Muhongo: Mengi anamiliki ardhi yenye ukubwa sawa na mji wa Moshi mara 80

Haya sio maneno yangu bali ni maneno aliyoyatoa Waziri wa nishati na madini muda mfupi uliopita bungeni mjini Dodoma.Hivyo amewataka Watanzania wasilalamike kuwa hawapewi fursa za uwekezaji..

huyu prof nshaanza kuwa na mashaka naye hivi kumbe ukisoma sana nayo shida tu, yeye ameng!ang!ana na mengi, hajaelewa hoja ya mengi nini? huyu naye kumbe niwakurudi darasani tena
 
Wakuu:

Utafutaji wa hizi resources (madini, mafuta na gesi) unahitaji uwezo wa kipesa, pamoja na uwezo wa kitaalamu (financial and technical ability).

Nilivyomuelewa Profesa Muhongo ni kwamba:
1). Serikali imetoa vitalu vingi vya madini kwa wazawa, lakini imegundua kwamba wazawa wengi hawana uwezo wa kitaalamu ya kuendeleza hayo maeneo ..... na ndiyo akatoa hiyo mifano ya akina mengi na wengine, kwamba mpaka sasa vitalu vingi havijaendelezwa (hakuna walichofanya), zaidi ya kusubiri "kuviuza" kwa wawekezaji wa kutoka nje
2). Hakuna mtanzania yeyote mwenye kampuni ya kufanya utafiti na uendelezaji wa mafuta na gesi (oil and gas exploration and production company); hivyo kwamba hata huo "upendeleo" ni vigumu kufanyika. Kwa Tanzania ni TPDC tu ndiyo wana uwezo wa kutafiti mafuta .... hawa wanahitaji kuwezeshwa kifedha tu ili wafanye kazi ya ukweli.
3). Mengi ni mjanja, kwani tayari ameshanunua hisa kwenye kampuni ya Swala Energy http://www.swala-energy.com/documents/ASXAnnouncementEquityplacement13November2013.pdf .... hiyo kampuni ina uwezo wa kununua vitalu bvya gesi na mafuta.
4). Wazawa wenye interest kwenye mafuta na gesi, wanaweza jikusanya, anzisha kampuni, nunua vifaa na ajiri wataalamu .... halafu hapo wakiomba kupendelewa, nadhani itawezekana.
 
Hawa wasomi wetu wanashangaza hoja wanazotetea..nimemsikia mmoja akijinadi ana Phd wakati hata kutamka neno "google" hawezi anatamka "gogo"
msomivwa Phd huyo wa Mzumbe..unakuta tayari alikuwa anaitwa Dr kabla hata hajahitimu
 
Haya sio maneno yangu bali ni maneno aliyoyatoa Waziri wa nishati na madini muda mfupi uliopita bungeni mjini Dodoma.Hivyo amewataka Watanzania wasilalamike kuwa hawapewi fursa za uwekezaji..

Maprofessor wa Tanzania wanaishia kubaka vitoto vya shule na kuvuambukiza magonjwa hatari. Sijui kapuku STD 7 atafanyaje. Muhongo aliingia bungeni kwa mbwembwe akijifanya anapambana na wabaridhifu ndani ya Tanesco na kutaja vipuri vya gharama vilivyoagizwa kutoka nje ya nchi kumbe ilikua ni misumari, kisha akatuambia jinsi nguzo za umeme zilivyokua zinatoka humu nchini na kupelekwa Mombasa Kenya kisha kurudishwa wakisema zimetoka South Africa. Wabunge wenzake wa CCM wakamwambia wenzako haweendi hvy wewe umepewa lifti usianze kuchezea honi utashushwa, akaufyata. Sasa story imebaki ni yeye na kupambana na Mengi. Siku ile ya mdahalo alikuwa anajigamba kuwa yeye ni msomi ni mtu wa "DATA AND FACT". kumbe data zenyewe za kuchonga. Msomi ukishatoa Data hurudii tena kitu kilekile kuwaambia wananchi, njoo na hoja nyingine ili watu wajue kwamba kweli wewe ni mtu wa data na sio data tu na vitendo pia. Mambo ya kuambiana ifikapo mwaka 2025 nchi hii itakuwa inameremeta kana kwamba itakuwa Disco Ligth hatutaki. Atuambie yale yaliokuwa yameandaliwa miaka 10 iliyopita sasa hv yamefikia wapi? Sio bla bla zake dhidi ya Mengi. Huyu anajambo na Mengi. Si ajabu kinamuuma jinsi mwenzake anavyokubalika kwenye jamii na yeye na Elimu yake hata akipanda daladala watamfananisha na Matonya. Ndio maana anapambana kumchafua mwenzake kwenye midani za kijamii. Lakini sio Muhongo tu aliyejaribu kapambana na Mengi na akashindwe wengine ni pamoja Sophia Simba, Lawrance Masha, Basil Mramba, Masilingi na hawa wote walikuwa mawaziri wakati wakipambana nae. Badala ya kupambana na wageni wanaenda kupambana na mzawa mwenzao. So stupid kabisa. Shame on them!!!!!!
 
