Mukama amponda Dr. Slaa Asema ni mchanga katika Duru za Siasa, Chadema ni hodari kusema Uongo

hata mimi nimeshanga sana mkama na dk slaa nani mchanga wa siasa amni au ni unafiki wa mkama
hivi kweli anaweza mfikia dk slaa kwa siasa na hata kwa mambo anayoyajua dk ni zaidi kuliko kitu kingine
 
kazi wanayo, yaani hawaoni kuwa maisha ni magumu kwetu watu wa chini? Anamponda slaa kwa sababu zisizo na msingi wowote!
 
unajua huyu mzee kwanza nacho jua ataleta ubinafsi kwenye chama chake kwa sababu ni mchoyo na ni mbinafsi hata kwenye mazingila yake anayoishi pale maeneo ya zoo tegeta majuzi kachinja ng'ombe ajakalibisha hata majirani zake kala peke yake sasa huo ni mfano mzuri wa uongozi? matokeo yake wamekuja wavua magamba wenzake ndo wamekula nyama pekee yao kitendo cha kumsema dk slaa ajatupata
 
Jamani huyu katibu mkuu wa CCM anaitwa MUKAMA na sii MKAMA, maana mtakuja haribu na kutukana jina kubwa....
 
chama cha ukoo a.k.a chama cha familia toka zamani wana msemo
'ccm ina wenyewe na wenyewe ndio sisi (yaani wao na koo zao)'

Tatizo wanawashutumu wenzao kwa yale wanayofanya wao.
 
CDM mjiande kujibu hoja sasa na sio kulia lia .... Dozi(Hoja) ndio hizo zimeanza kutoka sasa!
<br />
<br />
Kama dozi ziko hivi, ngoja ninywe maji tena ya uzima.
Eti Chadema wanawapa vijana Sh 500 ili waandamane! Haya dozi za kisisiemu sisiemu hizo jamani.
 
Labda dr. ni 'muongo', na wananchi wanaopata shida ni waongo pia!!?
Gharama za maisha 'hazijapanda'
CcM ni chama 'bora' kuliko vyote Afrika labda na 'ulimwenguni kote'
CcM 'hakuna' wezi nk.
Labda huo ni 'ukweli'
 
WA ZAMANI ALIKUWA NA NUNDU WA SASA ANA UPARA, CDM NI CHAMA CHA UKOO FULANI, SAWA, KUNA MBOWE NDUGU YAKE NI NANI MWINGINE CDM? WENJE KUNA WENJE MWINGINE CDM, MAREHEM SHELEMBI KUNA SHELEMBI MWINGINE CDM,ZITTO KUNA ZITTO MWINGINE CDM?

CCM KUNA YUSUF MAKAMBA PIA KUNA JANUARY MAKAMBA
2. JAKAYA KIKWETE KUNA RIDHWAN KIKWETE
3.ALLY HASSAN MWINYI KUNA HUSSEIN MWINYI
4.MOSES NNAUYE KUNA NAPE NNAUYE
5.JOHN NCHIMBI KUNA EMMANUEL NCHIMBI
6.ROSTAM AZIZ KUNA HUSSEIN BASHE
7. SAMUEL SITTA NA MAGRET SITTA


WANATAKA AKIMALIZA KIKWETE AMPE HUSSEIN MWINYI NA BAADA YA HUSSEIN MWINYI NI RIDHWAN KIKWETE, AMA KWELI CCM NI GAMBA
wOTE HAO NI WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAGAMBA MTU NA MTOTO WAKE , KAMA WANATAKA TUWAWEKEE AU TUWATAJE NA MAHAWARA ZAO WALIOWAPA NAFASI KWENYE MAGAMBA

mkuu naongeza data Karume family imejaa ccm, kuna msekwa kuna ana abdala.
 
Eti Misri inaongzwa kijeshi na watu 50,000 wanakamatwa kila siku!!! Hii kweli ni kali ya mwaka...Inaonekana hata habari huwa hafatilii huyu, maana angekuwa anajua anachosema asingeleta huu upupu wake kuhusu Misri na role ya jeshi kwenye suasa za Misri...ama kweli huwezi kujua mtu ana busara hadi pale utakapomsikia akiongea.

