Wanawake wengi wanapoteza wanaume wa kuwaoa kwa sababu hii

politicians

Senior Member
Apr 8, 2018
151
117
Habari wakuu!

Kwanza nakiri kuwa mapenzi hayana mtaalamu ila lazima tubadilishane udhoefu ilitujiimarishe zaidi na haya
mambo kwa sababu mapenzi ndio maisha yenyewe,kipindi natafuta mke wa kuoa nilipata tabu sana kwa sababu nilikuwa sijui kuwa wanawake wengi wana ugonjwa huu wa (kutosikiliza vizuri).

Hivyo basi leo nitajikita katika kuelezeza sababu hiyo kwa jinsi gani inawafanya wanawake wengi wanapoteza wanaume wa kufunga nao ndoa.

KUTOSIKILIZA VIZURI,
Hii ni sababu kubwa sana inayo wafanya wanawake kupoteza wanaume pontential wanaoweza kuwaoa, kwa utamuduni wetu wa kiafrika mwanaume mara nyingi ndio huwa anamuaza kumtongoza mwanamke, hapo ndio kwenye shughuli yenyewe sasa, asiliimia kubwa ya wanawake unapomtongoza huwa hakusilizi ili kukuelewa anakusikiliza ili akujibu yaani unakuta unaongea mwenzio jibu lake tayari lipo mdomoni anakusiliza umalize tu akujibu yaani hakuna connection kati ya "mdomo na ubongo" ndio maana unakuta mwanamke anaweza akakujibu shit kwa mara ya kwanza halafu badae akaanza kujutia mwenyewe.

Mwanamke anatakiwa asikilize vizuri kwa lengo la kuelewa "intention" ya mwanaume asikariri tu kuwa kila mwanaume shida yake ni ngono tu kwa mwanamke sio kweli, halafu sisi wanaume tunatofautiana utashi na uwezo wa kujieleza kwa hiyo mwanamke asiyesikiliza vizuri anaweza asielewe somo na kusababisha
akose mme kirahisi,

Kitu kingine muonekeano, kisaikolojia akili ya mtu hubadilisha muonekano wake, mwanamke anaweza akamuona mwanaume hamvutii hata kidogo kwa mara ya kwanza lakini kwa kumsikiliza na kupima akili yake anaweza akagundua kuwa huyo mwanaume ana mvuto wa kipekee tofauti na anavyoonekana kwa nje, kitu kingine umiliki wa vitu wanawake wengi wanatabia ya kumuheshimu mtu kulingana na vitu alivyonavyo kwa mfano wakimuona mwanaume mwenye gari wanamshobokea kuliko mtembea kwa miguu, katika maisha yangu nilishawahi kumuona tajiri akitembea kwa miguu umbali mrefu na omba omba anaendesha gari la kuazima, wanawake msikubali vitu viwadanganye kikubwa nikumsikiliza mtu vizuri nia yake hasa nini? Na kufanya tafakari kwa kujipa mda sio kukurupuka tu na majibu mafupi kama ya twitter, mtakosa waume,

Kitu kingine, mwanamke anaweza akatongozwa akakimbilia kujibu haraka nina mtu wangu, unamuuliza umeolewa?, ana jibu "hapana ni boyfriend wangu tupo kwenye mahusiano nae miaka mi 3 sasa" unamuuliza
ameshijatambulisha kwenu anajibu "hapana", sasa unabaki unajiuliza haya mahusiano yanahusiana na nini?
wanawake wengi wakati mwingine muda unawadanganya sana, wanasahau kuwa kuna wanaume wanaweza wakaanza mahusiano na mwanamke ndani ya mwezi mmoja na baada ya miezi 3 wakafunga ndoa na ndoa ikadumu vizuri tu.

