Mume wangu hahudumii familia

mkiwamonie

Member
Apr 25, 2017
15
9
Habari wapendwa,

Mimi ni mwanamke nilieolewa miaka 17 iliyopita, na tumajaaliwa kupata watoto 3 mkubwa kwa sasa yupo kidato cha nne, lakini kwa muda wote huo nilioishi na mume wangu hakuwahi kuhudumia familia kwa chakula wala chochote ndni kama Baba, pesa yake ni kusoma tu.

Mimi nilikua nafanya kazi binafsi (stationery) kwa sasa nimefungua kijibiashara cha kukidhi mahitaji ya familia, kibaya zaidi toka nimeanza kuishi nae ndugu zake wanapishana kukaa na huduma zote ni mimi mwenyewe.

Hata sasa kuna ndugu zake wanne ndani na wote ni tegemezi kwangu.

Nishaurini wapendwa niendelee ama nihame, maana habadiliki...
 
Kama umewahi kukaa naye chini kuzungumzia hii tabia yake isiyokubalika ndani ya ndoa na bado hakubadilika basi huyo hana hadhi ya kuitwa mume au Baba. Nakushangaa tu umevumilia hili kwa miaka 17.

Habari wapendwa
Mimi ni mwanamke nilieolewa miaka 17 iliyopita, na tumajaaliwa kupata watoto 3 mkubwa kwa sasa yupo kidato cha nne, lkn kwa muda wote huo nilioishi na mume wangu hakuwahi kuhudumia familia kwa chakula wala chchte ndni km bb pesa yake ni kusoma tu. Mm nilikua nafanya kz binfsi (stationery) kwa sasa nimefungua kijibiashara cha kukizi mahitaji ya familia, kibaya zaidi toka nimeanza kuishi nae ndg zake wanapishana kukaa na huduma zt ni mm mwnyw. Hata sasa kuna ndg zk ndni 4 wote ni tegemezi kwangu, nishaurini wapendwa niendelee ama nihame, maana habadiliki...
 
Miaka 17... Hamuyaongea Ndani watoto wa tatu, Bado Hamuwezi kushauriana Ndani... Let me watch upcoming Comments
 
Mmh uvumilivu gani huo!!? Ongea nae au hao ndugu pia waanze kuchangia mahitaji ya hapo. Unatesa wanao
 
Back
Top Bottom