Mume Mwema Anapatikanaje?

Mume Mwema Anapatikanaje?

yani umenifafanulia vyema bestito nashukuru sana kwa kunielewesha ila nimependa hii page hii imenigusa sana tena sana 4;NGUVU YA MAOMBI😛rayers are very powerful tools.Funga na kusali kwa imani utafanikiwa tu.Biblia ilishasema "Mke mwema hutoka kwa bwana"LIKEWISE mume mwema hutoka huko huko kwa bwana.Sio rahisi kuanza kumtafuta tu mume/mke mwema...na ukampata ni vizuri kumtanguliza Mungu ktk hili.
Swali lako ni gumu na "complex" kidogo kwa sababu kwa maoni yangu lina-cover sio tu psychology lakini hata spiritual matters.Majibu yangu ntayagawa katika maeneo ya kiroho na ya kisaikologia kama ifuatavyo:
1;SIFA UNAZO?:Ili kumpata mume/mchumba mwema....jiulize "wewe ni mwema?' na unadhani mume mwema ana vigezo gani?wewe unavyo?Kwa sababu utaidanganya nafsi yako bure kama umeweka viwango ambavyo hata wewe huna!Kumbuka ndege waliofanana huruka pamoja.
2;UMRI:Mwanaume kijana mwenye umri kati ya miaka 32-35 mpaka 40 ni mwenye uzoefu na mambo mengi na anaweza kuhimili misukosuko ya ndoa na maisha.Kwa lugha nyingine huu ni umri ambao mwanaume anajua vipaumbele vyake na nini anatakiwa afanye na ni kwa wakati gani!Huu ni wakati ambao hata kama alikuwa ni mwenda disco sana basi anweza kupunguza na kuacha kabisa na kuwa tayari katika maisha ya ndoa...tofauti kabisa na kijana wa miaka 25,28 nk.
3;ELIMU:Dunia imebadilika na ina changamoto nyingi sana.Ni muhimu kwa mume unayemtaka awe na elimu angalau ya advance diploma/bachelor degree.Hili litasaidia sii katika changamoto za kifedha hata katika malezi ya watoto na mahusiano yenu.Lakini elimu pia inasaidia hata uelewa wa mambo complex kama ya kiimani na kupunguza uhafidhina(unoko usio wa lazima).
4;NGUVU YA MAOMBI:Prayers are very powerful tools.Funga na kusali kwa imani utafanikiwa tu.Biblia ilishasema "Mke mwema hutoka kwa bwana"LIKEWISE mume mwema hutoka huko huko kwa bwana.Sio rahisi kuanza kumtafuta tu mume/mke mwema...na ukampata ni vizuri kumtanguliza Mungu ktk hili.
 
mhm! miaka saba mbona mingi sana hiyo jamani?
ukitaka mume mwema acha kufanya uchumba wa surprise, mi nilichumbia mke wangu au niseme tulikua marafiki kwa zaidi ya miaka saba, we enjoy it now ( sisemi kuwa hakuna ups and downs zipo)
 
Apataye mke apata kitu chema, naye ajipatia kibali kwa Bwana... (Mit 19:22).
 
Nimeipendaje hii comment yako kweli imenifanya nijue kuwa kuwa kunawatu wanaowatakia wenzao yaliyo mema sana nimefurahishwa sana na mawazo yako mazuri uliyonipa hapa , na vilevile umenielewesha vyema na nami nimekuelewa sana yaani sina cha kuongea hapa asante sana NA Mungu akubariki

you are a wisewoman, then expect to receive the Mume mwema soon! Best wishes!
 
Nikiri kutoka moyoni ya kwamba nimeipenda sana tafakari yako juu hili swala la mchumba/mume mwema nk, lakini pia niache nisikitike ya kwamba mawazo haya yote mara nyingi yanakuja mara baada ya mambo kuharibika ama kwenda ndivyo sivyo.

ladyfurahia baada ya kupenda hii tafakari yako na kusikitika pia, japo sitasema kwa nini nimefanya hayo yote mawili kwa pamoja na katika thread moja acha tu nirudi kwenye issue ya msingi.