La mwisho swala wanawake kutoa namba za simu, unakuta umekutana na mwanamke mahali flani ukamuomba namba ya simu anakujibu siku nyingine au mimi sina simu, halafu wakati huohuo mwanamke hajaolewa sasa unajiuliza kwani ukimpatia mtu namba yako ya simu kuna shida gani? unachotakiwa mpatie mtu namba yako ya simu halafu msikilize nia yake hasa nini?,ukiona humuelewi na anakusumbua una mbock tu kwani inachukua dakika ngapi?,katika dunia ya leo sio ya kupuuza namba ya mtu huwezi kujua kesho mtakutana wapi na atakusaidia kipi labda awe mtu mbaya,

Binafsi kama mwanaume siwezi kumnyima mtu namba yangu ya simu labda awe shoga au mwizi kwa sababu hao watu sina urafiki nao,all in all wanawake mjifunze kusikiliza vizuri ili muolewe mapema ukiwafanyia utafiti wanawake wengi walio olewa kwa kufunga ndoa kabisa wakiwa chini ya miaka 26 wana sifa ya kusikiliza vizuri kwa sababu wengi wao chini ya umri huo huwa ni viziwi kabisa kwenye mahusiano yenye tija.

Asante nawasilisha!
 

vanus

JF-Expert Member
May 27, 2017
835
1,943
“unakuta unaongea mwenzio jibu lake tayari lipo mdomoni anakusikiliza umalize tu akujibu yani hakuna connection kati ya "mdomo na ubungo"ndio maana unakuta mwanamke anaweza akakujibu shit kwa mara ya kwanza halafu badae akaanza kujutia mwenyewe”

Huu ni ugonjwa wa taifa, haswaa hao dada zetu degree holder, ujuaji mwingi sana, wakishajua kiingereza tu kidogo basi yeye kila kitu ni kubishana ili mradi ameropoka na yeye aonekane mtu kumbe ni hopeless unawaza hii pesa mzazi wake ni akheri angechoma mbuzi na beer za kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

sankara25

JF-Expert Member
Aug 19, 2022
392
766
Kuna baadhi ya wanwake ni waelewa sana tu mbona ata kwenye ishu ya kutoa no ni simple tu ata kama ako na mtu wake
 

politicians

Senior Member
Apr 8, 2018
151
117
“unakuta unaongea mwenzio jibu lake tayari lipo mdomoni anakusikiliza umalize tu akujibu yani hakuna connection kati ya "mdomo na ubungo"ndio maana unakuta mwanamke anaweza akakujibu shit kwa mara ya kwanza halafu badae akaanza kujutia mwenyewe”

Huu ni ugonjwa wa taifa, haswaa hao dada zetu degree holder, ujuaji mwingi sana, wakishajua kiingereza tu kidogo basi yeye kila kitu ni kubishana ili mradi ameropoka na yeye aonekane mtu kumbe ni hopeless unawaza hii pesa mzazi wake ni akheri angechoma mbuzi na beer za kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
haha ni hatari sana mkuu!
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
47,947
63,143
Habari wakuu!
kwanza nakiri kuwa mapenzi hayana mtaalamu ila lazima tubadilishane udhoefu ilitujiimarishe zaidi na haya
mambo kwa sababu mapenzi ndio maisha yenyewe,kipindi natafuta mke wa kuoa nilipata tabu sana kwa sababu nilikuwa sijui kuwa wanawake wengi wana ugonjwa huu wa (kutosikiliza vizuri).hivyo basi leo
nitajikita katika kuelezeza sababu hiyo kwa jinsi gani inawafanya wanawake wengi wanapoteza wanaume
wa kufunga nao ndoa.

KUTOSIKILIZA VIZURI,hii ni sababu kubwa sana inayo wafanya wanawake kupoteza wanaume pontential wanaoweza kuwaoa,kwa utamuduni wetu wa kiafrika mwanaume mara nyingi ndio huwa anamuaza kumtongoza mwanamke, hapo ndio kwenye shughuli yenyewe sasa,asiliimia kubwa ya wanawake unapomtongoza huwa hakusilizi ili kukuelewa anakusikiliza ili akujibu yani unakuta unaongea mwenzio jibu lake tayari lipo mdomoni anakusiliza umalize tu akujibu yani hakuna connection kati ya "mdomo na ubungo"ndio maana unakuta mwanamke anaweza akakujibu shit kwa mara ya kwanza halafu badae akaanza kujutia mwenyewe,.mwanamke anatakiwa asikilize vizuri kwa lengo la kuelewa "intention" ya mwanaume asikariri tu kuwa kila mwanaume shida yake ni ngono tu kwa mwanamke sio kweli,halafu sisi wanaume tunatofautiana utashi na uwezo wa kujieleza kwa hiyo mwanamke asiyesikiliza vizuri anaweza asielewe somo na kusababisha
akose mme kirahisi,

