The moment alipoteuliwa kuwa Katibu mkuu wa CCM he turned into gamba automatic. Kuna faida na hasara za kutumia hila kubakia madarakani, faida ni kuwa utaendelea kuliibia Taifa na kula bila aibu, hasara ni kuwa unakosa legitimacy ya kuwa kiongozi wa watu. Kiongozi ni yule mwenye uwezo wa kuwa-inspire watu, ukiisha ona kuwa umma haupo na wewe basi ni wakti muafaka wa kutafuta njia ya kutokea. CCM and its parents TANU and ASP wamekuwa wakitawala Tanzania tokea tupate uhuru. Kwa mantiki ya kawaida tu kama kwa miaka hamsini umeshindwa kubadilisha hali ya maisha ya wananchi ni dhahiri utakosa mvuto mbele yao. Watanzania wanahitaji mabadiliko ya kweli siyo ya awamu za uongozi ndani ya watu walewale.
The only legacy CCM itakayoweza kuwaachia watanzania ni ku-set precedence ya demokrasia ya kweli na huru. waruhusu katiba mpya ya watanzania, wakubali kuwa unaweza ukashindwa ukiwa ndani ya CCM ila pia unaweza ukashinda ukiwa nje ya CCM. CCM si baba wala mama wa watanzania na CCM si moyo wa Tanzania bali ni just a single cell like any other parties and stakeholders. Vinginevyo watajikuta wanabaki ni chama cha viongozi wa chama na dola ambao wanafaidika moja kwa moja kwa kushika nafasi zao hizo.