[QAUOTE=Avemaria;8747144]Ngoja nikuitie
snowhite,
Fixed Point Kongosho Ablessed FaizaFoxy Kaizer,
Asprin Teamo,
Himidini,
Mbu. Na babu DC naona ye keshajongea!
Nina imani hapo hutokosa jibu labda wasitokee.
^^
Avemaria nimeitika wito, naomba nieleze mambo mawili niliyoyaona kwa mleta mada kadri ninavyojua.
1: MUDA WA KUKAA BILA TENDO KWA MWANAUME
Hakuna muda uliothibitishwa kisayansi kwamba baada ya muda fulani mwanaume atahitaji tendo la ndoa. Hii kwa sababu ya hali ya afya, hali ya kisaikolojia, na hali ya mahusiano baina ya wanandoa. Hali ikiwa chanya mume atamhitaji mke walau kila siku au akijitahidi kuvumilia siku tatu na si zaidi ya juma moja. Chochote kinapokuwa hasi hapo, sio tu husababisha kukosa hamu ya tendo bali pia huathiri uzalishaji wa mbegu, uchovu, na hata uhanithi
2. TATIZO LINALOMGUSA MLETA MADA
Mume wa rafiki wa mleta mada ana matatizo ya kisaikolojia zaidi, iwapo tu hakuna matatizo ya ulaji.
Namtazama kiakili zaidi kwa sababu, nia ya kuhitaji tendo la ndoa kwa mwanaume huanzia akilini na kwa mwanamke huanzia moyoni. Ikiwa mwanaume ana msongo wa mawazo ikiwa ni fedha, kazini, amekwazwa kwa lugha hasi na mkewe, au amepata taarifa inayohusu maumbile yake nje au ndani ya ndoa, au tetesi za usaliti na mengneyo yanayomuathiri mfumo wake wa akili basi atakosa hamu ya tendo la ndoa muda wote mpaka apate suluhisho.
..
SULUHISHO
Ni wakati wa mwanamke huyo, kushirikiana kwa upole, lugha njema ili abaini ana jeraha lipi la moyo. Kama hapo kabla alikuwa anajiweza vema kitandani na mhitaji mzuri, basi mke adadisi hali ya kazini, adadisi tofauti yake kazini na nyumbani na hali ikizidi anaweza kumshirikisha Daktari.
Hoja ya kuwa na mwanamke wa nje naipa nafasi ya mwisho maana uchache wa mbegu haujali ni ndani au nje bali akague mawasiliano yao yapoje na hayo niliyoeleza
^^[/QUOTE]
Yani kama mtoa mada hajauelewa ushauri huu wa Avemaria!!ushauri ni wa kitabibu haswa!!