Habari za weekend wakuu,
Nimekuwa na wakati mgumu kwa muda mrefu bila kufurahia ndoa yangu tangu nimeolewa. Ni hivi mume wangu amekuwa ni mtu wa michepuko isiyo na idadi kibaya zaidi hakuna beki tatu atakakuja asiye tembea nae hata awe mbaya kiasi gani. Kilichonifanya nilete uzi huu humu kwa lengo la kupata ushauri.
Ni kuwa asubuhi niliamka vyema na kwakuwa ni weekend nilimuuliza ana ratiba gani akajibu hana ratiba yeyote atakuwepo tu nyumbani.Ilipofika saa nne tukapata mgeni ambaye ni Jirani, ni baba mtu mzima sana alikuja kumuonya mume wangu ache tabia ya kutembea na mkewe.
Wakati naendelea kutafakari hilo nikapokea ujumbe kwenye simu yangu kutoka kwa mwanamke aliyejitambulisha kama mpenzi wa mume wangu na anamuulizia kama yupo, nilimwambia akakana kabisa. Baada ya muda kidogo akapokea simu ambayo hakutaka nisikie akaenda kuongelea nje ya geti alipomaliza tu akaniaga nikamzuia asiondoke lakini akaondoka kibabe.
Binfsi sioni maana ya kufuga malaya kama huyo, anakula vyangu, hela anatumia zangu anaishi kwenye nyumba yangu halafu anifanye mie kama spare tyre?
Naombeni ushauri kuna haja ya kuendelea na mtu kama hayu? Nilidhani kumpa gari ndo kunamfanya aweweseke hivyo nikaamua kuliuza gari lake mwze wa tano lakini bado hakomi.
Nipeni dawa nimkomeshe.