Nikupongeze pia kwa kuweza kubainisha vifungu ya kitabu kimoja wapo cha Mungu yaani Biblia inayotoa muongozo halisi jinsi uchumba na hatimaye ndoa na maisha yake kila siku. Hakika wahusika yaani wachumba na baadaye wanandoa wakiweza kuishi katika misingi ya maandiko matakatifu ya Mungu yenye upendo, kuvumiliana katika shida na raha, kusaidiana, utii, nk hayo mambo ya mara uchumba ama ndoa kuvunjika ni ndoto kutokea. Maandiko matakatifu yameweka misingi na maelekezo ya jinsi ya kuishi, lakini sisi wanadamu kwa makusudi mazima tumeamua kuyakiuka na kuchagua misingi yetu ya kibinadamu, mara utasikia haki sawa, utandawazi nk, na mwisho wa siku tunaishia kwenye kuabika kwa kuvunja uchumba, ndoa kila siku iendayo kwa Mungu, hii yote ni kwa sababu ya jeuri na kiburi chetu sisi wanadamu.
Hayo yote kwa kiwango fulani yako nje kidogo ya mada yako mahususi, lakini ndipo msingi wa kukosea tulipoanza kuuacha na kuingia porini ambapo sasa wengine hajui turudije kwenye barabara sahihi.

Msingi wa Kimungu juu ya swala la familia umesimikwa kwa mwanaume, hivyo yeye ndiye mwenye wajibu wa kutafuta mwanamke mwema wa kuweza kuishi naye pamoja na kujenga familia bora yenye kumpendeza Mungu mwenyewe. Kumbe basi ni wajibu pia wa mwanamke mwenye nia siku moja ya kuja kujenga familia kuishi katika maisha mazuri yampendezayo Mungu, na kwa kufanya hivyo hakika ndio wewe utaitwa mke mwema na mwanaume mwema hakika atatoke na kukuijia ili mpate kujenga familia nzuri. Kuna msemo maarufu wa kiswahili unasema "Ndege wanaofanana huruka pamoja". Hivyo kama mwanamke ama binti atakuwa amelelewa na kuishi maisha mazuri yenye sifa za kumfanya aitwe mke mwema, hakika mume ambaye si mwema ni vigumu sana kumsogelea na hata kumwambia neno, hayo yapo na mimi kama mwanaume ninakuhakikishieni. Lakini ndio unakuta binti ama mwanamke amelelewa katika familia ama mazingira ambayo msingi sahihi wa Kimungu haupo naye ndivyo anavyoishi, hakika tegemea pia mwanaume wa aina yako, maana mume mwema hawezi kujaribu hata kukuambia neno, atapita pembeni na kwenda kutafuta wa kufafana naye ili waweze kuungana na kujenga familia yao kadri ya mapenzi ya Mungu.

Tuko hapa tulipo, tunalalamika, tunahaha, wanawake hawawaoni wanaume sahihi kwa ajiri ya kuungana nao, wanaume nao wanahaha wakitafuta wanawake sahihi wa kuungana nao katika familia, hakika hii yote ni kwa sababu tumeacha na kuasi mpango wa maisha ya Mwenyezi Mungu, turudi, tujisahihishe, hatuwezi kushinda.

Ndugu yangu Ablessed njoo huku utoe nasaha zako, mkuu Himidini unaitwa huku, maana juzi tuliona tangazo la kusudio la kuvunja ndoa kati ya ladyfurahia na ndg yangu Mentor eti kisa jamaa aliezea yaliyojiri huko nyuma hasa pale aliposema "Let me test this syndrome, ya mwarabu ina nini", bidada akaomba talaka.

Nisiwachoshe jamani, bye
 
yaani hapo sasa umenena mwana nashukuru kwa kunimaanishisha na kunielewesha ila bado hujaingia sana katika vifungu vya neno la Mungu kwanini hakuna kifungu ambacho kinaelezea KUMPATA MUME MWEMA vingi vinasema kumpata mke mwema why? nidadavulie kidogo best
Mkuu naona una hamu sana na hayo maandiko, ngoja nijaribu kupekua pekua bible kama nitafanikiwa nitakujuvya! lakini simply ni kwamba kama ilivyoandika kwa mwanaume,basi the vice versa is also true kwa mwanamke :smiling:
 
^^
Lyagwa
Asante kwa kuniita awali niliona list ndefu ya lady furahia nikaona niwape nafasi kwanza watajwa.
Back to the topic.
..
Bado naamini Mungu ndiye awezae kumpa mtu Mume mwema na siamini kuwa maandiko yamemtenga mwanamke Maana wote wamepewa nafasi ya kumuomba kwa nidhamu-atampa.
..
Tatizo linakuja kuwa Mtu anapata mchumba,,akishapata then ndipo anaenda kwa Mungu kuomba ila moyoni tayari ana choice yake ambayo ameamua.Ongeza tena yale mafunuo Oo! Nimeonyeshwa ni huyu! Oo! Ni yeye tu-Lakini Mungu anatazama tu.
Those who let choices in hands of God (to choose for them) will never go empty.
^^
 
