Mugabe kung'atuka akishindwa uchaguzi...

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,069
Reaction score
34,839
Rais-Robert-Mugabe.jpg

Rais Robert Mugabe

Raia wa Zimbabwe wanapiga kura katika uchaguzi wa Urais unaotajwa kuwa na ushindani mkali huku kukiwa na madai ya udanganyifu. Rais Robert Mugabe wa miaka 89 amesema atang’atuka ikiwa yeye na chama chake cha Zanu-PF watashindwa.
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) wamelalamikia Zanu-PF kwa kuhitilafiana na utaratibu wa uchaguzi ili kunyakua ushindi, lakini chama tawala kimekanusha madai hayo.Shughuli za kampeini zimekua ghasia zozote huku kukiwa na visa vichache sana vya kuwatisha wapiga kura.

Vyama vya Zanu-PF na MDC viliunda serikali ya muungano mwaka wa 2008 baada ya muafaka wa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi kufuatia matokeo ya Urais yaliyozua utata. Bw. Tsvangirai alishinda awamu ya kwanza, lakini akajiondoa kwa raundi ya pili akilalamikia mashambulizi yaliyolenga wafuasi wake.
Serikali ya Zimbabwe imewapiga marufuku waangalizi wa magharibi kuchunguza uchaguzi wa leo. Hata hivyo Muungano wa Afrika (AU), Kanda ya Kusini mwa Afrika (SADC) na makundi ya kijamii nchini Zimbabwe yamekubaliwa kufuatilia jinsi uchaguzi utakavyoendeshwa.

Watu milioni 6.4 wamejiandikisha kupiga kura hii, na maelfu walijitokeza kwenye kampeini za uchaguzi. Matokeo yanatarajiwa kutolewa kwa siku tano zijazo. Mwandishi wa BBC aliyeko Harare amesema kuna foleni ndefu katika vituo vya kupigia kura ikiwa siku ya mapumzoko kuhakikisha raia wanapata nafasi ya kuamua serikali mpya.

Mshindi wa moja kwa moja sharti apate asili mia 50 ya kura zote kutangazwa Rais. Ikiwa hakuna mgombea atapata kura hizo, raundi ya pili imepangwa kufanyika Septemba 11. Uchaguzi huu ndio wa kwanza kufanyika Zimbabwe chini ya katiba mpya iliyopitishwa mnamo mwezi Machi mwaka huu.
 
Huyu mze anajivunjia heshima sasa. Wananchi wamemchoka yeye bado yupo yupo tu huku akiboronga nchi.
 
Yaani kung'atuka ni hadi ashindwe..?? Huko si kung'atuka bali ni kushindwa... Kwani wanaoshindwa kwenye uchaguzi huwa wanaendelea kuwa na madaraka..??? Asituletee kizungumkuti..
 
Mugabe ni jembe admu kabisa kuwahi kupatikana Afrika, naamini hata watasha wanalijua hilo .
 
Rais-Robert-Mugabe.jpg

Rais Robert Mugabe

Raia wa Zimbabwe wanapiga kura katika uchaguzi wa Urais unaotajwa kuwa na ushindani mkali huku kukiwa na madai ya udanganyifu. Rais Robert Mugabe wa miaka 89 amesema atang'atuka ikiwa yeye na chama chake cha Zanu-PF watashindwa.
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) wamelalamikia Zanu-PF kwa kuhitilafiana na utaratibu wa uchaguzi ili kunyakua ushindi, lakini chama tawala kimekanusha madai hayo.Shughuli za kampeini zimekua ghasia zozote huku kukiwa na visa vichache sana vya kuwatisha wapiga kura.

Vyama vya Zanu-PF na MDC viliunda serikali ya muungano mwaka wa 2008 baada ya muafaka wa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi kufuatia matokeo ya Urais yaliyozua utata. Bw. Tsvangirai alishinda awamu ya kwanza, lakini akajiondoa kwa raundi ya pili akilalamikia mashambulizi yaliyolenga wafuasi wake.
Serikali ya Zimbabwe imewapiga marufuku waangalizi wa magharibi kuchunguza uchaguzi wa leo. Hata hivyo Muungano wa Afrika (AU), Kanda ya Kusini mwa Afrika (SADC) na makundi ya kijamii nchini Zimbabwe yamekubaliwa kufuatilia jinsi uchaguzi utakavyoendeshwa.

Watu milioni 6.4 wamejiandikisha kupiga kura hii, na maelfu walijitokeza kwenye kampeini za uchaguzi. Matokeo yanatarajiwa kutolewa kwa siku tano zijazo. Mwandishi wa BBC aliyeko Harare amesema kuna foleni ndefu katika vituo vya kupigia kura ikiwa siku ya mapumzoko kuhakikisha raia wanapata nafasi ya kuamua serikali mpya.

Mshindi wa moja kwa moja sharti apate asili mia 50 ya kura zote kutangazwa Rais. Ikiwa hakuna mgombea atapata kura hizo, raundi ya pili imepangwa kufanyika Septemba 11. Uchaguzi huu ndio wa kwanza kufanyika Zimbabwe chini ya katiba mpya iliyopitishwa mnamo mwezi Machi mwaka huu.

"Katiba ijayo lazima sasa iondoe kinga kwa marais ili mtu yeyote aweze kumshtaki Rais na hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa," Mateo Qaresi (July 2013).
 
Yaani kung'atuka ni hadi ashindwe..?? Huko si kung'atuka bali ni kushindwa... Kwani wanaoshindwa kwenye uchaguzi huwa wanaendelea kuwa na madaraka..??? Asituletee kizungumkuti..

Ni maswali ambayo nilitaka kuuliza wadau. Asante kwa kuniwahi
 
Mugabe ni Jembe la Ukweli although sikubaliani na the way he runs some things,his ways ila this guy has GUTS.Yani hata ukiangalia his interviews, jinsi anavyojibu maswali,aisee huyu jamaa lazima umkubali. This guy,dah!..I wish i cud pick his brain nijue tu his thoughts
 
Back
Top Bottom