketi ya kumpeleka kwao akafundishwe tabia Kisha aolewe na mwanaume mwingine .
 
Naona hata kazi anayofanya baby wako huijui mpeleleze isijekuwa nanihiii kama aliweza kuacha elf kumi kila siku sasa anashindwa nini??

Ameshaona wewe unajua kutafuta hivyo ujiongeze ukiona hakuna hela ujue amekosa

Unaonekana una gubu.
 
Hivi wenzangu nyie Ndoani kwenu, Hela ni Kila siku inaachwa Asubuhi mezani ?.

Mimi Bajeti ya Chakula naifanya Kwa mwezi, na nikitoa naitoa jumla , sitoi Kwa mafungu mafungu, itakua ndio tiketi ya kumpeleka kwao akufunfishwe tabia Kisha aolewe na mwanaume mwingine ..
Watu wanatofautiana maisha kaka na mtindo kwa ujumla

Mimi hua ananunua vyakula anaweka ndani anahakikisha gas na mkaa vipo then kuna ile hela sio kila siku mtakula maharage kuna nyama kuna samaki n.k hio hio kodi ya meza ndio ntaamua kama tutakula leo au tunalala njaa na kwenye kodi hiohio ndio mwanamke anajiongeza sio chumvi imeisha baba nanihii hakuna chumvi no
 
Back
Top Bottom