Muleba, Kagera: Mbolea ya ruzuku ya Serikali yatumika kulimia bangi

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,278
25,846
IMG_3331.JPG

Watendaji wa Vijiji na Vitongoji kadhaa wilayani Muleba, mkoani Kagera wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutumia mbolea ya ruzuku kwa kilimo cha bangi.

Mashamba makubwa manne ya bangi yamekutwa na kuteketezwa.

Katika operesheni maalum iliyofanyika chini ya Mkuu wa Wilaya ya Muleba aliyeambatana na Mkurugenzi wake wa Muleba, inadaiwa kuwa Watendaji hao walificha hata taarifa za uwepo wa mashamba hayo ya bangi.

Inasemekana kuwa bei ya bangi imepanda kutoka laki moja hadi laki mbili kwa ndoo moja.

Chanzo: ITV Habari
 
AISEE NIMEONA ITV SHAMBAA LAKIJANII SIJUI LINAMWAGILIWA NA MALORI YA MAJII DAH.. LIMETAKATAA KIJANI TUPU HK 7
 
Then serikali ikikuchukua hatua stahiki bila kujali mnakuwa wakali. Mbolea ya ruzuku watu wanalimia mihadarati ili iwe na afya...smfh!!
 
Kuitizama hiyo channel mnatafuta ugomvi na bwana yule... Tizameni Mawingu
 
Then serikali ikikuchukua hatua stahiki bila kujali mnakuwa wakali. Mbolea ya ruzuku watu wanalimia mihadarati ili iwe na afya...smfh!!
Watu wanatafuta cha kupass time, by the time they sober up its 2020... new hope
 
View attachment 470573

Watendaji wa Vijiji na Vitongoji kadhaa wilayani Muleba, mkoani Kagera wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutumia mbolea ya ruzuku kwa kilimo cha bangi.

Mashamba makubwa manne ya bangi yamekutwa na kuteketezwa.

Katika operesheni maalum iliyofanyika chini ya Mkuu wa Wilaya ya Muleba aliyeambatana na Mkurugenzi wake wa Muleba, inadaiwa kuwa Watendaji hao walificha hata taarifa za uwepo wa mashamba hayo ya bangi.

Inasemekana kuwa bei ya bangi imepanda kutoka laki moja hadi laki mbili kwa ndoo moja.

Chanzo: ITV Habari
Wallah mmea umekubali yani ni kijani tupu
Huyu mkulima ni fundi hasa
 
mbona mmea mzuri sana hivyo? rais alisema watu walime mazao yanayostaimili ukame. sasa watu wamelima ili wajipatie pesa arafu mnachoma. daah.
 
Back
Top Bottom