Mukama amponda Dr. Slaa Asema ni mchanga katika Duru za Siasa, Chadema ni hodari kusema Uongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mukama amponda Dr. Slaa Asema ni mchanga katika Duru za Siasa, Chadema ni hodari kusema Uongo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 11, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  * Huyu Mukama ni mgonjwa anasema Wananchi wajifunze ya Misri Eti Kuandamana kwao kama Chadema kumeashiria Nchi kuongozwa Kijeshi

  Wednesday, 11 May 2011 11:11 newsroom

  NA WAANDISHI WETU - GAZETI LA UHURU

  KATIBU Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, amemponda Dk. Wilbroad Slaa na kusema ni mwanasiasa anayejifunza. Amemfananisha Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA na mtu anayebadilisha dini na kujifanya mjuaji kuliko aliowakuta na matokeo yake anaropoka kila kukicha na kutoa matamshi ya vitisho kwa wananchi. Mukama alisema CCM inajadili mambo
  yake kwa uwazi na kilichofanyika ni mabadiliko ya kukijenga upya Chama na si vinginevyo, na kwamba kwa kutoa maneno ya uzushi Dk. Slaa ni sawa na mtoto anayelilia wembe, siku moja utamkata. Pia, amesisitiza kwamba hakuna waraka wa siri.


  [​IMG]

  Aliyasema hayo jana, wakati akifafanua kauli ya iliyotolewa na Dk. Slaa kupitia gazeti moja la kila siku lenye kichwa cha habari Dk. Slaa: Nchi haitatawalika, Anasa waraka wa siri wa CCM.
  Katika gazeti hilo, Dk. Slaa alikaririwa akizungumza katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Msakila mjini Sumbawanga ambapo alisema amebaini waraka wa siri wa CCM uliokuwa na muhuri wa SIRI ambao amedai CCM imekiri kuwa haikubaliki.

  Mukama alisema Dk. Slaa, haelewi nini maana ya nchi kutotawalika kwani Tanzania ni nchi inayoendeshwa kwa misingi ya demokrasia, inawekezeka kiuchumi na wananchi wanaishi kwa amani na utulivu.

  Dk. Slaa hana karama ya kutawala, kiongozi makini hupima hata matamshi yake, anazangumza mambo yenye mwelekeo wa kuwakosesha amani, lakiniwakati wao wakiendelea na maandamano, Serikali ya CCM inajenga miundombinu ya kusafirisha mazao, alisema.

  Aliwataka wananchi wajifunze yanayotokea Misri, ambako wameandamana na sasa wanaongozwa na jeshi la nchi hiyo, kila siku watu 50,000 wanakamatwa na kuhukumiwa.

  Alisema CHADEMA ni hodari wa kusema uongo, kwa kutumia haki yao ya kujieleza kusambaza uzushi na kwamba CCM haiwezi kushindana nao kwa kuzua mambo.

  Mukama alisema wamekuwa wakiwapatia vijana sh. 500 kuwavuta kwenye maandamano na kuwadanganya kwamba watawaondolea umasikini kupitia maandamano hayo.

  Akizungumzia kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa, alisema chanzo ni matatizo ya kisiasa yaliyozikumba nchi za Magharibi ikiwemo Libya ambao ndio wenye visima vya mafuta, nishati hiyo imepanda bei katika soko la dunia, na viwanda vyote nchini vinaendeshwa kwa kutegemea mafuta.

  Hakuna siri yoyote CCM, imejipanga kuboresha utendaji wa Chama kwa kuangalia vigezo vya msingi, na kila kimoja kimepitia kwenye vikao halali vya kikatiba, alisema.

  Akifafanua Mukama alisema CCM si kundi la watu ama ukoo fulani kama ilivyo CHADEMA, bali ni Chama kinachoendeshwa kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake tangu enzi za TANU na ASP.

  Alisema katika mkakati wa kufanya mageuzi CCM ilipanga kuboresha mambo muhimu, ikiwemo fikra na itikadi, muundo wake, viongozi wa Chama, watendaji, usalama na maadili, wanachama na kujiimarisha kiuchumi na fedha.

  Mukama alisema vigezo hivyo vyote havina usiri bali ni mikakati ambayo imewekewa mipango ya utekelezaji kwa maana ya kuunda CCM yenye mwelekeo tofauti.