Last edited by a moderator:
.........Habari yako mdada!!. Jaribu kupitia kitabu cha Waefeso 5;28-33. Katika mistari hii Mungu anaelezea sifa kuu ya Mwanaume(mwema) ni kumpenda mkewe na Mwanamke nae anatakiwa kutii ule upendo wa mumewe. Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya utii na upendo wa kweli kutoka kwa Mwanaume. Tatizo hapa linakuja kwa wadada wengi wanataka kuona au kumjua mwanaume mwenye mapenzi ya kweli ila hao hawapo tayari kuonyesha utii na tabia njema unaotakiwa kwa mume(sizungumzii hawala).

Pia maandiko haya yanasema kuwa siri hii ni kubwa sana, bila ya shaka unatakiwa umshirikishe Mungu ili upate kumjua na kumpata huyo Mume mwema mwenye sifa zilizotajwa na unazozihitaji wewe.

Nakushauri umtangulize na kumuomba Mungu, utampata mume mwema!
 
Kwa kufanya ngono utamjua tu.
 
Lyagwa nimeona wito nami sina budi kuitika wito wako. Jinsi ya kumpata mume mwema . Kama mtoa mada alivyoainisha vifungu vya neno la Mungu na kutoa kidogo mashaka yake juu ya kwanini mwananmke hakupewa muongozo wa kumpata mwanaume mwema. Ni kweli ukiangalia kwa haraka unaweza kusema hivyo lkn tukirudi nyuma na kuangalia mazingira ya uandishi yalitumia utamaduni upi tunaweza kuelewa lkn hapa si mahala pake ngoja nirudi kwenye swali la msingi. Binafsi nilipokua naomba mume mwema nilitumia andiko la ombeni jambo lolote kwa jina langu nami nitafanya au njooni tusemezane eleza mambo yako ili upate kupewa haki yako n.k. Kwa kweli nilienda mbele ya uso wa bwana kwa ujasili mwingi na kumuomba Mungu mwanaume niliekua namuhitaji kwa kifupi nilielezea nataka mwanaume wa jinsi gani hasa nilipojifahamu tabia yangu. Mara nyingi huwa tunaenda mbele za Bwana kuomba tukiwa tayari na mtu yaani tunataka Bwana atoe kibali tu kwani tulisha chagua au tunamuomba mungu atupe mume wa kufanana nae. Sasa hii kusema wa kufanana nae ipo general mno . Ni vizuri kua specific let's say umeomba mume ukapewa mcha Mungu lkn akawa na tabia ambazo wewe hazikufurahishi kama vile labda yeye muda wote yupo kwenye huduma na wakati wote ana watu hana muda na wewe au labda muongeaji sana. Sasa ni vizuri kumueleza bwana ukiwa tayari na vision ya mume unaemtaka . wakwangu nilikua tayari ninae moyoni ie picha ya mume wa aina gani nilikua tayari ninayo. Kwa hiyo basi ucha Mungu ni kitu cha lazima kuanza nacho lkn pia uende mbele zaidi na kumuomba Mungu mume unaemtaka nafsini mwako. Mume mwema anapatikana kwa Bwana piga magoti omba na Bwana atakupa umpendae.Naamini mume atokae kwa Bwana utampenda na yeye atakupenda na kukuheshimu.Kama nilivyoeleza mimi Bwana alinipa niliekua namtaka na sasa nina miaka 14 ya ndoa na miaka 2 ya uchumba so naweza kusema tupo pamoja kwa 16 yrs. Na muda huu wote tumeishi ktk amani na furaha isiyoelezeka na tunampenda Mungu. Nakumbuka kuna mtumishi flani aliwahi kusema andika sifa ktk karatasi yako za mume/mke unaemtaka pengine list hiyo itakua na 10 points eg mrefu, mpole, msomi wa degree, mweusi,n.k sasa hii list unaenda nayo mbele za bwana na pia itakusaidia kupata picha ya mume/mke unaemtaka.
 
Last edited by a moderator:
Ndiye mimi sema ukaniacha!!!

Hahahaha dogo, shida yako si ya mwingine ujue...

attachment.php
 
Kwanza kabasa nafurahi na kukushukuru kwa kuitika wito na pia kuelezea mtazamo na pia kwa kutoa ushuhuda mzuri wa jinsi ghani wewe binafsi uliweza kupata mume mwema kwa mtizamo na matamanio yako, hakika inapendeza, na wala sikutegemea ungekwenda mbali hivyo hadi kutoa ushuhuda, hii inaonesha ni jinsi ghani ulivyoguswa na mada ya dada yangu ndg ladyfurahia. Nasema shukrani once again for your positive response.

