Muhongo kamzidi 'ujanja' Magufuli?

Wewe kumbe mtupu hivi?
hoja yako ya hasara nimeijibu kwa kukutajia mashirika ya ndege
yanajiendesha kwa hasara lakini staffs wanapata free tickets kama kawaida

Vodacom wafanyakazi wote walioajiriwa wanapewa airtme na bundles za kutosha kwa matumizi yao
nna ndugu wako vodacom nafasi za chini..wanapewa bundle na airtime
hadi wanagaia ndugu wengine.....same na Tigo na kampuni tele
Mwanaume hupaswi kupenda vya bure mshahara si unapata
 
Managemeny ya Tanesco haijawahi kuwa independent
kila wanachoamua kinapata go ahead kutoka wizarani
sasa utailaumu vipi management halafu uisifie wizara?
we unaonekana mtupu kabisa unaongea mifano puumba kabisa

Na doubt uwezo wako hata wa hesabu sababu mifano yako mingi ni kichekesho
unazungumzia wafanyakazi kupewa unit 700
hivi unajua umeme wote wanaopewa wafanyakazi ni asili 0.02 ya umeme wanao uza?
sasa utasemaje shirika linapata hasara kwa wafanyakazi kutumia asilimia 0.02 ya sales?
na Vodacom nayo inapata hasara kwa wafanyakazi kupewa airtimer?
Daily News wanapata hasara kwa wafanyakazi kupewa magazeti bure?


hebu acha kujiumbua mkuu
Mkuu bila shaka na wewe ni muhanga wa ubatlisho uliofanywa na Rais..kichwa chako kinaweza kuwa ubinfsi zaidi kuliko akili.

Tanesco imetiwa hasara na manegiment wala si wanasiasa hizo unit unazosema ni danganya toto , watumishi wa tanesco wanatumia umeme bila kikomo pia wanajipa bonus kibao.

Naunga mkono kutumbuliwa kwa huyo jamaa.

Shirika ni la umma watu wapewe mishaha wajigawie bonus bado umeme watumie bure tukae kimya tu, hapana mkuu hii nchi ni yetu sote hakuna mwenye haki zaid acha awajibishwe ndo ataelewa hii si awamu ya NNE.
 
vodacom haitoi vocha kwa staff wake wote..

wanaopewa vocha vodacom ni wale wa position ambazo hata wangekuwa tanesco wangepewa vocha.. hiii ni fact no 1.

pili tanesco inajiendesha kwa hasara... naomba
unitajie shirika au kampuni yeyote inayotoa huduma bure kwa staff wake kipindi ambapo inapata hasara..

nataka tujenge hoja kwa facts..


je voda inatoa vocha kwa staffs wake wote kisa ni wafanyakazi wa voda au wanapewa vocha wale tu wenye majukumu yanayohitaji kuwekewa vocha???
naomba ulijibu hili swali usikimbie wala kupiga chenga chenga

uje na facts voda nani anapewa vocha nami nije na facts za tanesco..
Mkuu huyo ni muhanga wa mabadiriko haya anachokitetea wala hakijui wala usipoteze muda wako kubishana nae, binafsi watu kama hawa huwa nawadharau sana anatokwa na povu kujihalalishia mali ya umma.
 
Ni mtupu huyu jamaa....
naona analeta habari za vijiweni humu
hoja hana....analeta mihemko tu
eti sio wafanyakazi wote.....vodacom
sasa kama hata ni wachache si kitu hiko hiko?
Ila wewe si mtupu umejaa ubinafsi na hila za kuchukia watu kwasababu wamegusa masrahi yako. Pole ila kumbuka hii ni awamu ya tano
 
prof mhonga ni jembee.. hata mimi nikiambiwa niwape ranking mawaziri no 1 ni muhongo...

huyu baba anajua vitu ile deeep.. shule yake sio ya janja janja

tanesco management ina wajanja wajanja wengi sana...

japo mramba simjui performance yake.. ila Tanesco haijawai perform miaka yote.. so najua hajaonewa tu.. ni wale wale

hata ingekuwa mimi rais shirika la kuanza nalo lilikuwa tanesco... ningetimua hadi mfagiaji.. hakuna ambaye angebaki..

mtu wateja wote wako.. huna mshindani na bado unapata hasara.. kina voda na tigo wanagombea wateja ila wanapata faida... tanesco inalelewa sana
Pole sana.
 
LOVE HIM OR LOATHE HIM-muhongo is genius, sio hao "vihiyo" unaowapenda wewe.
 