  Alitoa mfano wa mambo yaliyobadilishwa ni kufanya uchaguzi wa Chama na jumuia kwa mwaka mmoja ili kupunguza muda wa kushughulikia uchaguzi kutoka miaka mitatu kwenda minne.
  ÒMiaka mitano ya utawala, ni mwaka mmoja tu ndo hatufanyi uchaguzi, mwakani tuna uchaguzi wa Chama , tumeona tufanye pamoja na jumuia, ili tupumzike 2013, 2014 tubaki na uchaguzi wa serikali za mitaa na 2015 uchaguzi mkuu, alisema.

  Alisema pia katika usalama na maadili, iliangaliwa viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kwa rushwa na vitendo vingine viovu, ilionekana hawawezi kusimamia vitendo vya kimapinduzi ambavyo Chama kinavitekeleza.

  Ni jambo la kawaida kufanya marekebisho hususan katika kipindi ambacho CCM inakubalika kwa wananchi, bado tuna nafasi kubwa hata katika uchaguzi wa 2010 imedhihirisha tumepata majimbo 187 mara tisa zaidi ya majimbo 22 ya CHADEMA, alisema.

  Alisema matokeo ya uchaguzi huo yamebainisha kwamba CCM bado inakubalika kwani hata wabunge wa viti maalumu ambao hupatikana kutokana na wingi wa kura , CCM ina wabunge 67 na vyama vingine vina wabunge 35.

  Hivi karibuni CCM ilifanya mabadiliko makubwa kwa kujivua gamba kwa baadhi ya viongozi waandamizi, walijizulu na kujipanga upya, ambapo nafasi ya Katibu Mkuu iliyoachwa wazi na Yussuf Makamba ilichukuliwa na Mukama.

  Siku chache baada ya mabadiliko hayo, baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi ndani ya CCM, walianza njama za kuwachafua viongozi waandamizi akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete.
   
 2. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hapo ndio anapoharibu, kuponda yaliyotokea Misri. Yeye ajibu hoja tu za Dr Slaa kama alivyofanya, inatosha
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii timu ya magamba inakera mno kama si kutuchosha, kila kukicha wao ni kusema Dr Slaa muongo, chadema waongo! hivi sisi wananchi hatuna uweza wa kutambua uwongo na ukweli mpaka hawa ma-'grandie' watuambie what is what?! Do not insult our intelligence we cant tell a lie when we hear it. And to prove my point Mukama & Co waangalie a sample ya lies from thier own closet;

  1- Maisha bora kwa kila mtanzania - CCM Presidential candidate promise 2005-2010
  2. Mgao wa umeme mwisho - Ngeleja 2010
  3. Serikali haijakopa benki za ndani - Mkullo May 2011
  4.
  5.
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Si alishasema hakuna tena siku tisini kwa mfisadi, akaechini na akae kimya, hana lolote si chochote ni mnafiki tu. alikua anatamani nafasi ya Makamba tu.:A S-baby:
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  Mwacheni,mdomo mali yake haulipii kodi.Ameshaanza kulewa madaraka.
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huyu sasa kwa pumba kumbe ni zaidi ya makamba
   
 7. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hizi data za Mukama zinatokea wapi, watu 50000 per day!!
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Anaogopesha Wananchi kutetenda Maandamano hajui kuwa huko Singida Nape anafanya hivyo pia tatizo ni watu wanaokwenda ni wale wanaopata or waliopata bidhaa kama Khanga, Scuff, Shati, Kofia n.k
   
 9. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu kama hajajiandaa ataharibu mambo sasa, sababu DR lazima amjibu. hatomuacha hata kidogo
  na ninatabiri kwa majibu atakayopewa ataingia mitini, hatosikika tena akijaribu kumchokonoa DR,
  na hata akiulizwa atasema kazi za katibu mkuu sio kuongea kwenye majukwaa

  subirini muone
   
 10. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbavu sina!! na hivyo anaupara!! bora nundu????
   
 11. SAUTI YA ZEGE

  SAUTI YA ZEGE Member

  #11
  May 11, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Wilson Mukama!!,"anasema kuwa Dr.ni mchanga wa siasa,hivi kati yake na Slaa ni nani mchanga wa siasa?,mbona alikuwa hafahamiki kwenye ulingo wa siasa.Mfa maji haachi kutapatapa,anapayuka sana ni afadhali ya Makamba.
   
