Nina uhakika Mzee Mangula au Marehemu Kolimba asingesema maneno haya, na hapo ndipo wepesi wa hoja za Mukama unapozidi kushika kasi; Viongozi wa CCM wanaokataa kwamba CCM imechuja kwa kila hali ndio wanaokipeleka chama chetu kaburini; Hata Nyerere miaka michache kabla ya kufariki, alizungumzia CCM kwa lugha kinyume na hii ya Mukama; Pia aliwahi kusema kwamba:
"WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO, NA WASIPOYAPATA CCM, WATAYATAFUTA KUPITIA CHAMA KINGINE".
Tunahitaji viongozi ndani ya CCM, wanaogundua kwamba nguvu ya Chadema ipo na inazidi kukua, na nguvu hii inatokana na CCM kusaliti historia yake yenyewe;