Vip huyo anayemiliki ardhi yenye ukubwa wa Km za mraba 25589 na mwingine tena km 14238?Cjawashika majina yao but Mengi ni km za mraba 3883.Prof aache ku brainwash wananchi.....Kila siku ni yeye na Mengi tuu then anashindwa ku address mambo ya msingi.Wananchi hatuhitaji hiyo debate yao. To me the Prof is arrogant.Power corrupt and absolute power corrupts absolutely.

Mkuu Vmark, ni kweli kabisa! Madaraka ni aina ya ulevi fulani hivi ambao hupelekea mwenye nayo kuwa arrogant. Wanasahau kuwa cheo ni dhamana na chenye mwanzo kina mwisho.

Unakumbuka suala la uwekezaji wa iliyokuwa Kilimanjaro Hotel mwaka 1998, ule ubabe wa aliyekuwa waziri ofisi ya raisi Utawala Bora (Wilson Masilingi) dhidi ya huyu huyu Reginald Mengi? Baada ya awamu ya tatu huyu W. Masilingi alipokosa hata nafasi ya ukuu wa wilaya alikuwa mpole hadi kutia huruma. Amshukuru JK mwaka huu kumteua kuwa balozi ughaibuni, alikuwa keshapigika kinoma!

Sasa huyu profesa aache arrogance inayomfanya kuwa mbabe bila sababu. Uwaziri wa kuajiriwa ni wa kitambo kifupi!
 
Mzee Madiba nenda kamwambie Mwl. Nyerere kuwa, MaCCM, yamekuwa ni Chama Cha Mizigo-CCM Tanzania
 
MENGI KAMA USIPO MCHUKULIA HATUA PROFFESOR HUYU SITA KUAMINI. LEO AMEAMIA MOSHI YA DAR ES SALAAM TATU ASHA BAINI NI UWONGO Muhongo Ni Muongo Mkuu Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Nashukuru hata mimi nimesikia na kuona wakati akieleza.

Tofauti yangu na waziri Prof Molongo ni jinsi anavyomchukulia Reginard Mengi. Licha ya kwamba yeye ni Professor lakini nadhani bado hajaelimika. Msimamo wa Mengi na TPSF si kumwezesha Mengi kama Mengi kumiliki raslimali za nchi. Hoja ya Mengi na TPSF ni kuwawezesha na kuwapendelea wazawa katika umiliki wa raslimali za nchi zao. Mzawa si Mengi peke yake wala yeye hajasema apewe yeye na wengine waachwe. Hilo ndo jambo la waziri kuelewa. Asigeuze mapambano hayo kwa mtu binafsi 'Mengi'.

Mengi anatuzungumzia wazawa wote hata kama yeye akifanyiwa zengwe basi mimi nipate ndo kilio cha Mengi, TPSF na wadau wengine Duniani kote wazawa huwa na credit zaidi kuliko watu wa nje kwenye suala la uwekezaji kwe raslimali za nchi yoyote ile. Kutaja size ya maeneo wanayomiliki bado haiondoi dhana ya wazawa kumiliki raslimali za nchi yao. Serikali inachotakiwa kujua ni kukusanya kodi. Sasa kama mtu anachukua na hafanyii kazi nyie chukueni kodi tu kwa assumption kuwa anazalisha bila kuangalia kuwa ameifadhi eneo bila kutumia. Simple as that.

