TOPIKI HII NAOMBA ISIUNGANISHWE NA NYINGINE MAANA INA MAAUDHUI TOFAUTI SANA NA ZILIZOJADILIWA.
UTEKELEZAJI WA MABADILIKO YA UPANGAJI WA MATOKEO YA SEKONDARI USITISHWE MARA MOJA.
Maamuzi ya kufanya mabadiliko katika alama za ufaulu na madaraja ni uamuzi uliokosa weledi na umakini.
Elimu yetu ina matatizo lukuki na inatakiwa kufanyiwa reform na si kudonoadoa tu tena pasipostahili.
1.mabadiliko yote yaliyofanywa hayatatui wala hata tatizo moja la kimfumo kwenye elimu yetu.
2.mabadiliko yaliyofanywa hayatasaidia kuondoa tatizo la wanafunzi kuanza kidato cha kwanza wakiwa hawajui kusoma na kuandika na wanaendelea mpaka kidato cha nne bado wakiwa hawajui kusoma na kuandika. Huu ni mfumo wa ajabu kabisa mana walimu wa sekondari nao wameshindwa kumwelekeza huyo asiyejua kusoma na kuandika na mbaya zaidi mfumo unamruhusu ama haumubaiani mpaka anafika kidato cha nne.haya ndio mambo ya kushughulikia.
3. mabadiliko haya hayajibu wala kuondoa tatizo la wanafunzi kwa sasa kushindwa kuielewa lugha ya kufundishia(kiingeleza) tofauti na zamani ambapo hata wale wazee waliokomea la nane walikimudu sawa sawa kiingeleza na hakukuwa na malalamiko kuwa lugha ni tatizo.
4.mabadiliko haya hayajibu wala kutatua tatizo la utungwaji na uidhinishaji wa vitabu vibovu na vya hovyo kutumika mashuleni tena vikiwemo na vya serikali mf kitabu cha hisabati kidato cha pili toleo jipya ni kitabu cha hovyo kabisa.
5.mabadiliko haya hayajibu wala kuondoa tatizo la wanafunzi kukosa uwezo wa kujieleza na kufanya kazi.
6.mabadiliko haya hayajibu wala kutatua tatizo la elimu yetu kushindwa kulisaidia taifa kupiga hatua kwenye sayansi na hatimaye mapinduzi ya viwanda.
7.mabadiliko haya hayajibu wa kutatua tatizo la mitihani kutungwa nje ya mihutasari(sylubus).
8.mabadiliko hayo hayajibu wala kuondoa tatizo la mitihani inayojibika kwa muda mrefu kuliko muda unaopangwa mf mtihani wa masaa matatu unahitaji masaa sita kuujibu.
8. mabadiliko haya hayajibu wala kuondoa tatizo la wanafunzi kukaa bila kusoma na wala kufundishwa tokea kidato cha cha kwanza hadi kidato cha nne bila kusoma hata topiki moja katika somo husika na wanapaswa kujibu mtihani sawa na aliyesoma na kufundishwa topiki zote.
9.mabadiliko haya hayatatui wala kuondoa tatizo la kukosekana kwa utunzi wa vitabu hapa nchini kwa ngazi ya kidato cha tano na sita katika masomo ya sayansi.
Kitu kibaya zaidi katika maamuzi haya ya alama na madalaja.
1. Mabadiliko haya hayajahusisha wadau wa elimu huku katibu mkuu akiamua kudanganya wazi wazi kuwa wadau walihusishwa,wakati waziri mkuu anaunda tume ilitegemewa kuwa tume ya waziri mkuu ingeweka wazi chanzo cha ubovu wa matokeo na ndipo serikali wangetutaka kufanya ama kutoa maoni ya kufanya EDUCATION GENERAL REFORM na mwisho hoja zingejadilika juu ya mapendekezo mengi na mwisho maamuzi yangeafikiwa.badala yake majibu ya panda wamekaa nayo na wakajipa maamuzi ya kuleta mabadiliko ya ajabu kabisa.
2. Hakuna chuo chochote mpaka sasa kinachojua ni alama zipi kati ya hizi mpya zinafaa kudahili mwanafunzi katika kozi ipi,ngazi ipi,ni kwa matokeo yapi mwanafunzi aka-resit kupata sifa ya kusoma kitu Fulani,mathalani inajulikana D tatu(D D D ) hazitoshi kumfanya mtahiniwa apate sifa ya kwenda kidato cha tano lakini wanajua anaweza kusoma certificate Fulani,sasa mfano atakaepata E tatu(E E E) hakuna chuo kilichojiandaa wala kujua ana qualify kusoma nini?pia kama daraja la nne la pointi 26,28,29 nk halikumfanya mwanafunzi kwenda advance lakini sasa daraja kwa pointi hizi si la nne tena bali daraja la tatu.
3. Mabadiliko haya hayajafanyiwa majaribio maana wamekurupuka sana na kuyafanya kuwa maamuzi ya dharura,utaendaje kutumia mfumo mpya katika mtihani wa mwisho kidato cha nne kwa wanafunzi ambao kwa miaka yao yote minne shuleni waliandaliwa kwa mfumo wa zamani.
Hapa tunajaribu makali ya panga kwenye shingo za watu, tutegemee wengi kuathirika,wenye matokeo watayasheherekea lakini hawa wataalamu wa baadae watakaotolewa katika mfumo huu ndio watakaoleta balaa katika kazi zao na athali zitakuwa za jamii yote,ikumbukwe maamuzi ya crash program(walimu wa bodaboda waliohitimu ualimu ndani ya miezi miwili),maamuzi ya mungai kuondoa masomo ya bishara na kilimo,maamuzi ya kuondoa mchujo kidato cha pili.
Haya ni baadhi ya maamuzi machache yaliyogharimu elimu na taifa.
HOJA ZILIZOTUMIKA NI KUFANYA MABADILIKO NI HOJA NYEPESI KWELI.
1. Utofauti wa miundo katika mitihani kati ule muundo wa Baraza la mitihani la taifa unajulikana kama FLEXIBLE GRADE RANGES yaani pamoja nakusema kuwa A inaanzia 81 baraza wanaweza kubadilisha kutokana na matokeo na kuamua ama A ianzi 70 ama 85 ama 90, na ule muundo wa unatumika katika mashule unaojulikana kama FIXED GRADE RANGES yaani mashuleni A inabakia kuwa 81 mpaka 100 bila kuajali matokeo yapoje.je hili nalo limewahi kuwa tatizo?limewahi kujadiliwa?
2. Utofauti wa alama za ufaulu zinazotumika kati ya kidato cha nne na kidato cha sita wakati elimu ni ileile ya sekondari.
Yaani Olevel kuna A,B,C,D na F wakati Alevel kuna A,B,C,D,E,S na F pia hata marks zinatofautia mfano kwa O level 81 mpaka 100 ni A wakati Alevel 75 mpaka 100 ni A.sasa hizi hoja tujiulize ni lini zimewahi kuonekana ni tatizo?ni lini zimewahi kujadiliwa?je ni tatizo kweli?