Mume kikojozi anavumilika??

Mume kikojozi anavumilika??

Duh pole huo kweli mtihani...akafanyiwe maombi
 
Sio tatizo dogo hilo ila for the time being kabla ya kupata tiba ya kudumu awe anategeshea alarm usiku kila baada ya saa 1 anaamka kukojoa labda itasaidia.
 
MUHESHIMIWA RAFIKI YANGU NKADABWI NASHAURI AENDE HOSPITALI AFANYE UCHUNGUZI WA HAYO MAGONJWA ALIYOAINISHA MYA KAKA HorsePower THEN IKIWA HANA DALILI AU HUO UGONJWA AENDE AKAOMBEWE KWA JINSI NA MNAMNA ANAVYOAMINI YEYE
 
muheshimiwa rafiki yangu nkadabwi nashauri aende hospitali afanye uchunguzi wa hayo magonjwa aliyoainisha mya kaka horsepower then ikiwa hana dalili au huo ugonjwa aende akaombewe kwa jinsi na mnamna anavyoamini yeye



sawa mheshimiwa sana rafiki nivea
maswahibu haya yanahitaji mawazo ya pamoja kama ivi na ushauri wa kindugu namna hii
thank uuu
 
sio tatizo dogo hilo ila for the time being kabla ya kupata tiba ya kudumu awe anategeshea alarm usiku kila baada ya saa 1 anaamka kukojoa labda itasaidia.



hili nalo lina msingi wake mkuu
nitamfikshia leo leo
 
Asante AshaDii kwa ufafanuzi mzuri. Tunajaribu kuexplore njia mbali mbali kuiokoa hiyo ndoa. Hilo angalizo lako ni zuri, sikulifikiria kabla. Cha msingi huyo dada asikate tamaa. Kama laiweza kumvumilia kwa miaka kadhaa, si vibaya akaendelea kumvumilia huku wakitafuta njia mbali mbali za kusolve tatizo.

Nakubaliana na wewe...

Mhhhm itabidi sasa avalishwe condom time analala :biggrin1:

Acha fujo fazaa! Lol! Mwenzio yamemkuta...
 
sina uhakika sana ila nafahamu kuna baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza kuchangia hili tatizo likiwepo
1. Diabetes
2. Urinary tract infection
3. Urinary tract stones
4. Prostate enlargement
5. Bladder cancer
6. Obstructive sleep apnea
7. Neurological disorders
na saa nyingine, acute anxiety or other emotional disorders (matatizo ya kisaikolojia). Lakini kama kuna mashaka ya imani za kishirikina ni vyema kuwaona viongozi wa dini kwa maombezi na ushauri zaidi.



nimenufaika na mchango wako huu pia
nitalifikisha kwa muhusika bila kuongeza wala kupunguza
thanks jamii forum kwa kua na watu kama ww
 
Nimefarijika na ushauri wa HORSEPOWERS- uliyejiunga 22-08-2008
ni ushauri wa kiu tu uzima na umejaa faraja pia kwa yote uliyo eleza
Mungu akubariki.




Sidhani kama suala la kukojoa kitandani ni sababu tosha ya kupeana talaka. Anaweza kumfundisha mumewe kuwa msafi, na kuepuka kunywa vitu vya maji maji usiku kupunguza hatari ya kukojoa usiku. Huyo mume anaweza kutumia muda mwingi kufanya kazi zake usiku ili akichelewa kulala apunguze hatari ya kukojoa kitandani. Anaweza kuvaa hata pampas za wakubwa na akisha kojoa usiku avue na kuendelea kulala bila pampas.

Kumbuka kuwa huyo kaka hakuomba kuugua huo ugonjwa, na kuvunja ndoa kwa sababu ya hilo tatizo la ugonjwa ambalo linavumilika na linaweza kutibika ni kutomtendea haki. Mtie moyo na nenda au mshauri aonane na wataalam wa afya mara kwa mara kwa msaada zaidi.
 
Siamini kama hospitali wameshindwa kumsaidia.
Anyways, afanye kama alivyoshauriwa hapo. Kuweka alarm ya kuenda toilet hata kama kila baada ya masaa mawili, kuchelewa kulala na kuepuka pombe na vimiminika usiku.

Kuna zoezi la muscles linaitwa kegel's exercise. Anakojoa na kuubana mkojo kabisa kwa sekunde tano na kuuchia tena kidogo. Anarudia hivyo hadi amalize. Mwanzoni ni ngumu lakini akizoea itakuwa kawaida tu kwake. Hii itaimarisha misuli ya kibofu (sphincter muscles) na kumsaidia kwa mengineyo.

Ni mtihani lakini mkiwa wasafi wala haitawapa shida.
 
sawa mkuu
mitihani migumu sana hii,tena mbaya zaid kwenye kutokea kwenye mahusiano ya ndoa
kwa mujibu wake anasema tatzo hili miaka kadhaa iliyopita mume wake hakua nalo
na ndio maana wanapata was was je kuna uwezekano pia kukawa na mambo ya ushirikina ndani yake?

Aende kwa maombi; ni tatizo linalohitaji divine intervention hilo.
 
kama wamehangaika hivyo.. nashauri wamwimbie kindumbwe ndubwe ataacha tu...
 
Mhh! jamani kweli kukojoa ndio iwe sababu ya ndoa kuwa mashakani? kama ni mimi wala nisingemuhadithia mtu mambo ya ndani ya mume wangu, zaidi tungeshughulika kutatua sisi wawili na ingeshindikana ningekaa nae karibu zaidi nimuonyeshe mapenzi zaidi ili ajawe na amani maisha ya upendo yaendelee. Hivi yako wapi mapenzi siku hizi???
 
kama wamehangaika hivyo.. Nashauri wamwimbie kindumbwe ndubwe ataacha tu...


dah kindumbwe ndumbwe tena??
Mume wa mtu huyu jamani,after all ni mwanaume mwenzetu jamani
leo kwake kesho kwetu tukumbuke..
 
siamini kama hospitali wameshindwa kumsaidia.
Anyways, afanye kama alivyoshauriwa hapo. Kuweka alarm ya kuenda toilet hata kama kila baada ya masaa mawili, kuchelewa kulala na kuepuka pombe na vimiminika usiku.

Kuna zoezi la muscles linaitwa kegel's exercise. Anakojoa na kuubana mkojo kabisa kwa sekunde tano na kuuchia tena kidogo. Anarudia hivyo hadi amalize. Mwanzoni ni ngumu lakini akizoea itakuwa kawaida tu kwake. Hii itaimarisha misuli ya kibofu (sphincter muscles) na kumsaidia kwa mengineyo.

Ni mtihani lakini mkiwa wasafi wala haitawapa shida.



ubarikiwe sana
shukrani sana
 
mhh! Jamani kweli kukojoa ndio iwe sababu ya ndoa kuwa mashakani? Kama ni mimi wala nisingemuhadithia mtu mambo ya ndani ya mume wangu, zaidi tungeshughulika kutatua sisi wawili na ingeshindikana ningekaa nae karibu zaidi nimuonyeshe mapenzi zaidi ili ajawe na amani maisha ya upendo yaendelee. Hivi yako wapi mapenzi siku hizi???


ni kweli kumuacha mwenza kwa tatzo hili na mengne si ishara ya upendo kwake,muhimu ni kusaidiana na kuvimiliana,na ndio maana tunaomba msaada wa ushauri
maisha yana majaribu sana mkuu
 
Back
Top Bottom