Mukama: CCM haijipodoi, chama hicho si jiwe, ni chama makini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mukama: CCM haijipodoi, chama hicho si jiwe, ni chama makini...

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by nngu007, Apr 15, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 15th April 2011

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amesema chama hicho si jiwe, ni chama makini, na mageuzi ilichofanya si ya kujipodoa.

  Ametamba kuwa, CCM ni chama imara ndiyo maana kimeweza kufanya mabadiliko ya uongozi bila nchi kutikisika.

  Mukama amesema, CCM ni chama kinachokua kifikra, kimuundo, na kimazingira, na kwamba mabadiliko yaliyofanywa ndani ya chama hicho si nguvu ya soda.

  “Hii sio nguvu ya soda, katu, katu, katu” na akasema hata vyama vya upinzani vinajua CCM ni namba moja.

  Ameyasema hayo mjini Dodoma wakati wa mkutano wa kuitambulisha sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyothibitishwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

  “CCM sio jiwe, CCM ni chama kinachokua… nani kama CCM, na mnakaa chini kama mpo kwenye tenga, tembeeni kifua mbele, tumeshinda” amesema Mukama katika viwanja vya Nyerere Square.

  Amewaeleza wananchi wengi wao wakiwa viongozi, wapenzi na wafuasi wa CCM kwamba, maamuzi ya Halmashauri Kuu ya CCM ilikuwa ni kutekeleza azma ya kujivua gamba.

  “Mageuzi haya yatafika mbali, na mtaona matokeo yake” amesema Mukama na kutamba kuwa yeye na sekretarieti ya chama hicho ni askari wa miamvuli, na anajivunia kuwa na damu changa katika sekretarieti ya CCM akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, na Katibu wa NEC wa siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Januari Makamba.

  “Sisi ni askari wa mwamvuli na tupo tayari kulibeba jukumu tulilokabidhiwa” amesema Mukama na kusisitiza kwamba, viongozi vijana CCM ni askari wa mwamvuli na wana dhamira ya kweli.

  “Mvuto mpya, watu wanaotaka kwenda na fasheni hawawezi kuwa wazee kama sisi, ni vijana, ni akina mama” amesema.

  Amesema, hoja zilizojadiliwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu ulioongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, zimezaa matunda stahiki.

  “Thamani ya fedha iliyotumika pale ilizaa gawio, ulikuwa na tija” amesema Mukama na kubainisha kwamba, maamuzi ya NEC CCM yalikuwa mazito, muhimu na hayajawahi kufanyika.

  Ametoa mfano wa uamuzi wa kuwapata wajumbe wa NEC kutoka wilayani badala ya mkoani kuwa ni wa kihistoria na wa kimapinduzi na si kweli kwamba thamani ya chombo hicho cha uongozi itapungua.

  “Sasa wajumbe wa NEC itabidi watazame chini…uongozi wa chama chetu umeunganisha wilaya na taifa” amesema katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi wakuu wa CCM mkoani Dodoma na makada wa chama hicho akiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, George Mkuchika, na Waziri wa Maji, Mark Mwandosya.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,912
  Trophy Points: 280
  Mvuto mpya, watu wanaotaka kwenda na fasheni hawawezi kuwa wazee kama sisi, ni vijana, ni akina mama" amesema.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,912
  Trophy Points: 280
  mmmmmmmmmmmmm
   
 4. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kama kweli mmejivua gamba tajeni wamiliki wa meremeta????
   
 5. Kibona Dickson

  Kibona Dickson Member

  #5
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuvunjwa kwa CC na Sekratariet si kujivua gamba,CCM inawahadaa na kuwapiga changa la macho watanzania,
   
 6. c

  chumakipate Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  sijui kujivua gamba hufanywa mara ngapi?na baada ya hapa wajivua nini?
   
 7. mpiganaji jm

  mpiganaji jm Member

  #7
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watoeni mafisadi na muwachukulie hatua za kisheria sio kuropoka eti nyie chama safi, msitumie ujinga wa watanzania kuwa rubuni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  njooni vyuo vikuu mpambane na wasomi nasio wakulima
   
 8. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kibaya chajitembeza? Kwani nyoka akivua gamba anabadilika kuwa binadamu? Hansa! Anaendelea kuwa nyoka tena aliyeongezeka makali na mwenye njaa. Ni kama vile chatu akishameza mnyama hulala hapohapo na huweza hadi kuzingilwa na mchwa na kila aina ya uchafu lakini siku chakula kikisha tumboni anavua gamba na kuliacha hapo na kwenda kuwinda tena. kwa maana hiyo tunategea ufisadi unaweza kuongezeka mara dufu. Labda wangesema wamemwua huyo nyoka yaani CCM kufutwa.
   
Loading...