Muhimbili kuanzisha benki ya mbegu za uzazi, kuzinduliwa na Rais Samia

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,774
Uwekezaji unaofanywa na Serikali ya awamu ya 6 inazidi kupaisha Hospital ya Taifa ya Muhimbili kufikia viwango vya Kimataifa kwenye tiba za kibingwa na bobezi ikiwemo upandikizaji wa mimba na Benki ya Mbegu.

---
RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua benki ya kuhifadhi mbegu za uzazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel akizungumza leo Februari 28, 2024 amesema Rais Samia atazindua benki hiyo hivi karibuni.

Amesema MNH imeanza kuhifadhi mbegu hizo za uzazi na mtu akitaka kupata mtoto basi atafika hospitalini hapo na kupandikiziwa.

“Mbegu zitahifadhiwa kwa muda wa miaka mitano hadi 10, mtu kama hahitaji mtoto kwa wakati husika zitahifadhiwa, wakati akiona sasa anahitaji kupata mtoto basi atapandikiziwa,” amesema.

Amesema sio lazima watu waende nje kupandikiza kwani ndani ya hospitali hiyo wanapandikiza na kutunza mbegu hizo.

“Sio lazima uende Uturuki kupandikiza mimba, Muhimbili tunafanya na kama ukihitaji kuhifadhi mayai yako hutaki mtoto kwa sasa hadi hapo baadae tunakuhifadhia mayai yako hadi hapo baadae utakapokuwa tayari tutalikutanisha na kupata mtoto,”amesema Dk Mollel.
 
Je,tutachangia kwa hiari kama damu?

Mbona maelezo yanajitosheleza...

MNH imeanza kuhifadhi mbegu hizo za uzazi na mtu akitaka kupata mtoto basi atafika hospitalini hapo na kupandikiziwa.

“Mbegu zitahifadhiwa kwa muda wa miaka mitano hadi 10, mtu kama hahitaji mtoto kwa wakati husika zitahifadhiwa, wakati akiona sasa anahitaji kupata mtoto basi atapandikiziwa,”
 
Inamaana wanaume wamepungua kiasi kwamba mbegu inabidi zipatikane hospitali?
Au ni msukumo wa mataifa ya nje, kuathiri vizazi halisi, na kuleta broiler wengi huku duniani?​

Mbona maelezo yanajitosheleza...

Unahifadhi mbegu zako za uzazi kwa miaka tajwa, zitatumika kupandikizwa utapohitaji ndani ya miaka tajwa...

MNH imeanza kuhifadhi mbegu hizo za uzazi na mtu akitaka kupata mtoto basi atafika hospitalini hapo na kupandikiziwa.

“Mbegu zitahifadhiwa kwa muda wa miaka mitano hadi 10, mtu kama hahitaji mtoto kwa wakati husika zitahifadhiwa, wakati akiona sasa anahitaji kupata mtoto basi atapandikiziwa,”
 
Back
Top Bottom