Huyu jamaa anaunganishaga mifano bila kuangalia kama inarelate au la! Ukiisikia hotuba yake utasikia misemo inapachikwa tu ili mradi ni msemo. Natamani nikae namsikia Mpoki akiongea kwa sababu Mkama naona ni Ze Komedi kwenye mambo ya msingi.
 
Napendekeza waandaliwe mdahalo wa wazi kati ya Slaa na Mukama,tujue nani mchanga kwenye siasa

Yaaah itafahamika mbichi na mbivu
 
mukama welcome to the politics battles vs chadema,be prepared always beacause CDM is the party of GENEOUS,you ll get heart attack if you wont take care aseeee
 
* Huyu Mukama ni mgonjwa anasema Wananchi wajifunze ya Misri Eti Kuandamana kwao kama Chadema kumeashiria Nchi kuongozwa Kijeshi

Wednesday, 11 May 2011 11:11 newsroom

NA WAANDISHI WETU - GAZETI LA UHURU

KATIBU Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, amemponda Dk. Wilbroad Slaa na kusema ni mwanasiasa anayejifunza. Amemfananisha Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA na mtu anayebadilisha dini na kujifanya mjuaji kuliko aliowakuta na matokeo yake anaropoka kila kukicha na kutoa matamshi ya vitisho kwa wananchi. Mukama alisema CCM inajadili mambo
yake kwa uwazi na kilichofanyika ni mabadiliko ya kukijenga upya Chama na si vinginevyo, na kwamba kwa kutoa maneno ya uzushi Dk. Slaa ni sawa na mtoto anayelilia wembe, siku moja utamkata. Pia, amesisitiza kwamba hakuna waraka wa siri.


awilson%20mukama.jpg


Aliyasema hayo jana, wakati akifafanua kauli ya iliyotolewa na Dk. Slaa kupitia gazeti moja la kila siku lenye kichwa cha habari Dk. Slaa: Nchi haitatawalika, Anasa waraka wa siri wa CCM.
Katika gazeti hilo, Dk. Slaa alikaririwa akizungumza katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Msakila mjini Sumbawanga ambapo alisema amebaini waraka wa siri wa CCM uliokuwa na muhuri wa SIRI ambao amedai CCM imekiri kuwa haikubaliki.

Mukama alisema Dk. Slaa, haelewi nini maana ya nchi kutotawalika kwani Tanzania ni nchi inayoendeshwa kwa misingi ya demokrasia, inawekezeka kiuchumi na wananchi wanaishi kwa amani na utulivu.

Dk. Slaa hana karama ya kutawala, kiongozi makini hupima hata matamshi yake, anazangumza mambo yenye mwelekeo wa kuwakosesha amani, lakiniwakati wao wakiendelea na maandamano, Serikali ya CCM inajenga miundombinu ya kusafirisha mazao, alisema.

Aliwataka wananchi wajifunze yanayotokea Misri, ambako wameandamana na sasa wanaongozwa na jeshi la nchi hiyo, kila siku watu 50,000 wanakamatwa na kuhukumiwa.

Alisema CHADEMA ni hodari wa kusema uongo, kwa kutumia haki yao ya kujieleza kusambaza uzushi na kwamba CCM haiwezi kushindana nao kwa kuzua mambo.

Mukama alisema wamekuwa wakiwapatia vijana sh. 500 kuwavuta kwenye maandamano na kuwadanganya kwamba watawaondolea umasikini kupitia maandamano hayo.

Akizungumzia kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa, alisema chanzo ni matatizo ya kisiasa yaliyozikumba nchi za Magharibi ikiwemo Libya ambao ndio wenye visima vya mafuta, nishati hiyo imepanda bei katika soko la dunia, na viwanda vyote nchini vinaendeshwa kwa kutegemea mafuta.

