Kama umegundua jamaa Ana ndoa yake Tafadhali acha ndoa ya watu Dada,Wanaume wengi humu wamekutia moyo kua endelea Na huyo jamaa Ila unajipa laana amini usiami kama wewe ni mkristo lazima haya kuna siku yatakurudia.
Ni jinsi gani huyo Dada mwenye mme ameumia hebu fikiria ulivyoumia wewe alivyokwambia Ana Mke hadi wivu ukakukaba si zaidi ya Mama watoto wake alivyotoa jozi baada ya kuambiwa ukweli juu yako?
Alichokiunganisha Mungu binadamu asikitenganishe hivyo usiwe mmojawapo ya wavunja ndoa za watu,mliyoyatenda yatosha sasa tubu Mungu atakupa aliye wako achia ndoa ya watu nakusihii ktk jina la Yesu.
Nimeshikwa Na huzuni Nakuhisi maumivu ya huyo Mke Na watoto,usipo mwacha naomba Mungu aje Akugeuzie hiki kibao uje uyahisi haya maumivu kabla hujafa.