 12. p

  plawala JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napendekeza waandaliwe mdahalo wa wazi kati ya Slaa na Mukama,tujue nani mchanga kwenye siasa
   
 13. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Atakimbia jukwaa la mdahalo, wana jamvi mimi nilikuwa nampenda sana Makamba kwa udhaifu wake kwani ilikuwa ni turufu ya wanamageuzi lakini alipokuja Mukama nikafikiri tumenyang'anywa turufu yetu lo! kumbe tume-double kwenye turufu Mungu atupe nini tena zaidi ya hilo. Viva Mukama tuangushie hilo li-mnyama CCM kwa kuropoka na kusema uongo
   
 14. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Eti Misri inaongzwa kijeshi na watu 50,000 wanakamatwa kila siku!!! Hii kweli ni kali ya mwaka...Inaonekana hata habari huwa hafatilii huyu, maana angekuwa anajua anachosema asingeleta huu upupu wake kuhusu Misri na role ya jeshi kwenye suasa za Misri...ama kweli huwezi kujua mtu ana busara hadi pale utakapomsikia akiongea.
   
 15. B

  BUBERWA D. JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  hawa CCM wameondoa afadhali wameingiza potelea mbali.
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  CDM mjiande kujibu hoja sasa na sio kulia lia .... Dozi(Hoja) ndio hizo zimeanza kutoka sasa!
   
 17. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Eti CHADEMA wanawalipa wale waandamanaji sh.500 ili waandamane....CCM sio chama cha Kikabila au ukoo kama CDM hii na yenyewe ni kali walisema ni chama cha wachaga sasa wajiulize Sugu,zitto,Silinde,Shibuda,Wenje,Msigwa,Vicent,Kaihula, Regia n.k n.K ni wachaga wa wapi au wote ni watu wa kaskazini???.....hizi hoja za ukanda na udini hunikumbusha ile signature ya moja ya member wa hapa JF kuwa hiyo singo ilishachuja
   
 18. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  WA ZAMANI ALIKUWA NA NUNDU WA SASA ANA UPARA, CDM NI CHAMA CHA UKOO FULANI, SAWA, KUNA MBOWE NDUGU YAKE NI NANI MWINGINE CDM? WENJE KUNA WENJE MWINGINE CDM, MAREHEM SHELEMBI KUNA SHELEMBI MWINGINE CDM,ZITTO KUNA ZITTO MWINGINE CDM?

  CCM KUNA YUSUF MAKAMBA PIA KUNA JANUARY MAKAMBA
  2. JAKAYA KIKWETE KUNA RIDHWAN KIKWETE
  3.ALLY HASSAN MWINYI KUNA HUSSEIN MWINYI
  4.MOSES NNAUYE KUNA NAPE NNAUYE
  5.JOHN NCHIMBI KUNA EMMANUEL NCHIMBI
  6.ROSTAM AZIZ KUNA HUSSEIN BASHE
  7. SAMUEL SITTA NA MAGRET SITTA


  WANATAKA AKIMALIZA KIKWETE AMPE HUSSEIN MWINYI NA BAADA YA HUSSEIN MWINYI NI RIDHWAN KIKWETE, AMA KWELI CCM NI GAMBA
  wOTE HAO NI WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAGAMBA MTU NA MTOTO WAKE , KAMA WANATAKA TUWAWEKEE AU TUWATAJE NA MAHAWARA ZAO WALIOWAPA NAFASI KWENYE MAGAMBA
   
 19. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mukama, the 'bottle neck' ndiye ameonekana angalau ana nguo yenye vilaka dhidi ya wenzake ambao hawajavaa kabisa!
  Ila kwa vile wote ni Vipofu yeye amechaguliwa na wale wenye jicho moja moja.
   
 20. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  Mukama kumbe ni kama waziri wa zamani wa Sadam, sahaf. Yeye na Dr Slaa nani mchanga kwenye siasa? Umma ndio tunamsikia sasa hivi tu kwamba kuna mtu anaitwa mukama.
  Halafu hutu jamaa ni bingwa wa kuongea bila data, ndie huyu aliyedanganya jf ni mali ya chedema na sasa anakuja na takwimu za watu 50,000 kukamatwa kila siku Misri, kazipata wapi? Na hata kama wapo wanaokamatwa ni wa chama kilichokuwa kinatawala maana kilifutwa na mpaka sasa mawaziri wake washahukumiwa mvua kadhaa jela. Kama jeshi linaweza kuchukua nafasi ya kuliwajibisha joka ccm ni afadhali wachukue nchi tena tutawapokea kwa mikono yote miwili.
  .
   
Loading...