Muhongo: Mengi anamiliki ardhi yenye ukubwa sawa na mji wa Moshi mara 80

Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
519
500
Nashukuru hata mimi nimesikia na kuona wakati akieleza.

Tofauti yangu na waziri Prof Molongo ni jinsi anavyomchukulia Reginard Mengi. Licha ya kwamba yeye ni Professor lakini nadhani bado hajaelimika. Msimamo wa Mengi na TPSF si kumwezesha Mengi kama Mengi kumiliki raslimali za nchi. Hoja ya Mengi na TPSF ni kuwawezesha na kuwapendelea wazawa katika umiliki wa raslimali za nchi zao. Mzawa si Mengi peke yake wala yeye hajasema apewe yeye na wengine waachwe. Hilo ndo jambo la waziri kuelewa. Asigeuze mapambano hayo kwa mtu binafsi 'Mengi'.

Mengi anatuzungumzia wazawa wote hata kama yeye akifanyiwa zengwe basi mimi nipate ndo kilio cha Mengi, TPSF na wadau wengine Duniani kote wazawa huwa na credit zaidi kuliko watu wa nje kwenye suala la uwekezaji kwe raslimali za nchi yoyote ile. Kutaja size ya maeneo wanayomiliki bado haiondoi dhana ya wazawa kumiliki raslimali za nchi yao. Serikali inachotakiwa kujua ni kukusanya kodi. Sasa kama mtu anachukua na hafanyii kazi nyie chukueni kodi tu kwa assumption kuwa anazalisha bila kuangalia kuwa ameifadhi eneo bila kutumia. Simple as that.

Mulongo alikuwa SA nilitegemea walau amejifunza kitu jinsi serikali ya SA inavyojali wazawa linapokuja suala la wawekezaji. Waziri angetueleza hayo maeneo aliyoataja kuwa hayatuimiki ipasavyo yamekaliwa tu na anaowaita wazawa je anakusanya kodi. Kama hapana kwanini? Naweza kuchukua fremu kwa mwenye fremu nisiitumie lakini kama nalipa pango lake hutamsikia analalamika. Ila baada ya muda piga fine kwa kukosesha watu ajira. Si kugeneralise kuwa wazawa hawana uwezo au hawatumii fursa wanazopewa. Au wanyang'anywe wape wengine.
 

Mhadzabe

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,887
2,000
Prof. Anajukwaa la kumshambulia Mengi na kweli amefanikisha azma yake. Najiuliza chuki kiasi hicho amefanyiwakitu gani kibaya na Mzee Mengi? Hivi kipi bora mtanzania anayewekeza hapa nchini, na mwekezaji toka nje? Hao wageni sijui wanamuonaje msomi huyu!
 

Fenento

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
320
225
Haya sio maneno yangu bali ni maneno aliyoyatoa Waziri wa nishati na madini muda mfupi uliopita bungeni mjini Dodoma.Hivyo amewataka Watanzania wasilalamike kuwa hawapewi fursa za uwekezaji..

Kama Mengi anamiliki kihalali hakuna tatizo ni mtanzania na ni haki yake. Tatizo ni pale watu wakuja wanapo miliki ardhi yetu kwa njia ya kuhonga na hata kudhurumu.
 

Paul S.S

Verified Member
Aug 27, 2009
6,098
2,000
Jamani tusitake kupotosha na kuukwepa ukweli kwa ghiliba ya mipasho na ngojera
Kilichopo ni hoja kwamba wazawa wamenyimwa umiliki wa maeneo ya gesi na kupewa wageni
Majibu ya Prof Muhongo yamelalia hoja hiyo,sasa ninyi mlitaka ajibu vipi
Shambulia hoja yake kama ya kweli ama ya uongo na si kuiitangonjera kwakuwa imejibu na hakuna hoja
 

Vmark.

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
1,353
0
Vip huyo anayemiliki ardhi yenye ukubwa wa Km za mraba 25589 na mwingine tena km 14238?Cjawashika majina yao but Mengi ni km za mraba 3883.Prof aache ku brainwash wananchi.....Kila siku ni yeye na Mengi tuu then anashindwa ku address mambo ya msingi.Wananchi hatuhitaji hiyo debate yao. To me the Prof is arrogant.Power corrupt and absolute power corrupts absolutely.
 

Mungai Msele

Senior Member
Dec 19, 2013
105
0
Haya sio maneno yangu bali ni maneno aliyoyatoa Waziri wa nishati na madini muda mfupi uliopita bungeni mjini Dodoma.Hivyo amewataka Watanzania wasilalamike kuwa hawapewi fursa za uwekezaji..