Mulongo alikuwa SA nilitegemea walau amejifunza kitu jinsi serikali ya SA inavyojali wazawa linapokuja suala la wawekezaji. Waziri angetueleza hayo maeneo aliyoataja kuwa hayatuimiki ipasavyo yamekaliwa tu na anaowaita wazawa je anakusanya kodi. Kama hapana kwanini? Naweza kuchukua fremu kwa mwenye fremu nisiitumie lakini kama nalipa pango lake hutamsikia analalamika. Ila baada ya muda piga fine kwa kukosesha watu ajira. Si kugeneralise kuwa wazawa hawana uwezo au hawatumii fursa wanazopewa. Au wanyang'anywe wape wengine.

heshma kwako mkuu
 
Kijana masikini toka Serengeti amesoma sasa anadharau kila mtu. Ila tusimlaumu hata bosi wake hana elimu yake kwahiyo anajua tu kuwa is business as usual, anajua hawezi kufanywa chochote but the end will justfy the means
 
watu kama muhongo ktk nchi ya china wananyongwa siye tunawachekea na hasa wafuasi wa chama anachokiwakilisha
Watu wanathamini wazawa ktk uwekezaji yeye anawaza uwekezaji wa nje yaliyotokea kisesa ndiyo matunda ya viongozi kama muhongo.Pia watanzania tunatakiwa kushituka kwanini watetezi wa wanyonge wanachukiwa kama siyo kununuliwa refer Zito ktk serikali hii kwa namna hii watanzania kwa nafasi zetu tutumie fursa tunazopata kuwaadhibu.
 
Hawa wasomi wetu wanashangaza hoja wanazotetea..nimemsikia mmoja akijinadi ana Phd wakati hata kutamka neno "google" hawezi anatamka "gogo"
msomivwa Phd huyo wa Mzumbe..unakuta tayari alikuwa anaitwa Dr kabla hata hajahitimu

kwa hyo we unaona akitamka unavyotaka wewe ndio msomi?,hayo ni matamshi tu kaka na ndio maana accent ya kiswahili cha Dar haiwezi kuwa sawa na ya Moshi,usomi upo pale pale,accent inaathiriwa na mazingira aliyokulia mtamkaji mkuu
 
Hawa wasomi wetu wanashangaza hoja wanazotetea..nimemsikia mmoja akijinadi ana Phd wakati hata kutamka neno "google" hawezi anatamka "gogo"
msomivwa Phd huyo wa Mzumbe..unakuta tayari alikuwa anaitwa Dr kabla hata hajahitimu
Kutamka vizuri maneno ya Kingereza si kipimo cha Usomi kwani Wasomi wa Kihindi na Mainjinia wa Italy matamshi Yao ni Full utata tena wanatamka Vibaya kuliko wasomi weusi .kumbuka Taaluma(Elimu) hutolewa ktk Lugha mbali mbali Dunia wapo wasomi wa Kichina,kijerumani kifaransa kirusi kirumi kispain nk wana PHD wamezipata kwa masomo ya Lugha zao na Hawajui Kingereza kwani kwao si muhimu sana Kama kwa watu weusi ambao wamejawa na kasumba Kuwa kuzungumza Kingereza ni Usomi ! Je?yule Mzungu mzaliwa wa Uingereza ambaye hajaenda shule lakini anamwaga English balaa ni Msomi ?
 
Hili suala la Mengi na Waziri inaelekea litachukua kipindi kirefu kupata mshindi na Sidhani Kama Lina uhusiano na taaluma zao Binafsi cha Msingi ni watu kuacha ushabiki kwani hatima ya sakata lenyewe haeleweki !
 
Kwa hiyo Watanzania milioni 46 hawataruhusiwa kuwania vitalu kwenye sekta ya gesi kwa sababu kuna Mtanzania mmoja- anayeitwa Mengi- anamiliki ardhi yenye ukubwa sawa na mji wa Moshi wa mara 80?


Hata hoja ya kwamba Watanzania wakipewa vitalu watauza bado haina mashiko. Ni wawekezaji wangapi wamekuja Tanzania na baada ya kupata fursa ya kuwekeza wanauza na kujipitia fedha? Hata kwenye migodi mfano wa North Mara huko nyuma hakukuwa chini ya Barrick. Mbona serikali haisemi kuwa wageni hawatapewa kwa sababu watauza? Hivi hayo makampuni ya nje wanakuja na hela kwenye magunia?

Na kama Watanzania hawana uwezo, akiwa kama waziri mwenye dhamana ya hii sekta anaona dawa ni kuwapa watu wa nje? Vitalu vimetolewa hata kabla ya sera ya gesi haijawa tayari! Haraka ya nini kama sisi watanzania hatujawa tayari?
 
