Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,578
- 19,463
Nimeona nikumbushie kidogo kutoka katika Historia kuwa Tarehe 16 March 1938, Hitler alivamia eneo la Czechoslovakia la Sudetenland kwa madai kuwa eneo hilo lilikuwa na wajerumani wengi ambao walikuwa wakionewa na utawala wa Czechoslovakia.
Wakati huo Hitler alikuwa na jeshi kubwa sana kiasi kuwa Czechoslovakia haikufurukuta kujitetetea. Kwa miezi sita Ujerumani ikawa imejimilikisha eneo hilo kwa mabavu huku ikiliita Protektorat Böhmen und Mähren (Protectorate of Bohemia and Moravia). Mwishowe serikali ya Czechoslovakia ikaona isiwe taabu wakakubali kuliachia eneo hilo chini ya makubaliano yaliyofanyika Munich tarehe 17 September 1938 yakijulikana kama Munich agreement kuwa Ujerumani haitajimegea eneo jingine la Czechoslovakia wala la nchi yoyote jirani.
Hata hivyo, baada ya Makubaliano hayo, yaani ndani ya wiki moja tu September 21, Ujerumani ikaivamaia Poland huku ikidai kuwa kuna sehemu fulani ya Poland nayo ilikuwa na wajerumani wengi lazima irudishwe chini ya utawala wa kijerumani. Kabla uvamizi huo wa Poland haujatulia , kesho yake Sepmbeter 22 wakavamia pia eneo la Hungary kwa madai hayo hayo. Uvamizi huo ndio uliochockea kuanza kwa vita ya dunia mwezi huo huo Sepember 1939.
Uvamizi uliofanywa na Ujerumani pia uliifanya Japan nayo ifanye hivyo hivyo kwa majirani zake China na Korea. Kwa hivyo vita iliyoanza Ulaya kutokana na dikiteta mmoja kuvamia ardhi za majirani zake ikajikuta imesambaa dunia nzima haraka sana na kuwa vita ya dunia.
Wanahistoria wamekuwa wanaona uvamizi wa Urusi huko Crimea, kwa madai kuwa ni sehemu ya Urusi, na baadaye huko Donetski kuwa kuna warusi wengi na amewahi pia kuvamia sehemu ya Moldova (transnistria) pamoja na maeneo mengine ya Georgia huko Abkhazia na South Ossetia, kwa madai hayo hayo ni kama yale ya Hitler wakati huo. Ushabihiani huo wa malengo ya Putini na ya Hitler ndiko kunakosababisha wapenda amani waisaide sana Ukraine kijeshi ishinde vita hivyo ili kuzuia Putin asije akaisambaza duniani kote.
Sasa hivi amekuwa anaweka pressure kwa Belarus nayo kuingia vitani kumsaida. Kujiunga kwa Irani kwenye vita hiyo kunaweza kuanza kuchochea Saudi Arabia na Israel kuwa upande wa Ukraine kijeshi kutokana na uhasama wao na Iran na mwisho vita ikasambaa out of control.