ni mingi but in real sense ni michache, mapenzi ya surprise ndio yanaponza wengi, umepigwa chini hapa basi ili kumkomoa mwenzio unaibukia kule tena ukifika kule unatangaza kabisa na ndoa, sasa yakija kukupata ya kukupata mnaishia kulaumu ndoa!!! Vijana wana mambo, [pata muda mzuri wa kufahamiana kiundani, mila zenu na desturi, tabia na mienendo yenu, je mtafiti kweli? au je huyu mwenzangu ana pretend au ni kweli tutakuwa pamoja,
Kumbuka
ladyfurahia, you are about to choose a pesron ambaye utaishi naye kwa maisha yako yote yaliyobaki, mtashirikiana baadhi ya vitu kama sio vyote, utalala nae kitanda kimoja, shuka au blanket moja. Sasa kama hujafanya uchaguzi sasa hebu imagine hayo maumivu utakayoyapata, utatembea kwa washenga, wazazi, wachungaji na hata wazee wa ndumba but kamwe ndoa haitasimama.
Ni muhimu sana sana tukaacha kukurupukia ndoa kama kweli tunataka tuwe na waume au wake wa at least 60% ya our wishes, na ukitaka kujua kama huyo mtu ndio huyu na mta-match basi jitahidi kuwa mnatoka mara kwa mara ndipo utapata hasaaaaa tabia zake, kama mna gari angalia hata anavyo-behave anapo-drive, akichomekewa na dala dala au likitokea lolote njiani liwe kubwa au dogo, pima reaction yake inavyokuwa. Jaribuni kwenda sehemu zenye watu wa hadhi ya chini, je anawaonaje? anawajibu vipi?
Pia, huyu mwenzio ni mcha MUNGU, si laziam awe wale ma-radical, NO NO ila naamanisha kuwa at least awe na hofu ya MUNGU, tabia zake nyingine zikoje? usafi, ulaji na lugha yake? hebu imagine unakuwa na mchumba ambaye sentensi haiishi keshaweka tusi au akikasirika au akichukizwa kidogo tu ameshaweka rundo la matusi!!! Pata picha hio familia watoto wataiga nini toka kwa mzazi wa namna hio?
Lakini pia jaribu kuchunguza japo hata katika maongezi yenu, ana mtazamo mpana wa maisha kiasi gani? hapa nazungumzia elimu, ujenzi, biashara, na mengineyo ya jinsi hio, kwa mfano, anajisikiaje kuendelea kuishi kwenye nyumba ya kupanga? ni kweli huwezi kuanza maisha na kuwa na nyumba but at least awe na vision kuwa one day tutakua na nyumba yetu, au napenda sana nisome kozi ile au hii au unaonaje kama watoto wetu (kama MUNGU atatujalia) wawe wanasoma kwenye shule nzuri kama hii? na vitu kama hivyo.
Je huyu mchumba wako awapo na rafiki zake huwa anawachukuliaje na kukuchukuliaje? Kama kiburudisho au kama ATM? Rafiki zake ni watu wa aina gani? wana mtazamo gani katika maisha? ni watu wa kupenda shortcut au ni wapiganaji katika kweli na haki? Wana maisha ya style gani? kujirusha kwa sana au ni watu ambao hata kama watakutana Bar lakini bado wataongea at least sentensi tano zenye kuzungumzia their future?
Suala la kuwa na tamaa nalo laweza kujionyesha kwenye kipindi hicho cha uchumba, tamaa mbaya ya mali za haraka haraka (kwa mfano, mbona fulani kafanikiwa kuliko sisi, mbona fulani ananyumba sisi hatuna?) au je huwa anatamani wewe uweje? kwa mfano, (mwanaume akimuona mwanamke) anaweza sema natamani mchumba wangu angekuwa anavaa kama fulani, natamani angekuwa mweupe au mweusi kama fulani au mrefu au mfupi kama fulani aliejazia nyuma kama fulani, such tamaa hupelekea kumjengea SHETANI upenyo wa kuchip in mawazo maovu.
Sasa haya yote kwa akili ya binadamu ntayaweza kweli au nitayaonaje au mbona watu husema hakuna aleimkamilifu? Nakushauri kwa akiba ya baadae kuwa, vitu hivi hudhihirika tu pale unapokua na NIA ya kweli, MUNGU si mjinga akupe mtu mpuuzi atakayeiumiza ndoa yako ambayo yeye mwenyewe katika kitabu cha Mhubiri Sura ya TANO ile mistari yote inazungumzia kuwa NI HERI KUWA WAWILI KULIKO KUWA MMOJA, MAANA WAPATA IJARA NJEMA KWA BWANA, kumbe MUNGU huwakubali walioko kwenye ndoa, kumbe kuna mambo mazuri NDOA maana ukiendelea kusoma sura hio hio anasema kuwa, ni rahisi sana kuvunja vijiti vitano mkiwa wawili kuliko ukiwa mmoja (ni tafsiri yangu) na pia kuwa kumbe mkilala wawili mwapeana joto kuliko kulala peke yako na tena ni rahisi huyo mmoja kumwinua mwingine pale aangukapo (hii ni pamoja na stress za kazini na maisha) unaporudi nyumbani, mkeo au mmeo hukufariji na kukupongeza ndio kuinuana huko. Pia katika Kitabu cha Wimbo ulio bora na Methali kuna maneno na mistari yenye kudhihirisha kuwa NDOA ni kitu chema na kwamba hakika amebarikiwa yule anywaye maji yatokayo kwenye kisima chake mwenyewe na wala sio yeye pamoja na wageni.......kwahio Mkabidhi sana MUNGU njia zako, unapoomba kitu usingalie kuwa mbona mimi ni mzinzi, ni mwizi na mengineyo mengi, jikabidhishe kwa MUNGU, repent everytime mimi naamini na najua nitakua kinyume na watu wengi ila mimi naamini TOBA ni kitu ambacho ni ongoing maana tunatenda mengi mabaya kila siku na kila dakika, tunakosea tunapojiona kuwa tumeokoka sana na hatuhitahitaji tena TOBA. kumbuka tunaokolewa kwa NEEMA tu kwahio hata haya ya kuwajua wapenzi wetu na wachumba wetu ni kwa NEEMA tu
Labda utajiuliza kwamba, ok sasa nimeyajua haya yote na kwamba the person ambaye nikim-date hayuko kwenye viwango vyangu, ninataka kuondoka kwake. Niseme hivi, KWELI itakuweka HURU, jifunze kuwa mkweli na muwazi, kaeni jadilianeni na mwelezane au tumia Elders kama huo uchumba unadhani ulishaanza ku-mature. Ni afadhali kuumia huku mwanzoni kuliko kukubali kubeba msalaba for the rest of your life.
ladyfurahia Mpwa wangu mpenzi, nilichokiongea ni kwa jinsia zote mbili, japo hakiko sahihi kwa asilimia mia moja lakini naamini kitasaidia na wengine, niko wazi kuendeleza mjadala, tukosoane, tusahihishane ili tuweze kujenga familia zenye manufaa
mandenyi
Aine na wengine