Wewe kumbe ni mtupu kabisa
kama vodacom na Tigo ni baadhi ya wafanyakazi na sio wote
bado inatetea hoja yangu kuwa 'staff rates' inatumika
na hoja ni kuwa staff rates sio invention ya TANESCO
ipo dunia nzima....

Kama wewe akili yako inakufanya uamini staff rates inatakiwa kwa the few
na sio wote hiyo ni opinion yako tu..wengine wanaweza kupinga pia
na wakaona ni bora kwa wafanyakazi wote...
bottom line staff rates iko dunia nzima
Unajua mkuu unanifanya niondoe Imani yangu kwako? Unamjibuje mtu ambaye tangu mwanzo keshakuonyesha hajui chochote? Watu kama hawa una achana nao waendelee kukariri sijui nilifanya pwc sijui najua!!!
 
sio kweli hili naomba uthibitishe.. kuna mtu namjua ameajiriwa tigo na hapewi vocha kisa position yake haimruhusu kupewa vocha... na nimeshamwita anakuja.. naomba uweke facts zako kuhusu hili
Acha ubishi wanapewa muda wa maongezi na GB za kutosha za net,ninao ndugu na marafiki wanafanya kazi tigo
 
Wanaokumbuka hadithi za utotoni...wanakumbuka hadithi ya kuwa paka ana roho saba
na kwa kuwa ana roho saba basi ukijaribu kumuua unashangaa anaibuka tena akiwa hai..

Unaweza mlinganisha Waziri Muhongo na hadithi za paka wenye roho saba...

Kila ikitokea scandal ya kutosha kumtimua Waziri Muhongo..'upepo' unabadilika
'anabaki ana dunda tu'


Kwanza kuna scandal maarufu ya Escrow...licha ya kuwa imerudi tena
na tunatakiwa kulipa tena mabilioni..Waziri Muhongo utasema sio yeye
alieishupalia huko nyuma kuwa yale mabilioni ni halali kuyalipa

Scandal ya Flow meter bandarini....baada ya waziri mkuu kuvamia bandarini
akatajiwa ni waziri gani alihusika na suala zima la scandal hiyo ya flow meter..
'upepo' ukapita....Waziri Muhongo ana dunda...

Likaja la Dangote ...na uzushi kuwa anataka gesi bure....na kauli za kushangaza
na kitendo cha Waziri Muhongo kuwa bega kwa bega na washindani wa Dangote
na kutokea sintofahamu za kila aina..hadi Dangote alipoenda Ikulu
ndo 'yakaisha'...still Muhongo ..;ana dunda tu'

Ndo likaja hili la 'kupandisha bei ya umeme'...ambalo ushahidi uko wazi wizara
ilikuwa inajua 'mchakato wote toka february 2016...hadi juzi...
na hata sababu za Tanesco kupandisha bei....ikiwemo ya Tanesco
kuingiliwa maamuzi na kulazimishwa kupunguza bei na kuondoa 'service charge'
maamuzi ya kisiasa ambayo source ni waziri Muhongo....

Sasa badala ya Magufuli kumtimua waziri Muhongo kwa kusababisha hiyo mess
Magufuli anakuja kumtimua Mramba ambae maamuzi mengi kama sio yote
yalianzia kwa 'orders' za waziri Muhongo.......

Muhongo huyu huyu ambae kila mara anaongea kwa uwazi kabisa kuwa
Tanesco iache kuzalisha....iwe inanuanua umeme kwa asilimia 100
wakati anajua kuwa Tanesco inanunua kwa bei ya juu kuliko inavyouza
kwa umeme huo ambao inanunua ambao bado ni aslimia chini ya 50
sasa je iwapo itanunua kwa asilimia 100...watapataje faida?
kama asilimia chini ya 50 tu wanategemea ruzuku serikalini?

Huyo ndo Muhongo.....ije mvua lije jua....Magufuli anamuamini na kumsikiliza
na hata kumpongeza kwa maamuzi yake yanayoleta 'utata' kila sehemu
kuanzia kwenye gesi,umeme,vitalu vya gesi,madini na kila anachokigusa..

Kweli hadithi za utotoni za paka kuwa na roho saba...hazikuwa burudani tu ya kufurahisha
genge......
mkuu labda kwa kuwa wote wafupi.
 
Nimesikia u-genius wa professor wetu Mhongo... Sasa si aelezewe alivyo genius kama wengine walivyomuelezea alivyo kilaza. Badala ya kuwa haters na Fans, toeni basi hata kifupi kwanini professor ni genius.
 
Back
Top Bottom