Kobello
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 9,295
- 9,067
Mkuu,mukama hakumaanisha kuwa serikali ingetaka ruhusa ya chama.Ni upotevu wa muda,unless wantaka kuvunja serikali ya mtaa.Binafsi nakubaliana na maelezo ya Mukama kwani yana mantiki kwa kiasi fulani. Suala la Arusha ni suala la kisiasa zaidi na siyo suala la kiserikali. Ni suala ambalo mwanzo wake ni mgogoro wa kisiasa.
Hivyo, suluhu yake ya kwanza ilitakiwe iwe ya kisiasa. Hivyo, lingehitaji maamuzi ya viongozi wa kisiasa na kushirikisha viongozi wa kisiasa kwa mambo yale yanayohusu siasa. HIvyo, kama lingekuwa linahusu siasa peke yake basi lilitakiwa liwe linahusisha mazungumzo kati ya Katibu Mkuu Slaa na Katibu Mkuu Mukama na kulitafutia ufumbuzi.
Bahati mbaya, suala hili limetoka kwenye ulingo wa siasa na kuwa suala la serikali. Kwanza kutokana na taratibu za uchaguzi wa meya ambazo huongozwa na taratibu za kiserikali na pili mazingira ya maandamano na kesi zilizoko mahakamani ambazo vyote vinahusiana na suala la serikali. Kutokana na mantiki hii ya pili, tunaweza kuona kwa vile linahusiana na masuala ya serikali ya mitaa ambayo yanaangukia mikononi mwa Ofisi ya Waziri Mkuu basi hakuna mtu sahihi wa kufanya mazungumzo haya isipokuwa Waziri Mkuu.
HIvyo, Mukama hakuhitajika kabisa kuwa sehemu ya mazungumzo hayo na uhalali wa mazungumzo hayo hauitaji ridhaa, au baraka za CCM kwani suala hili si la kisiasa tena bali la kiserikali. Kutokana na hiilo kauli zote za Mukama hazihusiani na mazungumzo haya kwani Pinda hakwenda kuzungumza kama mwakilishi wa CCM bali kama kiongozi wa serikali ambaye anatafuta suluhisho la jambo ambalo linaingilia utendaji kazi wa serikali ya mitaa - in this case Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Kwa hiyo hakuna namne yoyote ambayo Pinda anaweza kutaka kibali toka CCM kufanya jambo la serikali ambalo yeye aliapa kutekeleza na kusimamia.
Ila kwenye uhalali wa serikali iliyokuwepo Arusha,Pinda hawezi kuuengua huo uhalali. Na hata akitaka kuuengua uhalali itabidi amtumie attorney general la sivyo haitakuwa haki.
Haya mazungumzo hayataaffect uwepo wa meya Lymo.