Nje ya maada nichukue furasa hii kukupongeza binafsi kwa safari yako ya maisha, ulipofikia kila mtu mwenye mapenzi ya dhati na huu wito angependa kufika huko na zaidi, sisi tumo lakini hata nusu huenda hatujagusa, lakini tunamshukuru Mungu na kuzidi kumuomba yeye pekee maana kupitia yeye alituwezesha kuwa hivi tulivyo katika umoja wetu. Kila la kheri sana dada Ablessed na ubarikiwe sana.
 
Last edited by a moderator:
^^
Lyagwa
Asante kwa kuniita awali niliona list ndefu ya lady furahia nikaona niwape nafasi kwanza watajwa.
Back to the topic.
..
Bado naamini Mungu ndiye awezae kumpa mtu Mume mwema na siamini kuwa maandiko yamemtenga mwanamke Maana wote wamepewa nafasi ya kumuomba kwa nidhamu-atampa.
..
Tatizo linakuja kuwa Mtu anapata mchumba,,akishapata then ndipo anaenda kwa Mungu kuomba ila moyoni tayari ana choice yake ambayo ameamua.Ongeza tena yale mafunuo Oo! Nimeonyeshwa ni huyu! Oo! Ni yeye tu-Lakini Mungu anatazama tu.
Those who let choices in hands of God (to choose for them) will never go empty.
^^

Himidini, nashukuru kwa kuwa umeitika wito wangu.

Aidha pia nashukuru binafsi kwa kukuita maana hakika sikukosea, nasema hivyo kwa sababu kuu moja tu, mchango wako una kitu kipya ambacho kwa namna ya pekee kabisa naweza kusema umekitaja na kukieleza vema (short and very precisely ) nacho ni jinsi ya maombi.

ladyfurahia, njoo huku uchote namna nzuri ya kupeleka maombi kwa bwana juu ya kupata mume mwema. Hakika penye wengi hapaharibiki neno, jf ni kisima cha elimu.
 
Last edited by a moderator:
Habarini bandugu marafiki zangu wote na wasio marafiki pia.

Naingia kwa ujio kama alivyokuja Raisi Obama kimkuku kuku na wakiana kwa leo wapendwa wangu
marafiki zangu ninaingia kiimani zaidi na ni vyema muelewe nilichoamua kukizungumzia hapa na sio
kufakamia bila hata kuelewa topic hii yasemaje: Kabla sijaenda mbele zaidi tazama picha hii hapa:

View attachment 100908 na hii View attachment 100909 hapa tena View attachment 100910 mwisho View attachment 100911

Kila mmoja wetu anajua kua Maandiko matakatifu yanavyosema sana jinsi ya kupata Mke kuliko Mume na maandiko maarufu ni kama-‘’Mithali18:22-‘’Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana’’ na Mithali.31:10-’’Mke mwema( Kiswahili imetumia neno moja tu .’’Mwema’’ lakini Kiingerea ktk Bible mbalimbali imetumia maneno mengi yenye nguvu ya ajabu na kushangaza kujua kumbe Mwanamke mtarajiwa kuwa Mke ni kitu kizuri na cha ajabu sana hasa aliyetoka kwa Bwana. Maneno yaliyotumika ni kama.’’ wife of noble character’’, ‘’capable’’, ‘’intelligent’’ ‘’virtuous woman’’, ‘a competent wife’’, ‘’worthy woman’’), ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. Tena Biblia ya King James na New King James ndizo zimetumia neno ‘’Virtuous woman’’ ( notice: Ni woman!) na maana ya neno ‘’Virtuous’’ ni ‘’good’’, ‘’moral’’, ‘’ethical’’, ‘’upright’’, ‘’honourable’’, ‘’excellent’’, ‘’pure’’, ‘’worthy’’, ‘’honest’, ‘’righteous’’, ‘’exemplary’’, ‘’squeaky clean’’, ’’blameless’’, ’’praiseworthy’’, ‘’incorruptible’’, ’’high-principled’’), pia Mwanzo.24:1-67.

