Muhongo kamzidi 'ujanja' Magufuli?

Prof na Dk ipi elimu kubwa?
 
Hive wale walk look alia kuwa hela za Escrow siyo za umma je wana ujasiri wa kusema tena hivyo bila kupepesa macho. Profesa mkweli unalisemeaje hili? Kama siyo za umma mbona Tanesco imeamriwa izilipe tena kwa mhusika!
 

yaani anaweza kufumaniwa na mke wake bado akachomoka!
 
The Boss hatari kwa synthesis na analysis! Pongezi kwako!
 
Voda mpaka costumer care wanawapa airtime utapoteza muda kumuelewesha
 
CCM inawabunge kibao wenye uwezo wa kushika hiyo nafasi ya Prof. Muhongoa sema tu rais hajaamua. E.g. Mtu kama Dr. Dalali Kafumu aliyekuwa kamishina wa madini atashindwaje kuwa waziri? Kilichowazi hapa Muhongo na Magufuli lao moja.
 
Ni mtupu huyu jamaa....
naona analeta habari za vijiweni humu
hoja hana....analeta mihemko tu
eti sio wafanyakazi wote.....vodacom
sasa kama hata ni wachache si kitu hiko hiko?
Mkuu achana nae huyo mbona hiyo ipo kwenye mashirika kalibu yote? Hapa kwetu wafanyakazi wote tunapewa ila inatofautiana viwango kutokana na nafasi ya kila mwajiriwa.
 
Wengi waliotumbuliwa walikuwa wanamuunga mkono Lowassa. Hawa akina Muhongo wao ccm damu ndio maana huoni kutubuliwa. Ccm wabaguzi kushinda makaburu


Ndukiiiii[emoji125] [emoji125] [emoji125]
Lowassa huyu fisadi au kuna mwingine
 
Usipowajua Wanasiasa wa nchi hii...ukawa unajua mambo yao ya Magazeti na wanayoongea kwenye TV basi wanakupoteza...ukiwafahamu wanayofanya na maamuzi yao kama huna roho ngumu unaanguka na kuzimia hapo hapo...wanavigeugeu balaa na wanafanya watu wengine kama hawana akili vile...
 
Kwa professa muhongo unapoteza muda bure yule mtu yuko smart na anaifahamu kazi na ndiyo maana hata magufuli hana sababu ya kumgusa, ww andika tu sana kwa sababu una muda na unalipwa kufanya hivyo
 
Wadau, naona kuna wachangiaji wanaleta hoja kuwa TANESCO wanagawa unit 700 bila kuinyambua hoja vizuri. Nisaidieni kujibu haya maswali mawili:
  1. Staff gani au wangapi wanapewa units 700?
  2. Kila baada ya muda gani?
Kwa bei za sasa za umeme, units 700 gharama yake ni shs laki mbili na ushehe (kwa maana ya 292 TShs per unit, kwa wateja wa T1). Je, mnadhani ni bora TANESCO izijumuishe hizi pesa kwenye mishahara ya wanufaika au ni bora kuendelea kuzigawa kama inavyosemekana?
 
Herufi ya H inaleta utata kwenye jina lke ila ukiminus H unapata taswira nzima ya maisha yake.

Na mara nyingi watu wa aina hii wanakua na uwezo wa kujenga hoja na ukaamini kua ni kweli anachoongea na ndio maana utaona kama ana roho ya paka tena paka shume.
 
Mkuu, The Boss hapa itabidi uwe mpole tu. Bila shaka umeshawasikia "watanzania" halisi - wapiga kura - kuhusu Mhongo, TANESCO, EWURA na ESCROW. Hapo ndipo utafahamu kwa nini bado haiwezekani kuwa na uongozi wa maana nchini. Akina Mhongo na bosi wake wako katika mashamsham kama ya yule mkuu sana wa kule duniani aliyedai majuzi kuwa: “I could stand in the middle of Fifth Avenue and shoot somebody and I wouldn’t lose any voters,”!

Leo hii huwezi kuwashawishi "wapiga kura" kwa hoja yeyote ile. TANESCO ilivyovurugwa na inavyoendelea kuvurugwa na wakubwa wa nchi ni suala lililowekwa wazi siku zote. Hata shahidi "tumbili" yupo; atakuthibitishia. LAKINI hizo hoja ngumu na fikirishi za nini? Waachie CHADEMA hizo. Sisi tunatakiwa tu kushuka hadi kile kiwango maarufu cha kuimba mapambio ya kuwapongeza watakatifu wetu wanaotujali "sisi wanyonge" kwa kuzuia ongezeko la bei na kumfurusha CEO "mwenye roho mbaya sana" na watanzania! Basi!
 

"Nine lives of a cat"
 

Voda wafanyakazi wote wanapewa voucher Including Customer care Staff. Ni fact hyo. Haya urudi kwa hoja ya msingi.
 

Kwann uhangaike kumweleweaha mtu asiyetaka kukuelewa. Mwacha afe na umbumbu wake.
 
Tatizo kubwa ninaloliona kwenye serikali ya Magufuli ni kuwaogopa wanasiasa wenzie wa Ccm....

Na hicho ndicho kitamkwamisha........
Sio kuwaogopa wanasiasa anawaogopa walimu wake yaani maprofesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…