Usimnyime mume wako anapohitaji tendo la ndoa

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,518
22,007
Hii inawahusu wanawake wote walioolewa ambao ni wachoyo wa tendo la ndoa na waume zao.

Lady mpe tu haki yake mumeo kila anapohitaji, usimnyime kabisa.

Mfanye mumeo asiwe mtu wa kuchelewa kurudi nyumbani kwa kumpa haki yake bila masharti.
Usipofanya hivyo atakuwa anachelewa kurudi nyumbani kwa kupita kwa vimada wake

Kwa kumpa kila mara hakuna unachopoteza wakati mnajiburudisha wote na mumeo. Yaani hapo, wewe pia hupata faida za raha ya kupendeza, ni raha inayokufufua kutoka katika dhiki na kukupandisha hadi juu ya kilele cha mlima kilimanjaro.

Kumbuka, ulipokubali kuolewa naye, ulimpa haki za kisheria za mwili wako. Haijalishi kwamba mlifanya sherehe ya harusi au hamkufanya alipokuoa, we mpe tu hadi awasahau kabisa vimada wake. Agano lenu siku ya kuoana naye lilishuhudiwa na Mungu Mwenyewe (Mal 2:14).

Kumbuka huu usemi wa watu wazoefu ktk mahusiano usemao "njia ya kwenda kwenye moyo wa mwanamume ni kupitia chakula" maana halisi ya huo usemi ni hii "chakula kinachoshibisha na kuburudisha mwili na roho huimarisha afya" hivyo wewe na mwanaume wako mnaimarika sana kwa kutokunyimana.

Haijalishi udhaifu wa mumeo , kamwe usitumie mwili wako kumdanganya kuwa upo kwenye siku zako wakati sivyo.

Mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake, lakini mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe (Mithali 14:1).

Ukiwa mchoyo utatoswa, na ukitoswa usitafute mchawi.

Je upo tayari kuibomoa /kujenga nyumba yako kwa mikono yako mwenyewe?

Ubarikiwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom