Kaolewe tu mdada..
Ukaendeleze kula raha za dunia, mahali mama yako mdogo alipoishia........
Mambo ya Walawi 18: 6-23
walawi 18:6? ?Hakuna mtu awaye yote atakayemsogelea ndugu wa karibu ili kukutana naye kimwili. Mimi ndimi BWANA.
7?? ?Usimvunjie heshima baba yako kwa kukutana kimwili na mama yako. Yeye ni mama yako, usiwe na mahusiano kama hayo naye.
8? ?Usikutane kimwili na mke wa baba yako, hiyo itamvunjia heshima baba yako.
9? ?Usikutane kimwili na dada yako, wala binti wa baba yako, au binti wa mama yako, awe amezaliwa katika nyumba hiyo au mahali pengine.
10? ?Usikutane kimwili na binti wa mwanao ama binti wa binti yako, utajivunjia heshima.
11? ?Usikutane kimwili na binti wa mke wa baba yako, aliyezaliwa na baba yako, huyo ni dada yako.
12? ?Usikutane kimwili na dada wa baba yako, ni ndugu wa karibu wa baba yako.
13? ?Usikutane kimwili na dada wa mama yako, kwa sababu ni ndugu wa mama yako wa karibu.
14? ?Usimvunjie heshima ndugu wa baba yako, kwa kukutana kimwili na mke wake, yeye ni shangazi yako.
15? ?Usikutane kimwili na mkwe wako, yeye ni mke wa mwanao, usiwe na mahusiano kama hayo naye.
16? ?Usikutane kimwili na mke wa kaka yako, utamvunjia heshima kaka yako.
17? ?Usikutane kimwili na mwanamke kisha na binti yake. Usikutane kimwili na binti wa mwanawe au binti wa binti yake. Hao ni ndugu zake wa karibu, huo ni uovu.
18?? ?Usimchukue dada wa mke wako kuwa mke mwenza na kukutana naye kimwili wakati bado mke wako anaishi.
19?? ?Usimsogelee mwanamke ili kukutana naye kimwili wakati wa unajisi wa siku zake za mwezi.
20?? ?Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi.
21?? ?Usimtoe mtoto wako ye yote awe kafara kwa mungu Moleki, kamwe usilinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi BWANA.
22?? ?Usikutane kimwili na mwanaume kama mtu akutanaye na mwanamke, hilo ni chukizo.
23? ?Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili, huo ni upotovu.'