kitu kingine muonekeano, kisaikolojia akili ya mtu hubadilisha muonekano wake,mwanamke
anaweza akamuona mwanaume hamvutii hata kidogo kwa mara ya kwanza lakini kwa kumsikiliza na kupima
akili yake anaweza akagundua kuwa huyo mwanaume ana mvuto wa kipekee tofauti na anavyoonekana kwa
nje,kitu kingine umiliki wa vitu wanawake wengi wanatabia ya kumuheshimu mtu kulingana na vitu alivyonavyo kwa mfano wakimuona mwanaume mwenye gari wanamshobokea kuliko mtembea kwa miguu,katika maisha
yangu nilishawahi kumuona tajiri akitembea kwa miguu umbali mrefu na omba omba anaendesha gari la kuazima,wanawake msikubali vitu viwadanganye kikubwa nikumsikiliza mtu vizuri nia yake hasa nini?na kufanya tafakari kwa kujipa mda sio kukurupuka tu na majibu mafupi kama ya twitter,mtakosa waume,


kitu kingine,mwanamke anaweza akatongozwa akakimbilia kujibu haraka nina mtu wangu,unamuuliza umeolewa?,ana jibu "hapana ni boyfriend wangu tupo kwenye mahusiano nae miaka mi 3 sasa"unamuuliza
ameshijatambulisha kwenu anajibu "hapana",sasa unabaki unajiuliza haya mahusiano yanahusiana na nini?
wanawake wengi wakati mwingine muda unawadanganya sana,wanasahau kuwa kuna wanaume wanaweza
wakaanza mahusiano na mwanamke ndani ya mwezi mmoja na baada ya miezi 3 wakafunga ndoa na ndoa ikadumu vizuri tu,

la mwisho swala wanawake kutoa namba za simu,unakuta umekutana na mwanamke mahali flani ukamuomba namba ya simu anakujibu siku nyingine au mimi sina simu,halafu wakati huohuo mwanamke
hajaolewa sasa unajiuliza kwani ukimpatia mtu namba yako ya simu kuna shida gani?,unachotakiwa mpatie
mtu namba yako ya simu halafu msikilize nia yake hasa nini?,ukiona humuelewi na anakusumbua una mbock tu
kwani inachukua dakika ngapi?,katika dunia ya leo sio ya kupuuza namba ya mtu huwezi kujua kesho mtakutana wapi na atakusaidia kipi labda awe mtu mbaya,binafsi kama mwanaume siwezi kumnyima mtu namba yangu ya simu labda awe shoga au mwizi kwa sababu hao watu sina urafiki nao,all in all wanawake mjifunze kusikiliza vizuri ili muolewe mapema ukiwafanyia utafiti wanawake wengi walio olewa kwa kufunga ndoa kabisa wakiwa chini ya miaka 26 wana sifa ya kusikiliza vizuri kwa sababu wengi wao chini ya umri huo huwa ni viziwi kabisa kwenye mahusiano yenye tija.Asante nawasilisha!
Kwa swaga hizi labda uowe muimba kwaya wa misa ya jioni.

Bado huwajui wanawake wewe.
 

frenderPH

JF-Expert Member
Oct 30, 2019
582
711
Wanawake wanachofanya ni sahihi, kwasababu akisema akufurahishe wewe kwa kukubariana na unacho kihitaji yeye atajidhulumu nafsi yake, na wao ni watu wanahitaji kuchagua. Mwanamke ukimuomba namba akakaza sio kwamba ni utoto, pengine haujamvutia anashindwa kukwambia direct. Mwanamke akivutiwa na wewe ukimwambia chochote atafanya kama namba atakupa tena fasta, atakwambia hayupo kwenye mahusiano hata kama anayo ili tu umtongoze akukubalie. So tusiwajaji sana. Tuwape heshima yao kama wanawake.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 

Iringakwanza

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,017
1,589
Wanawake wengi Wanaolewa ni wale wasiokuwa na matumizi mabaya ya fedha na ukipata mwanamke muwazi hasa kwenye matumizi itakuwa vizuri zaidi mwanamke kama huyu ata ukimpa pesa nyingi hutojutia sababu ni muwazi na ata mkifanikiwa hawezi kuonesha tamaa na yeye kumiliki mali wala kukuzunguka kufanya mambo mengine kwa siri
 
24 Reactions
Reply
Top Bottom