Muhimu kuiona hii kwa wanaume/wanawake tu!!!

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
Jamani samahanini wanajf hivi huwa najiuliza kama mwanaume kuwa ugonjwa wa kisukari ukikupata mwanaume mambo huwa hayaendi (jogoo inawezekana akawa hapandi mtungi) na kufanya sex kiujumla inakuwa ni ishu kwa sababu jogoo kuwika ni9 ishu hasa ukizingatia kuwa jogoo mpaka awike inabidi msukumo wa damu uwe mkubwa kuelekea kwenye sex organs au mpaka upigwe insulin injection.

Kiujumla heshima ya ndoa inakuwa haipo nyumbani kisa baba hatekelezi majukumu yake ya tendo la ndoa.

Sasa nauliza hivi ugonjwa wa kisukari ukiwakuta kinamama na wenyewe mambo yanakuwa hivyo hivyo tu au ni kwa wanaume?
 
Ulibwino, mkalamba? peleka jf doctor mkuu watakujibu..:juggle:
 
walioenda kwa babu na kunywa juice wanafurahi jinsi ndoa zilivyoimalika.......nenda kwa babu....
 
Kwa wanawake sielewi lakini naweza kuongelea kuhusu wanaume wenye kisukari,mimi nimekuwa na kisukari kwa miaka 13 kama ukifata masharti hiyo athari haitakwepo.Unatakiwa kufata masharti ya kula matunda na mbogamboga kwa wingi,kunywa maji mengi,acha kutumia soda na pombe zenye sukari(bia 2-3 kama Serengeti au pombe kali mara 1-2 kwa wiki haina madhara)kupunguza sio kuacha vyakula vya wanga,vyakula vya protini kama mayai,nyama,maharage na maziwa ule mara kwa mara,ufanye mazoezi,ulale mapema na mwisho umeze dawa kwa wakati baada ya kula sio kabla.
Kama una uwezo nunua mashine ya kupima glucose na kujipima kwa uchache mara 2 kwa wiki ukiamka na masaa 2 baada ya mlo,mashine hizi ni elfu 45 tu.
 
ukizingatia kuwa jogoo mpaka awike inabidi msukumo wa damu uwe mkubwa kuelekea kwenye sex organs.

Jibu umeshajipa mwenyewe hapo...ni kweli ili jogoo liwike, lazima mwanaume apate ashki, halafu anamwaga hormones ambazo zinaongeza msukumo wa damu kwenda kwa jogoo, na hapo ndipo atawika. Kwa wagonjwa wa kisukari hili linakuwa linapunguzwa ufanisi na hivyo kuwika kunakuwa na mushkeli kidogo (NB: Sio wagonjwa wa sukari wote).

Kwa wanawake mechanism ni tofauti, haitaji msukumo wa damu na hivyo...hata akiwa na kisukari bado anaenjoy mchezo kama kawaida!
 
Jamani Mzambia umeniacha hoi na kichwa
cha hii thread ...
Kwa wanaume/wanawake tu
Kwani kuna nani tena dear?
 
Kwa wanawake sielewi lakini naweza kuongelea kuhusu wanaume wenye kisukari,mimi nimekuwa na kisukari kwa miaka 13 kama ukifata masharti hiyo athari haitakwepo.Unatakiwa kufata masharti ya kula matunda na mbogamboga kwa wingi,kunywa maji mengi,acha kutumia soda na pombe zenye sukari(bia 2-3 kama Serengeti au pombe kali mara 1-2 kwa wiki haina madhara)kupunguza sio kuacha vyakula vya wanga,vyakula vya protini kama mayai,nyama,maharage na maziwa ule mara kwa mara,ufanye mazoezi,ulale mapema na mwisho umeze dawa kwa wakati baada ya kula sio kabla.
Kama una uwezo nunua mashine ya kupima glucose na kujipima kwa uchache mara 2 kwa wiki ukiamka na masaa 2 baada ya mlo,mashine hizi ni elfu 45 tu.

Good sound advice mkuu!!
Na kwa wale ambao hawakuweza ku-manage diabetes mpaka kufikia kwamba hili tatizo limekua chronic basi dawa kama Viagra na nyengine ndio zinasaidia, lakini bado inabidi wamwone daktari, kufanyiwa vipimo vingine then kuandikiwa dawa hii!!
 
Kitu cha kwanza ukishajuwa una diabetes ni kuikubali hali hii na kufata masharti ambayo watu wengi hawayafati na baadae kupata matatizo ya macho,figo,ukosefu wa nguvu za kiume na kadhalika.Mimi baada ya kujihisi kuchoka kila mara,kukojoa sana na kusikia kiu kila wakati 1998 nilipimwa na kugundulika na diabetes,nilikutana na babu wa miaka 78 ambaye aliishi na kisukari kwa miaka 42 na huwezi amini ana afya nzuri.Ushauri wake ndio nimeuandika hapa juu,umenisaidia sana na tusisahau kumshukuru MUNGU.
 
Kuzingatia masharti ni muhimu ila sababu Babu yupo ni kuwahi mapema na utaratibu umeboreshwa kwa hiyo itakuwa rahisi kupata huduma na heshima itarudi,wanawake uvumilivu unatakiwa manpokuwa katika kipindi hiki ambacho kupatikana kwa tiba kumeifanya kuwa ya mpito
 
Jamani Mzambia umeniacha hoi na kichwa
cha hii thread ...
Kwa wanaume/wanawake tu
Kwani kuna nani tena dear?

Nilikuwa sijawahi kukuona Mrembo una hasira, leo ndio nimejionea
Mpaka nimeogopa kuku-quote pamoja na mabuti yangu . . lol:lol:
 
tusipoteze muda kutafuta dada au ushauri, we kama unakisukari wahi loliondo fasta na ie historia
 
Kwa wanawake sielewi lakini naweza kuongelea kuhusu wanaume wenye kisukari,mimi nimekuwa na kisukari kwa miaka 13 kama ukifata masharti hiyo athari haitakwepo.Unatakiwa kufata masharti ya kula matunda na mbogamboga kwa wingi,kunywa maji mengi,acha kutumia soda na pombe zenye sukari(bia 2-3 kama Serengeti au pombe kali mara 1-2 kwa wiki haina madhara)kupunguza sio kuacha vyakula vya wanga,vyakula vya protini kama mayai,nyama,maharage na maziwa ule mara kwa mara,ufanye mazoezi,ulale mapema na mwisho umeze dawa kwa wakati baada ya kula sio kabla.
Kama una uwezo nunua mashine ya kupima glucose na kujipima kwa uchache mara 2 kwa wiki ukiamka na masaa 2 baada ya mlo,mashine hizi ni elfu 45 tu.

Pole kwa kuugua kisukari kwa kipindi kirefu kiasi hicho! Ok, ukipenda njoo kwa babu Loliondo tatizo linaweza kupungua kama si kwisha.
 
Back
Top Bottom