Mukama aibuka, aishambulia CHADEMA!

Mukama aibuka, aishambulia CHADEMA!

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
*Asema inakabiliwa na ukame wa viongozi waliopikika kimaadili
* Hata kupata wagombea hutegemea 'iokoteze' walioshindwa michujo au chaguzi za CCM
* Asena kwa mtaji huo haiwezi kuwa chama chenye tija na hatma njema kwa taifa.


NA BASHIR NKOROMO

KATIBU Mkuu wa CCM, Wilson Mukama amesema Chadema hakiwezi kuwa chama chenye tija na hatma njema kwa taifa kutokana na kulazimika kuokoteza hata wagombea wake kutokana na wanaoshindwa kwenye michujo au chaguzi ndani ya CCM. Alisema, Chadema na vyama vingine vya upinzania hapa nchini, vinazama katika hali hiyo, kutokana na kutokuwa na tanuru imara linalowawezesha kutoa viongozi waliopikika kimaadili, kama ilivyo ndani ya CCM. Amesema, Chadema wanaposema, kwamba kwa CCM kutowafukuza au kuwanyima uongozi baadhi ya wana-CCM ni kuizika CCM, huko ni kulia kinyume kwamba kwa kutofanya hivyo CCM imewakosesha watu ambao wangehamia kwao hivyo chama chao kinakufa.

Mukama alisema hayo jana wakati wa sherehe ya kuwapongeza wana-CCM Kata ya Msasani kwa kukamilisha chaguzi zao ndani ya chama katika kata hiyo, iliyofanyika kweny6e ukumbi wa Maisha Club, Msasani jijini Dar es Salaam. Mukama alisema, CCM ni taasisi iliyojengwa katika misingi imara na mshikamano wake ni kama ngumi inayoundwa na vidole vitano na kitaendelea kuwa imara kwa sababu viongozi wake wanatokana na tanuru lililowapika kimaadili wakapikika.

"CCM bwana ni tasisi yenye viongozi wenye chimbuko la maadili, siyo kama vyama vingine vinaongozwa na wenye vilabu vya usiku halafu eti navyo ni vyama vya kuweza kuongoza nchi", alisema Mukama. Alisema kutokana na CCM kuwa chama chenye chimbuko la maadili bora, ndiyo sababu kila kinapofanya uchaguzi wa kupata viongozi wake huwa ni wa kihistoria kwa kuwa anayepenya kuwa kiongozi huwa amepita kwenye tanuru la uchujwaji wa hali ya juu.

"Juzijuzi tulipokuwa tunateua majina ya wagombea, Kamati yetu ya maadili, haikuacha kuchunguza hatua kwa hatua na kwa makini kama kila aliyeomba uongozi anazo sifa bora na zinakidhi viwango vya kushinda anayetakiwa kuondolewa yeye abaki, hivi ndivyo chama chenye misingi ya uadilifu ya uongozi kinavyokuwa", alisema Mukama na kuongeza:- "Sasa hivi vyama vingine vinaweza kufanya mchujo wa aina hii? thubutu.

Si mlisikia juzi juzi mbunge mmoja alijaribu kuonyesha nia ya kutaka uenyekiti wa Chama fulani, wee mliona alivyofurumushwa". Mukama alisema, wanaosema CCM inakufa ni wavivu kufanya tathmini au wanasema hivyo kudanganya watu na nafsi zao huku wenyewe wakiwa wanajua kwamba CCM ni imara tena kwa vigezo.

"Hivi jamani tujiulize na wao (wapinzani) wakitaka pia wajiulize chama chenye mwelekeo wa kufa kinaweza kupata wagombea ambao ni Wazee, Vijana kina baba na kina mama tena wengi wasomi kabisa waliobobea hadi ngazi za uprofesa, wanaokanyagana kwa wingi kama tulivyoona wakiomba uongozi katika nafasi mbalimbali? ", alihoji Mukama. Alisema, tutokana na hali ya uchaguzi ndani ya Chama iliyojionyesha katika ngazi za mikoa, baada ya kumalizika ngazi ya taifa, CCM itakuwa itakuwa imara zaidi tayari kwa kutwaa dola tena baada ya uchaguzi mkuu wa 2015.