Kijana masikini toka Serengeti amesoma sasa anadharau kila mtu. Ila tusimlaumu hata bosi wake hana elimu yake kwahiyo anajua tu kuwa is business as usual, anajua hawezi kufanywa chochote but the end will justfy the means

Sidhani Kama malumbano ya Mengi na waziri yana uhusiano na Taaluma zao Binafsi kwani hata mengi nae ni DR siku hizi nae anahesabika Kama msomi . Tatizo lililopo ni masilahi na watu hawajui kiundani kuna nini ! Wamekurupuka kushabikia kila mmoja anamshabikia mtu wake ambaye anaona Kama anaonewa ni vyema watu tungesubili tuone mwisho wa hii sinema ndipo watu watoe hukumu zao
 
Mpambano kati ya Mtumishi wa Serikari na Mfanyabiashara mkubwa Tz unatarajia nini hapo ? Ebu tabiri mshindi ?
 
Prof muhongo pamoja na shahada zake bado ni kilaza kifikra na kimaono. Elimu yake badala ya kumkomboa kifikra ndio kwanza imempofua... Baba na mababu zetu walipigania na kupata Ukombozi wa kisiasa...wananchi wenye upeo na uzalendo hivi sasa wanapigania ukombozi wa kiuchumi.

Kama tungependa kuzingatia fikra za prof muhongo za kitumwa na za kudharau wananchi wazawa na kukumbatia wageni, angesema kabisa kuwa hakuna mzawa mwenye uwezo wa kuongoza nchi...tutafute viongozi wa nje watutawale kwa mtindo wa uwekezaji hadi tutakapojiweza...shame.

Nawe faizafox umedata km prof wako . Mdahalo niliufuatilia na mengi akuwahi kuda i apewe yeye binafsi umiliki wa 35% ya kitalu kilichofanyiwa exploration... Alcohol is is it is a no kuwa katika uwekezaji serikali izichukulie raslimali za nchi kuwa no MTAJI wake wakati wa kuingia ubia, badala ya kuimba ngojeraa kuwa nchi na wananchi wake in makapuku wa mitaji na teknolojia, kwa hiyo hatujiwezi.

Na kwa upumbavu wako unaona ni saw a kwa prof wako kutoa siku moja kwa mzawa kutimiza masharti ya kununua kitalu TPDC wakati wawekezaji wa nje wamepewa hadi May mwakani?
Mungu ibariki Tanzania kwa kutupunguzia watu wenye husda, wachumia matumbo yao na wenye macho yanayoona hadi vinapoishia vitovu vyao tu.

Nawe ni punguani mwingine? nisome vizuri, Mengi amesema hizo 35% apewe yeye akatafute wawekezaji. Kasahau kuwa kaambiwa Tanzania inabaki na 65% na zinafunguliwa Kampuni na zitakuwa kwenye soko la hisa na kila awezae akanunuwe hisa.

Sasa wewe sema hizo 35% kama Mengi hakutaka yeye agawane na wawekezaji alitaka nini?
 
huyu prof nshaanza kuwa na mashaka naye hivi kumbe ukisoma sana nayo shida tu, yeye ameng!ang!ana na mengi, hajaelewa hoja ya mengi nini? huyu naye kumbe niwakurudi darasani tena

Kinachomfanya Muhugo asieleweke ni kwa sababu yeye ni Proffesor. Hivi inakuaje watu wanataka Proffesor afikirie kama mtu wa kawaida sasa nini tofauti kati ya proffesor na asiekua proffesor.

Raisi alieleza kwa ufasaha gharama zinazohitajika kabla ya kuingiza faida ya biashara wengi wakaridhika kuwa kwa wabongo hawako tayari kufanya risk ya namna hiyo, sasa kinachofahamika nikuwa Muhugo atatumia foreign investors na mengi naye atatumia foreign investors sasa nini tofauti.

Wabongo wengi hatuna utaratibu wakufikiria mambo kwa kina, hebu tuchukue time kidogo tutafute nini hasa tatizo la msingi lakin tusitegemee proffesor awe na mawazo kama yetu. Hapo ndio kosa letu lilipo. Muhugo na Mengi wanazungumza kitu kimoja lakin kwakua wote niwasomi kinachogomba ni maslahi. Itafurahisha zaidi kama wanatetea maslahi ya waTanzania na itasikitisha sana kama wanatetea maslahi binafsi!
 
Back
Top Bottom