Mume wangu hapendi ndugu zangu

Hoja yako ya kwanza sio poa.
Haifai umwambie ndg yako kuwa mmewe hapendi aishi pale...utasababisha ndg wote wamchukie
 
Dada yangu angekua mtu wa mitandao ningesema ni wewe aisee
Ila nyie Kuna wanaume wana gubu na roho mbayaπŸ™Œ..majuzi nimepata taarifa mume wa Dada Katia chumvi juice za mdogo wanguπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Jamani ..mwezi uliopita Katia simu kwenye ndoo ya maji...ngachokaaa
 
We kipindi ulimshirikisha kweli mumeo au ulijiamulia mwenyewe kuwa nimchukue??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpangishie chumba huyo mdogo wako. Umri wa mwanachuo unatosha kujitegemea
 
Never gaslight hasa katika hiki kizazi, utavuna mabua. Ubinafsi amekuja ujulia ndani ya ndoa, muulize sababu ni nini hasa maana mwanamke sikuzote hujitoa ndani ya picha mbaya. Aseme ni nini hasa lasivyo hata process za ndoa zisingeenda na mwanaume mbinafsi hutambulika mapema sana kuliko mwanamke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yap, ndiyo maana nasema asitafute picha mbaya kumpaka mmewe bali atafute tatizo haswa ni nini. Hapo kajump to conclusions tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naungana na mdau mmoja hapo juu. Ukishaona situation kibinadamu umeshindwa, ngumu, imekutatiza na huoni njia ya kutokea isiyoleta ugomvi, peleka kwa hakimu asiepokea hongo.

You need spiritual intervention. Washirikina weng wanajua hii formula. Mapema tu wanamtafuta fundi. Wanaroga si kitoto. Because kuna some matters solution yake ni spiritual. Kwa nilivyokusoma wewe ni mtu wa Imani. Sina experience sana lakin nachoweza kusema Pray...

Kwa Imani yangu kuna neno utasoma ktk Isaya 11:6-9. Its possible for the impossibles to happen. Naamini ukiomba kwa kumaanisha na ukalitolea sadaka utaweza. Yumkini ni maroho tena ya kurithi kabisa. We utahangaika kumbe shetani the mastermind yuko nyuma hapo.

Anataka usikie uchungu usiweze kureason kwa hekima au busara. Wewe ukiumia ni rahis kumchukia your partner. Utajikuta unaongea maneno ya uchungu. Ugomvi polepole unaanza. Unakuja kushtuka mlango ulifunguliwa kitambo..mkampa adui nafasi. Kuna mdau hapo juu kashauri dogo either apangiwe au arudi nyumbani kwanza. Mungu alimwambia kaini kama ukitenda vyema hutapata kibali?? Kuna vibali mpaka vije lazima uhustle..chek majaliwa. Ilimbidi ajirisk maisha yake ili apate kibali (if its true..if not watajijua wenyewe). So its a hustle. Keep in mind shetani hapendi ndoa, hapendi amani, hapendi maelewano, hapendi umoja. See the real enemy...deal wit the problem from the root.....
 
Kwanza huyo Jamaa anapata wapi muda wa kuonana na watu wa nyumbani,mie huwa nikiondoka nyumbani SAA 12:30 kurudi ni SAA 3-6 usiku hadi watoto huwa wananimisi.
Ndugu akija nyumbani anaweza akamaliza wiki nzima ndio akaniona has a Jumapili.
 
Kwa Ni mtoto asikae hostel?Kuna Sababu gani za kumtesa mtoto kisaikolojia hapo nyumbani.......by the way Kuna possibility kubwa huyo Bwana kaomba nanihino Sasa kwa vile umesema binti anatabia njema utakuwa kanyimwa Sasa Ni gubu kwa kwenda mbele
 
Wakati wa kumleta mdogo wako ulimshilikisha mmeo?au ulimleta kwa mabavu
 
..Inawezekana ni kutokana na familia alikotokea yeye, kubwa/ndogo

labda ndoa yenu bado changa ~huenda huyo binti anamkosesha kujinafasi atakavyo yeye ,mtoto wa kike na wa kiume ni tofauti ktk mazingira flani ...
(kumbuka mmoja ni ndugu, mwngne msaidizi wa kazi, kwahyo hawana nafasi sawa)

...huyo binti ana umri gani? Maana umemtaja sana kama mtoto, kama wadau wanavyosema, hilo la mapenzi nalo linawezekana pasipo wewe kujua

...inawezekana unampenda sana na kumthamini mdogo wako kuliko mme wako by the way

...inawezekana ndugu zako nao wanamtegemea yeye kwa kiwango kikubwa (kinyume na ulivyosema)
fikiria hili neno "nakuja sebuleni kukaa nikute seat" (maana yake 'boss')

hebu fatilia zaidi
 
Mimi naona sawa ndugu waje wasalimie na kuondoka wakikaa sana wataleta mazoea.isije tokea kama yule jamaa wa moro aliekuwa analalamika kutukanwa na shemegi
 
Ndoa bado changa ila watapatikana tu
Sasa ndoa changa unaanza kuleta an outside person kweli. Hapo iwe ndugu wa mume au mke. Jenga ndoa na ndugu zako wahudumie kwasehemu yao. Usichanganye mafaili ya undugu na ndoa, mwanaume kashaona hii ndoa itafeli maana ndugu hawataisha. Ndugu zako siwake na wake siwako. Unasema it's simple as that kwasababu hamjaanza kuwa na watoto ila mkishakuwa nao believe me it's not simple. I know you love your siblings but never let it interfere with your marriage soon or later, you will have to choose.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamnyima naniliiii
 
Mmeo ni mbinafsi,mchoyo ,tho mbaya Kwa wageni ,anapenda muwe nae tu ndani bila buguzi,

Ebu eleza maisha kabla ya mdogo wako kuhamia hapo yalikuwaje ? Nikimaanisha kujiachia ndani na mengineyo,labda dogo anawaharibia ndio maana mume wako hapendi buguzi.,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…