Katika Agano Jipya, tunakutana na neno kuchumbia au Mchumba wazi wazi ktk Luka.2:5 ingawa hatuambiwi Joseph (yusufu) alimpataje mdada Mary (Maria mama wa Yesu) Kwakua ni ivyo kwamba Bible imeongelea sana kuchumbia au Mchumba wazi wazi ktk Luka.2:5 ingawa hatuambiwi Joseph alimpataje mdada Mary. Kwakuwa ni ivyo kwamba Bible imeongelea sana kupata Mke mwema ambaye anapatikana tu kwa Bwana, mchumba bora je? anayepelekea mke mwema, tunampataje? kwa kizazi chetu cha leo cha DOT .COM ambapo hatuchanguliwi Wachumba/Wake zetu na wapendwa marafiki zetu, Viongozi wa Kanisa. Maparoko au Wazazi kama zamani, tunafanyaje kuwa salama?

Tutafanyaje kumpata mchumba mwema (mume) kwa kizazi hichi jamani na je kwanini haya maneno hayakuandikwa kwenye Bible? kwani sisi madada tunachanganyikiwa nami pia yameniconfuse mwenzenu kabisa wala sijaelewa, kwani Mume (Mwanaume) mwema hapatikani kwa Bwana? au ni versa vesa tu hapa.ambayo imewekwa, kwani hakuna wanaume wema wa kuolewa nao.? Ndo mana nimependa niwashirikishe jambo hili la kiimani tuchambue kidogo. kwani huwa nikisoma vifungu hivi vinanitatiza sana. Nakuwa sielewi kabisa my frendo. HAKUNA MWANAUME MWEMA TOKA KWA MUNGU?
Karibuni mabestito kwa uchambuzi zaidi hapa.

cc: Nicas Mtei, Ruttashobolwa, Erickb52, Mr. Rocky, Arushaone, Mtambuzi, Mamndenyi, lara 1,
stevoh, jouneGwalu, Kipaji Halisi, Jiwe Linaloishi, Filipo, Liverpool, Passion Lady, charminglady, Paloma, Mentor, Heaven on earth, everln salt, gfsonwin, Lady doctor, Asprin, Madame B, Lucas, @Rular Swaga, Lyagwa, Ben Saanane, mimisa, na marafiki zangu wote jongeeni

Hongera sana kwa kuwaza hili....
Sijui umri wako..bt kwa mtazamo wangu,jiandae mapema sana kwa sala na kufunga....pia usisaha kutoa sadaka kama shukrani au unajua ktk bible am Christian,hakuna sehemu yeyote ilioandwikwa nijaribu kwa kutoa nanyi mtaona nitakavyowazidishia baraka,jaribu uone kwa kutoa na sala....
Ulisha wahi kusoma habari za HABAKUKI?
"UTAYAWEZA YOTE KWAKE YEYE AKUTIAYE NGUVU"PHILP 4:13.
 
Kwanza kabasa nafurahi na kukushukuru kwa kuitika wito na pia kuelezea mtazamo na pia kwa kutoa ushuhuda mzuri wa jinsi ghani wewe binafsi uliweza kupata mume mwema kwa mtizamo na matamanio yako, hakika inapendeza, na wala sikutegemea ungekwenda mbali hivyo hadi kutoa ushuhuda, hii inaonesha ni jinsi ghani ulivyoguswa na mada ya dada yangu ndg ladyfurahia. Nasema shukrani once again for your positive response.

Nje ya maada nichukue furasa hii kukupongeza binafsi kwa safari yako ya maisha, ulipofikia kila mtu mwenye mapenzi ya dhati na huu wito angependa kufika huko na zaidi, sisi tumo lakini hata nusu huenda hatujagusa, lakini tunamshukuru Mungu na kuzidi kumuomba yeye pekee maana kupitia yeye alituwezesha kuwa hivi tulivyo katika umoja wetu. Kila la kheri sana dada Ablessed na ubarikiwe sana.
Mkuu ilibidi nitumie ushuhuda wakati mwingine ni ngumu kutumia theory. Nashukuru sana kama kuna watakaojifunza kupitia ushuhuda wangu . ubarikiwe sana
 
Kwa ujumla vijana wa kike na kiume wana wakati mgumu sana wakati wa kumpata mwenzi wa maisha. Inakua rahisi kwa mwanaume cse yy ndo mfanya maamuzi japo nao wana wakati mgumu cse mapenzi ni. Vise versa : vile unavyo mpenda mwenzako sivyo atakavyo kupenda.

Kikubwa ni kumuomba Mungu tukiamini mume na mke mwema anatoka kwa Lkn tunapaswa kua na subira ktk kusubiri majibu. Usilazimishe tamaa zako kua majibu.
Superlike...umpendae akupendi al that way...unaweza dhani ndo mwema huyo...kumbe ufikiliavyo wewe ni tofauti na Mungu akuchukuliavyo
 
Back
Top Bottom