Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,448
- 16,312
"MADAKTARI, wauguzi wanakimbizana kutoa huduma kwa wagonjwa, kama wakati wa Rais John Magufuli.” Ni kauli ya mmoja wa wagonjwa waliozungumza na Raia Mwema jana, kuhusu mabadiliko ya utendaji wa hospitali hiyo, tangu ilipopata Mkurugenzi Mpya, Profesa Mohamed Janabi.
Mgonjwa huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji hospitalini hapo, kwani Profesa Janabi amekuwa akiingia kazini mapema kuliko madaktari wake, na kuzunguka kila sehemu na kila idara kuona wanavyohudumia wagonjwa. “Siku za nyuma wagonjwa tulikuwa tunawahi kufika, lakini huduma zinaanza saa tatu au saa nne. Sasa hivi madaktari wengi saa moja wako kazini, ikifika saa mbili kazi zinaanza yaani ni mshangao wa hali ya juu,” alisema mgonjwa huyo.
Mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo, alisema kuna mchakamchaka tangu Profesa Janabi aingie. "Mkurugenzi anafika, saa moja yuko kazini, wewe mwenzangu na mimi unaingiaje saa mbili? Akifika anazunguka kote, anajua nani wanapaswa kuwapo, akiona mgonjwa anazungumza naye, shida yake, kwa nini yuko hapa, amesikilizwa, yaani anafuatilia kila kitu," alisema Muuguzi huyo.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili hospitalini hapo, umebaini kuwapo mabadiliko hayo. Eneo ambalo madaktari wakilitumia kusimama na kupoteza muda, sasa hivi hakuna anayesimama nje, usafi unafanyika kwa kiwango cha hali ya juu.. Lakini pia madaktari na wauguzi wamekuwa na kuhudumia wakipokea wagonjwa vizuri tofauti na awali.
Wakati wa Rais Magufuli, huduma kwenye hopitali Hiyo ziliboreka huku kiwango cha rushwa kikielezwa kupungua. Madaktari na wauguzi waliwajibika ipasavyo, wakihofia kutumbuliwa kutokana na ziara za ghafla alizofanya hospitalini hapo.
Hivi karibuni, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Profesa Janabi aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, akichukua nafasi ya Profesa Lawrence Maseru aliyestaafu. Alimteua Dk Peter Kisenge kuziba nafasi ya Profesa Janabi. Kabla Dk Kisenge alikuwa Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo JKCI.

Raia Mwema.