Kwa maana hio Mengi awaambie wananchi kwann inchi hii ni Maskini? Serikali ya Ccm haina Mwelekeo hapa ilikofika, Yaan inakosa Sera nzuri za Kuvutia hadi wanaanza kusema mambo ya Mtu binafsi.
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,148
2,000
Mengi anakwamisha umeme wa uhakika?

Mkuu hao ndio wasomi wetu wa kiwango cha juu kabisa,wanapenda kukwepa majukumu na wajibu wao kwa kutoa sababu za kipumbavu kabisa. Yaani kwa sasa hapa Nchini hakuna tofauti kati ya Msomi na asiesoma,huyu PROF UCHWARA anataka kutuaminisha kuwa Mengi kumiliki ardhi yenye eneo lililosawa na Moshi ndio chanzo cha tatizo la Umeme,Mikataba mibovu kwenye Madini na Gesi,Elimu Mbovu,Huduma bomu za Afya na Maisha mabovu kwa kila Mtanzania. Shame on you MUHONGO.
 

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,180
1,195
Kuna watu na viatu kwa kweli. Ninaanza kuamini baadhi ya maprofesa ni makanjanja! Huyu ni profesa wa nn hasa? Mimi nategemea angetueleza anafanya nini tupate umeme wa uhakika! Anafanya nini watanzania wawezeshwe ili wachangie nchi yao kupata maendeleo na zaidi waweze hata kujenga vyanzo vya nishati! Hawa ndo wale wanaoamini hatabwatoto wao hawawezi kusoma na kuandika! Sishangai kwa baadhi ya maprofesa kama huyu kuwasha gari toka UDSM kwenda Ubungo kusaga mahindi debe moja kwa kuogopa tu kuwa kijana wa kazi akienda na baiskeli atakwiba! Badala ya kukaa na kutafiti tufanye hivi ama vile tutapiga hatua! Afanye tafiti gani ili tukwamuke hapa au pale yeye kesharidhika kuwa mimi Profesa bwana! Ama anakiri na anaamini kuwa Mengi anamiliki eneo kubwa hivyo aoni kuwa atakuwa na uwezo angalao naye wa kuwekeza kwenye gesi! Kwani Reginald atawekeza wapi zaidi ya hapa kwake. Believe me non of those you call foreign investors ambaye ana mapenzi mema na hii nchi. Wote wanachuma tu na watatimka baada ya kushiba.
Niwape mfano, kuna mlalahoi mmoja naye anajiita mzungu, akaja hapa baada ya kuona fursa zilizopo akakimbilia kuoa binti wa kitanzania, akamtumia kusajili kampuni na baada ya muda akapata na uraia! Wengi wetu tulijiuliza hii kampuni ina wageni wengi lakini fedha hatuzioni. So hata watu wa TRA walikuwa hawaoni kama kampuni ina generate income. Uchunguzi nilioufanya nikagundua kuwa yeye hulipwa kupitia account yake huko uingereza na yeye hudraw kiwango kinachotosheleza wageni wake na mishahara nyingine hubakia huko huko kwao. Tulipokuja kumconfront alikimbia na sasa karudi kwao. Nilichotaka kusema tu ni kuwa Muhongo anajaribu kuwakumbatia hao anaoamini kuwa wana fedha na kudharau eti sisi watanzania hatuna hela! Kama hana hela aseme yeye hana hela na siomkila mtu hana hela. Huo ni upofu wa fikra! Changamoto ka hizi ndugu zangu Watanzania tusikubali kuamini kuwa sisi ni maskini bali viongozi wetu ndio wenye fikra za kimaskini. Wenye kuamini kuwa kila kitu cha mzungu na mzungu! Wafike mahali sasa wajuenkuwa Watanzania wameamka na wanaweza!
 

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
555
500
Jamani wakuuu naomba aliefuatilia hii hoja anipe details nilipitwa kidogo na bahati mbaya habari nayo nimekuta imepita aahaaaaaaa Jaaaaaaaaaam Jaaaaaama Strabag mtatuuuuua
 

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,898
2,000
Huyo Profesa ni mjinga...kwa sheria ya ardhi hakuna Mtu anayemiliki ardhi Tanzania
...sote tumepangishwa na serikali.

kama Muhongo/muongo anaona kuwa Mengi kakodiswa ardhi kubwa kwaninj wa serikali waliomkodisha wasimnyang'anye hiyo ardhi......kumbe kina maprofesa wajinga !?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom