Weww unachezea watu akili hizi post zako hizi
Habari zenu wadau wa humu tena, ninalileta hili ili tu nipate ushauri, nijifunze si nia mbaya hasa kwa wale ambao mko ktk ndoa mke/mme naomba ushauri wako si kejeli, ukinitukana sidhani km utakuwa umenisaidia kwa kweli maana ni bora mm ninaitaji kujua kuliko wale waliokaa na kulalama mitaani.
Mm niko ktk ndoa kwa miaka minne tuna watoto wawili, nimegundua mume wangu anachepuka kwa siri kiasi kutojali hisia zangu kabisa, pamoja na mapito mengi na kuamua kusamehe na kusimama km mke hiki kitu mm kinanikwaza sana na naumia sanasana maana najiuliza nn nimeshindwa kumfanyia, mm ni mwanamke ambae si mpofu kitandani najitaidi kumpa kadri niwezavyo ila nashangaa mwenzangu anashindwa kujali na kuheshimu ndoa yake. Naweza kukaa miezi miwili tunalala mtu akitoka job kwa malaya, mara kichwa kule tunalala mzungu wa nne! Visa jamani, ni tabia ambazo akishaanza kuchepuka amebadirika. Siku akiamua kukushika akishamaliza yy ww huku bado hajali nabaki na hamu naumia sana moyoni.
Mm sidhani km mwanaume akitembea nje km anaweza kumridhisha mkwe, jamani mm ni mwanamke naejiheshimu na nina hisia zangu, nifanyaje? Maana namwambia lakini anakataa na hata umwitie yoyote huwa hakubali!
Najiuliza hivi mtu unawezaje kuishi na mwanamke mkeo ukajisahau kiasi unamletea dharau ukishaonja nje ndoa una maana gani, maana huwa nasikiliza jirani akipiga kelele najiuliza nimelala na mwanaume kweli! Naomba ushauri wako.
Najuta kumpenda mwanaume asiyenipenda mwenzenu, naombeni ushauri wenu wadau