Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,417
Mwanafunzi mmoja nchini Iran, Reza Parastesh, alijikuta akiwa mikononi mwa polisi mwishoni mwa Juma lililopita kwa sababu ya kufanana sana na mchezaji Lionel Messi. Tukio hili lilitokea baada ya msongamano wa watu kutaka kupiga naye picha na hivyo kutishia amani na utulivu hivyo Polisi kulazimika kumhifadhi ndani kwa muda kuepusha dhahama.