Katika hafla hiyo, wanachama wa Kata hiyo, waliuopongeza uongozi wa juu wa CCM kwa namna ulivyoweza kuweka taratibu zilizo wazi na za haki katika kuhakikisha uchaguzi ndani ya chama unazaa viongozi walio dhabiti. Mapema, Mukama alikabidhi hati kwa vijanan na makamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM, ambao wameshiriki katika shughuli mbali mbali za kuimarisha chama kwa namna moja au nyingine.
 
huyu ndiye walimtegemea kuwasaidia kuleta mabadiliko ndani ya ccm kupitia ile kamati yake ya uchunguzi sasa naye anatuambia kuwa ccm haina matatizo na wanaosema ina matatizo wanajidanganya. mapendekezo yake yote aliyoyatoa kumpa mwenyekiti wake jk kuhus matatizo yaliyopo ndani ya ccm kumbe alikuwa akimdanganya.
 
huyu ndiye walimtegemea kuwasaidia kuleta mabadiliko ndani ya ccm kupitia ile kamati yake ya uchunguzi sasa naye anatuambia kuwa ccm haina matatizo na wanaosema ina matatizo wanajidanganya. mapendekezo yake yote aliyoyatoa kumpa mwenyekiti wake jk kuhus matatizo yaliyopo ndani ya ccm kumbe alikuwa akimdanganya.

Watu wanatoleana bastola ili wachaguliwe yeye haoni kuwa ni tatizo
 
Tambwe Hiza, Msabaha, Shaibu Akwilombe, Dr Aman Walid Kabouru, Masumbuko Lamwai, Makongoro Nyerere... all of these have been in the opposition... and the list goes on
 
huyo hata hana hadhi...,ebu tu kwanza angalieni mavazi yake pamoja na kofia anayovaaga....!
 
hana jipya huyo asubirie 2015 ifike aone wanavogaragazwa kama mbwa mwizi
 
Mukama alisema hayo jana wakati wa sherehe ya kuwapongeza wana-CCM Kata ya Msasani kwa kukamilisha chaguzi zao ndani ya chama katika kata hiyo, iliyofanyika kweny6e ukumbi wa Maisha Club, Msasani jijini Dar es Salaam. "CCM bwana ni tasisi yenye viongozi wenye chimbuko la maadili, siyo kama vyama vingine vinaongozwa na wenye vilabu vya usiku halafu eti navyo ni vyama vya kuweza kuongoza nchi", alisema Mukama.

Hivi nchi hii ukiwa na kilabu cha usiku ni 'dhambi kubwa' kiasi chama chako hakipaswi kuongoza nchi...bali ukiwa fisadi na mbadhirifu wa rasilimali za umma unakuwa umepikika 'kimaadili' na kutamba kuwa unastahili kuongoza nchi! Kama vilabu vya usiku ni vibaya kiasi hicho, walifuata nini 'Maisha Club'? Kwa nini Mukama hakukataa alipoalikwa kwenda Maisha Club ikiwa watu wanaojihusisha na hizo club hawana maadili na hawafai kushika uongozi wa nchi!?
 
Magamba aliyoahidi kuyavalia njuga kuyavua iliishia wapi? Kashindwa kuyavua, na wenye nayo wanaendelea kudunda ndani ya CCM, naye anaridhika! Anakubali kula matapishi aliyoyatyema!

Kitu hii ni katika CCM pekee duniani ndiyo utakuta!
Mafisadi wamemshinda kuwatokomeza ndani ya CCM, halafu eti anaijia juu CDM, kwani wao CDM ndiyo iliwaweka?

You and your party are sinking fast!

Kuna binti mmoja mdogo tu jana ktk kongomano la Mwl Nyerere kule UDSM aliongea vitu vya maana kuhusu ukombozi wa pili wa Mtanzania, kuliko pumba hizi za Mukama. Mukama jiulize, kwa nini binti huyo asichague kuingia CCM?

Aingia kwa mafisadi? Pu!!!!
 
maadli yapi anayoyaongelea???mukama acha kujiabisha,mwanassm yeyote hana haki ya kuongelea maadili maana yeye mwenyewe hajui maadili ila anajua wezi na udhambiki kama mkama,hata watoto wao wanaanza wizi na utapeli wakiwa wadogo ili wakisha kuwa wakubwa wawe wezi kama baba zao.
nani anabisha?????.kama unabisha tuelezee usafi wako kwa kuwa mwanaccm toka ukiwa mdogo,au mtee baba yako.
 
chadema imeingiza magaidi igunga kutoka afghanistan na pakistan-mukama
 
Hapa unaweza ukala bann bure.
Ngoja mi nihame jukwaa hili, Mukama tuheshimiane.
 
Yupo sahihi...wanaoshindwa kuchaguliwa CCM ndio wasafiiiiiiiiiiiiiiii.......wanaoshinda ni undugunaisation na watoa rushwa.


sasa kwann CDM isichukue wanaoshindwa wakati ni wasafi kimaadili?
 
lowassa ameshinda kule Monduli,na yeye amepikwa akapikika?Amemsikiliza Sumaye
alichosema?Huyu mzee kwanza alikuwa awapi siku zote?Mbona kuna uchaguzi wa ccm sikumbuki wapi
watu walitupiana viti?
 
Back
Top Bottom