Ukiuliza swali hili utaambiwa mwanaharakati hufai kuwa mke!
Kusuka ya elfu tu shida.......huyo unaweza mwambia ishu za lace wig au hata kubond tu weave akakuelewa......?......pole mwanamke mwenzetu kwa kumeza kimeo.........
Kwa hiyo maswali yasiulizwe kwa kuogopa tu judgement ya mtu???
Mweeeeeeh
No, siyo jinga sema approaching yake inaweza haikuwa nzuri!!
Nina miaka zaidi ya kumi kwenye ndoa, mke wangu hajawahi kanyaga saloon!! Ukimuona yupo smart na anabadilisha mitindo ya nywele kila siku na ni yoyote unayofahamu.
Aliacha kwenda saloon baada ya kugundua kuwa kuna wanaume wanawatumia wahudumu wa saloon kama makuwadi!!
So, kila akienda saloon anakuwadiwa kwa nguvu zote!! Na wanampa na mbinu zote, bahati nilishtuka mapema nikambana akanipa full story.
Tangu hapo mke wangu saloon ni big no!! Lengo ni kujaribu kupunguza ile risk ya kuchange tabia kwa ajili ya familia yangu na mimi mwenyewe.
Kama una swali uliza utajibiwa
Natural hair is the best taste for Me , it's either low cut or dread locks.
Unajuaje kama tatizo ni Gardner mwenyewe? utaniambia Gardner ana mtoto, una uthibitisho upi kama Gardner ndiye biological father? Kuna vitu vingine huwaga ni siri za ndani na zinahifadhiwa!
hayo ni macho ya nje...kwa macho ya ndani unauhakika alikuwa anamvumilia????
......ni wivu unamsumbua huyo mumewe.
Kwahiyo huyo mkeo hajuwi kusema NO? Mpaka wewe umfungie ndani asionane na watu?
Inaonekana mke wako hawezi kusema No...na akisema No basi kwa mtu ambae hajampenda au hana kitu mfukoni.
Sasa utamzuia sehemu ngapi? Maana kuna yeye kufanya kazi ofisi fulani,kwenda sokoni,kwenda hospital, kwenda shopping nk. Je hizo sehemu kama nako akitongozwa utamzuia asiende tena? Binafsi naona tatizo siyo wahudumu wa salon bali tatizo liko kwa mkewe.
Habari wanaume mje mtujuze.
Mume anapomzuia mkewe kwenda kusuka au kutengeneza nywele kwa mafundi au saloon au kuja fundi au mtu wasaloon anamaasha nini?
Wakati anamuoa kamkuta na nywele safi za asili gharama ya kusuka kwa wiki anaweza tumia 1000 au 2000some time mwanamke anajigharamia.
Best yangu ana wakati mgumu wajuzi wa mambo wasomi wa mambo ya ndoa vitabu vya mungu vinasemaje?
Na huyu mwanaume anatatizo gani?
Karibuni nisiwachoshe
Kuepusha shari siyo mpaka awe hawezi kusema no!! Ye mwenyewe alikereka na hali hiyo thus why alitoa ushirikiano maana angekaa kimya mi ningejuaje ilhali siingii saloon za kike!?
Ila inapotokea yeye mwenyewe amechoshwa na hali hiyo!! Kila saloon anayoingia anakutana na tabia hizo na akaniambia wanaume wa mji huu wanatumia watu wa saloon kama makuwadi!! Na akasema nimehama saloon kadhaa hali ni hiyo hiyo unadhani ningemfanyaje?? Nimlazimishe aendelee kwenda saloon au nimtafutie alternative?
Ndo mana nikasema huyo jamaa aproaching yake haikuwa nzuri ila ni kweli kuna tatizo atakuwa ameliona. Aende pole pole atasolve tatizo na mkewe akaendelea kujipodoa na kupendeza kila siku.
Nilichofanya ni kumfungulia mini saloon yake home na kumtafutia mtaalam inapobidi ila mengi anafanya mwenyewe!! Na nilipoamua kuvunja hiyo cheni haina maana hatongozwi ila siwezi kumuacha nimpendae aingie kwenye kitanzi ambacho kikimnasa ndo amesepa!! Na huo ndiyo uanaume, unapoona hatari ya kuibiwa basi pambana kiume siyo mpaka uibiwe ubaki unalalama
Acha kamba zako mkuu!! huyo mke wako ni mzuri kiasi gani hadi kufikia kila salon anayokwenda anatongozwa? angalau basi ata ungesema baadhi ya salon lakini wewe unasema salon zote? Nooo i cant buy that.
Yaani kila salon ya kike anayokwenda anatongozwa yeye!!? Eti nimemfungulia salon nyumbani are you sure?
Nisije nikakuuliza maswali hapa alafu ukala chocho.