Mulugo: Division Five haipo na sifuri ipo palepale

Mulugo: Division Five haipo na sifuri ipo palepale

Naangalia TBC 1 hapa,naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi philipo mulugo,amekanusha maneno ya mchome ya kuongeza daraja la 5 na kusema daraja hilo halipo na sifuri ipo pale pale. Source; TBC 1

Huyu aliyesema Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na Zanzibar ndo tumwani? wakati kuna press release ya wizara inasema yote hayo?
 
Hivi Mulugo yupo madarakani kwa interest za nani kwasababu hajijui wala hajiwezi. Haiwezekani serikali hiyohiyo ije na mpango na yeye kama mdau namba moja haukanushe. Kweli alifeli shule huyu jamaa, lakini kama ni lazima awe waziri kwanini apewe wizara ya maana sana wakati wizara ya wanawake na watoto ipo akasaidiane na Sofia
 
Naangalia TBC 1 hapa,naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi philipo mulugo,amekanusha maneno ya mchome ya kuongeza daraja la 5 na kusema daraja hilo halipo na sifuri ipo pale pale. Source; TBC 1

hii serikali inaniachaga hoi sana,huwezi amini kuwa ni serikali moja cuz watu wale wale huja na matamko tofauti
 
Hivi ni vituko sasa hakuna daraja la 5 wakati kwenye matokeo ya darasa la saba kuna wanafunzi kibao wameandikiwa kuwa wamepata daraja la 5.Halafu yeye anaibuka na kusema kuwa daraja la 5 halipo.
 
Safi sana, tena sana. Walitaka kuharibu elimu yetu. Nimefurahi sana zito kurudi, Naenda grocery ya Karibu kujipongeza sasa hv
 
Naangalia TBC 1 hapa,naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi philipo mulugo,amekanusha maneno ya mchome ya kuongeza daraja la 5 na kusema daraja hilo halipo na sifuri ipo pale pale. Source; TBC 1

Aliyetoa tamko hili atakuwa ni waziri wa nchi iliyo ungana na Zibambwe wote wangekuwa viongozi wa nchi moja wasingetoa matamko yanayo sigana.
 
Nyie hamjamuelewa vizuri mulugo,kauli ya leo ameshaisema apo awali.anamanisha kuwa,div 5 ipo lakin sio chochote bado itakuwa na hadhi sawa na div0.ndio mana akasema wanafunz wasifurahie kwa sababu bado ziro ipo palepale.
 
Huo ni uthibitisho kuwa hawa jamaa wamekutupuka. Wanadai wameshirisha wadau lakini inaonekana kuja personal interest zaidi lakini walichotangaza hawakukubaliana hata wao wenyewe kwa sababu zifuatazo:
1 Gazeti la Nipashe Jmosi lilionesha kuwa Kawambwa alitofautiana na Mchome kuhusu kufutwa kwa Div zero
2. Mulugo naye anasema hakuna Div 5 prof Mchome alijichanganya wakati taarifa yao kwa umma iliyopo kwenye tovuti yao inaonesha Div Zero inefutwa.
3. Mulugo anadai kuwa viwango vya F6 hawajatoa wakati Mchome ameshavitangaza.

Hii ni aibu kwa Wizara ya Elimu kama wao kwa wao hawakuambizana, sasa wadau ni nani?
 
Kwa sasa tushike la huyu wa leo hadi hapo yatakapotokea mabadiliko, na anavyomalizia amesema alama mpya za kidato cha sita zitatangazwa pia wakishafanya "calculation".

mhhh............., hiyo ndio system.
tabu pale politics inapofanya mchezo na policy za nchi.
 
Hawa jamaa wanacheza na akili zetu, unafikiri km tungekaa kimya angekanusha hyo kauli? Sauti za watu ndo zmemfanya akanushe lakini nia yao ipo palepale.
 
Huo ni uthibitisho kuwa hawa jamaa wamekutupuka. Wanadai wameshirisha wadau lakini inaonekana kuja personal interest zaidi lakini walichotangaza hawakukubaliana hata wao wenyewe kwa sababu zifuatazo:
1 Gazeti la Nipashe Jmosi lilionesha kuwa Kawambwa alitofautiana na Mchome kuhusu kufutwa kwa Div zero
2. Mulugo naye anasema hakuna Div 5 prof Mchome alijichanganya wakati taarifa yao kwa umma iliyopo kwenye tovuti yao inaonesha Div Zero inefutwa.
3. Mulugo anadai kuwa viwango vya F6 hawajatoa wakati Mchome ameshavitangaza.

Hii ni aibu kwa Wizara ya Elimu kama wao kwa wao hawakuambizana, sasa wadau ni nani?

Viwango vya form six?? Ebu tuwekee ndugu wengine hatujaviona kama vimetoka. Je nako kuna div five?
 
Mulugo naibu waziri wa elimu mbunge wa Songwe na MNEC wa wilaya ya chunya leo akiwa ktk kipindi cha jambo Tanzania ametolea ufafanuzi wa mambo mbali mbali ya elimu na ametamka rasmi kuwa div. 5 ameifuta kuwa hata hivyo ilitamkwa kimakosa, ktk kuelezea alama za madaraja amefafanua kwa kina sana. Nimeamini kauli ya wapiga kura wake wa songwe wasemavyo MULUGO ANATOSHA.
 
Viwango vya form six?? Ebu tuwekee ndugu wengine hatujaviona kama vimetoka. Je nako kuna div five?
Hata form 6 kuna Div 5. Tembelea tovuti yao mambo yote hadharani kwa sasa siko mahali muafaka nitaweka baadaye
 
Nyie hamjamuelewa vizuri mulugo,kauli ya leo ameshaisema apo awali.anamanisha kuwa,div 5 ipo lakin sio chochote bado itakuwa na hadhi sawa na div0.ndio mana akasema wanafunz wasifurahie kwa sababu bado ziro ipo palepale.
Mkuu,mulugo amesema daraja la 5 halipo na akawashangaa walioongeza hilo daraja. Hata mtangazaji alipomuuliza waliotamka walilipata wapi? Akasema hataki kuongelea hilo na akasema anatoa tamko la wizara kuwa hakuna daraja la 5,na sifuri ipo palepale.
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Naangalia TBC 1 hapa,naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo,amekanusha maneno ya Mchome ya kuongeza daraja la 5 na kusema daraja hilo halipo na sifuri ipo pale pale.

Source; TBC 1

Nini sasa hii? Katibu Mkuu ana Wizara yake na Naibu Waziri ana Wizara yake! Ngoja aje sasa Dr. Kawambwa naye aseme.
 
Mbona wanazidi kutuchanganya? Tumuamini nani sasa Mchome au Mulugo? Au Mulugo katoa maoni yake kama raia wa kawaida na sio kiongozi wa serikali?
 
Back
Top Bottom