Hakuna siri yoyote CCM, imejipanga kuboresha utendaji wa Chama kwa kuangalia vigezo vya msingi, na kila kimoja kimepitia kwenye vikao halali vya kikatiba, alisema.

Akifafanua Mukama alisema CCM si kundi la watu ama ukoo fulani kama ilivyo CHADEMA, bali ni Chama kinachoendeshwa kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake tangu enzi za TANU na ASP.

Alisema katika mkakati wa kufanya mageuzi CCM ilipanga kuboresha mambo muhimu, ikiwemo fikra na itikadi, muundo wake, viongozi wa Chama, watendaji, usalama na maadili, wanachama na kujiimarisha kiuchumi na fedha.

Mukama alisema vigezo hivyo vyote havina usiri bali ni mikakati ambayo imewekewa mipango ya utekelezaji kwa maana ya kuunda CCM yenye mwelekeo tofauti.

Alitoa mfano wa mambo yaliyobadilishwa ni kufanya uchaguzi wa Chama na jumuia kwa mwaka mmoja ili kupunguza muda wa kushughulikia uchaguzi kutoka miaka mitatu kwenda minne.
ÒMiaka mitano ya utawala, ni mwaka mmoja tu ndo hatufanyi uchaguzi, mwakani tuna uchaguzi wa Chama , tumeona tufanye pamoja na jumuia, ili tupumzike 2013, 2014 tubaki na uchaguzi wa serikali za mitaa na 2015 uchaguzi mkuu, alisema.

Alisema pia katika usalama na maadili, iliangaliwa viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kwa rushwa na vitendo vingine viovu, ilionekana hawawezi kusimamia vitendo vya kimapinduzi ambavyo Chama kinavitekeleza.

Ni jambo la kawaida kufanya marekebisho hususan katika kipindi ambacho CCM inakubalika kwa wananchi, bado tuna nafasi kubwa hata katika uchaguzi wa 2010 imedhihirisha tumepata majimbo 187 mara tisa zaidi ya majimbo 22 ya CHADEMA, alisema.

Alisema matokeo ya uchaguzi huo yamebainisha kwamba CCM bado inakubalika kwani hata wabunge wa viti maalumu ambao hupatikana kutokana na wingi wa kura , CCM ina wabunge 67 na vyama vingine vina wabunge 35.

Hivi karibuni CCM ilifanya mabadiliko makubwa kwa kujivua gamba kwa baadhi ya viongozi waandamizi, walijizulu na kujipanga upya, ambapo nafasi ya Katibu Mkuu iliyoachwa wazi na Yussuf Makamba ilichukuliwa na Mukama.

Siku chache baada ya mabadiliko hayo, baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi ndani ya CCM, walianza njama za kuwachafua viongozi waandamizi akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Kwa haya matapishi aliyoongea Mukama natabiri Chuo chetu cha Morogoro kimpe PhD ya heshima
 
Mukama achana na hayo (ya dr slaa) kwa sasa rekebisha uteuzi wa makatibu wako kwani unaboa hasa wana-ccm mfano uteuzi wa kyela kupelekewa mtu mhuni kwa sababu tu ana kadi ya ccm na anajua fitina,na sasa baada ya kukatliwa mmempeleka makete, haieleweki ndiyo kujivua gamba au kuvaa gamba? Rekebisha chama achaneni na usanii mnamuangusha kikwete. Chama kinaendeshwa zaidi kwa ubabe na majungu hatuwezi fika hii yote ni kutokana na kupeana kazi kwa fadhila na urafiki ovyoo?
 
Tumeshajua busara za mukama. hatuhitaji kufikiria zaidi kuwa makamba ni bora kuriko huyu the man with zero facts(the man with total lack of informations). Jamaa amechaguriwa kumalizia kifo cha chama cha magamba. Tusubiri tuone,no sooner the time will tell.
 
Yego Mukama,
Mbona unatuangusha hivyo.... si uwe unatuomba ushauri kuliko kuropoka hivyo!!

