Mulugo: Division Five haipo na sifuri ipo palepale

Mulugo: Division Five haipo na sifuri ipo palepale

Sarakasi bado ina endelea!! kesho atakuja Kawambwa na kauli yake.
 
Tz utafikiri tuko kwa waganga wa kienyeji kila mmoja anaongea ya kwake alafu serikali ni ile ile moja ya baraza moja la mawaziri na rais mmoja




Nahisi kuugua makorofindo!!
 
What does this mean? Mtendaji anaema hivi na waziri anasema kinyume chake! Ndani ya Wizara moja!
 
Kila mtendaji anatoa maoni yake, walishindwa kukubaliana kwenye vikao vya pamoja. Sasa kila mmoja kwa nafasi yake anasema anachoona kinamfaa. Maoni yangu wangefuta kabisa mitihani.
 
Kwa alivyo huyu jamaa kichwani, si ajabu akawa amekosea kama alivyokosea kuhusu Tanzania kuwa ni Muungano wa Tanganyika na kisiwa cha Zimbabwe. Tushike ya Mchome tu, huyu itakuwa kakosea.
 
Hili la kutumia CA kwenye matokeo ya mwisho litaweza kuleta changamoto nyingi sana:
- Vipi kama mwanafunzi anabadilisha masomo? Kwa mfano kuacha baadhi ya masomo anapotoka kidato pili kwenda cha tatu. Litawezekana vizuri endapo masomo yote ambayo mwanafunzi anaanza nayo kidato cha kwanza ndiyo hayo hayo anakuja kufanyia mtihani wake wa mwisho wa kidato cha nne.

Linakwenda vizuri vizuri zaidi kwa kutumia mfumo wa GPA na semester system.
 
nimemaliza mtihani wa kwanza, haukuwa mgumu sana..nategemea kupata division 5 sasa baba angu Mulugo kaifuta..bora niache mitihani nirudi kwetu...iramba kwa bro Mwigulu.
 
Kuita daraja la tano au sifuri hakuna tija yoyote kama maana yake haijabadilika. Ni sawa na kuepuka kusema mtu "amekufa" na badala yake ukasema "ametangulia mbele za haki"!
 
Kweli tuna ongozwa kwa hisia!mkulu hivi haoni aibu haya madudu ya Mawaziri wake kweli?
 
Duuuuu!!
Poor communication kati ya wizara na watendaji wake.

Unaweza ukaona namna kazi zinavyofanywa kwa ubabaishaji.

no team working and networking.
Kila kukicha ni vioja juu ya viroja.
Aaaaaaaa only in Tanzania!!
Haya twende kazi sasa.

Anaetakiwa kufanya approval za hizo ranks mpya ni waziri,so means wizara inataarifa,so means hadi news zinaenda public hana taarifa?inasikitisha sana kodi za wananchi zinalipa mishahara watu wasiostahili..miaka 3 ijayo,kiwango cha juu cha kuomba kazi itakuwa certificate maana kutakuwa hakuna mtu mwenye uwezo wa kusoma tena degree coz wanafunzi watakuwa hawana qualifications za kuingia chuo kikuu.
 
Naangalia TBC 1 hapa,naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo,amekanusha maneno ya Mchome ya kuongeza daraja la 5 na kusema daraja hilo halipo na sifuri ipo pale pale.

Source; TBC 1

Naibu waziri (mwanasiasa) vs katibu mkuu (mtendaji): tumwamini nani?
 
Hi Wizara kama haina mwenyewe...!Kila mtu anajisemea
 
Ndio kawaida ya Serikali yetu ya CCM...

Hii muvi ni kam ile ile ya Pinda na Magufuli juu ya margin ya uzito kwenye barabara zetu...

Pathetic!!!
 
Haya ni matokeo yaliyotoka ya Std 7 niliyo copy kwenye necta website kwa mmoja wapo wa watahiniwa. Tujadili hili nalo. Hivi form six itakuwaje jamani kama darasa la saba ndo hivo. Bila shaka huyu atachaguliwa kwenda sekondary!! Ingawa inasemekana kuwa wamefaulu 52% (kitu kama hicho) ukiangalia shule zote wamepasua vibaya mno maana hata hizo E ni za kutafuta. Hivi huyu ana Division ngapi? Sasa kuna divisions kwenye primary. Mungu Ibariki Tanzania.
Kiswahili - D, English - E, Maarifa - E, Hisabati - E, Science - E, Avarage Grade - E​
 
Leo Radio one akihojiwa alisema "NI BORA KUTIBU KULIKO KUZUIA" Mimi nimemzoea kuwa hatuna mtu hapo kwani huwa yeye principal yake ni "ONGEA KWANZA FIKIRI BAADAYE". Hii ndo maana mdomo wake unaweza kunena mambo ambayo ni surprise na kutuachia maswali kama huyu jamaa akili yake inachujio au la.
 
Back
Top Bottom