Mwana wasu, ebu rekebisha mambo ukiandae vyema chama chako kuwa chama kikuu cha upinzani. Hizo ziara mnazofanya za kichama kwa kutumia ruzuku iliyoisha pungua kitakimaliza kabisa hicho chama chako. Hamtakuwa na fedha nyingine za EPa kwa ajiri ya uchaguzi mwaka 2015 na ndo mwanzo wa kuingia mkenge na kuwa chama cha upinzani.
 
Mukama hivi unafikiri Watanzania ni wajinga kama wewe?
Wilson-Mukama1.jpg

Ukichaa wenu na ufisadi wenu mnafikiri sisi tunavichwa maji kama vyenu sio. Umepewa nafasi na fisadi kikwete sasa unaona kama dunia imekushukia leo. Unachofikira sasa ni kujenga, kuhamisha utajiri wa Watanzania na kuwasomesha watoto wako na ndugu zako kutumia tax payer money sio. Tunawaelewa nyie kwa miaka 50 sasa... mpaka leo hii mmetuletea umaskini na wizi wa kipindukia. Ondokeni serikalini kabla ya hatujachkua hatua zetu mikoni. Unamzungumzia Dr Slaa badala ya kikwete aliekaa ikulu kwa wizi na hata kazi yenyewe ni usanii mtupu. Alileta Richmond ni nani? Alieleta EPA ni nani, alileta Dowans ni nani? Alieleta majanga muhimbili ni nani? Alijaza watoto wasiosoma mitaani ni nani? Mnachoongea ni wajinga watawasikiza
 
mukama welcome to the politics battles vs chadema,be prepared always beacause CDM is the party of GENEOUS,you ll get heart attack if you wont take care aseeee
Hapo kwenye red,sidhani kama ni typo.....ni yaleyale ya kutumia cofta kutibu kifua kikuu!!
 
Yego Mukama,
Mbona unatuangusha hivyo.... si uwe unatuomba ushauri kuliko kuropoka hivyo!!

Mwana wasu, ebu rekebisha mambo ukiandae vyema chama chako kuwa chama kikuu cha upinzani. Hizo ziara mnazofanya za kichama kwa kutumia ruzuku iliyoisha pungua kitakimaliza kabisa hicho chama chako. Hamtakuwa na fedha nyingine za EPa kwa ajiri ya uchaguzi mwaka 2015 na ndo mwanzo wa kuingia mkenge na kuwa chama cha upinzani.
Mkuu huyu jamaa sii wa nyumbani usimpe sifa hizo!..Hayupo ktk ukoo wa wasilanga..
 
WA ZAMANI ALIKUWA NA NUNDU WA SASA ANA UPARA, CDM NI CHAMA CHA UKOO FULANI, SAWA, KUNA MBOWE NDUGU YAKE NI NANI MWINGINE CDM? WENJE KUNA WENJE MWINGINE CDM, MAREHEM SHELEMBI KUNA SHELEMBI MWINGINE CDM,ZITTO KUNA ZITTO MWINGINE CDM?

CCM KUNA YUSUF MAKAMBA PIA KUNA JANUARY MAKAMBA
2. JAKAYA KIKWETE KUNA RIDHWAN KIKWETE
3.ALLY HASSAN MWINYI KUNA HUSSEIN MWINYI
4.MOSES NNAUYE KUNA NAPE NNAUYE
5.JOHN NCHIMBI KUNA EMMANUEL NCHIMBI
6.ROSTAM AZIZ KUNA HUSSEIN BASHE
7. SAMUEL SITTA NA MAGRET SITTA


WANATAKA AKIMALIZA KIKWETE AMPE HUSSEIN MWINYI NA BAADA YA HUSSEIN MWINYI NI RIDHWAN KIKWETE, AMA KWELI CCM NI GAMBA
wOTE HAO NI WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAGAMBA MTU NA MTOTO WAKE , KAMA WANATAKA TUWAWEKEE AU TUWATAJE NA MAHAWARA ZAO WALIOWAPA NAFASI KWENYE MAGAMBA

Wakuu, hii nimeipenda ... lol. Magamba nomaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom