Mugabe aomba msaada wa dola bilioni moja za Marekani

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameomba kupatiwa msaada wa dola bilioni moja za kimarekani ili kukabiliana na baa la njaa lililosababishwa na ukame nchini humo

Taifa hilo halijapokea mvua ya kutosha tangu mwaka jana na watu 1.5 milioni wanahitaji msaada wa chakula, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Maelfu ya mifugo wamefariki kutokana na ukame.
chanzo :BBC
 
Lazima asalimu Amri kwa hawa watu, mentality yao ni kubwa sana. Mbona kabla ya kuwatukana hakupata baa la njaa?
 
Ngoja tuone kama atakataa msaada kutoka kwa aliyowaita mashoga ...
 
Wanaomsifu Mugabe sijui huwa wanatumia kiungo gani kufikiri.
mimi mwenyewe nawashangaa, watu wa Zimbabwe wamekua wakimbizi south Africa, wanadharaulika sana na leo hii wananchi wanakufa njaa huku yeye na familia yake wakiishi kifahari
 
rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameomba kupatiwa msaada wa dola bilioni moja za kimarekani ili kukabiliana na baa la njaa lililosababishwa na ukame nchini humo
chanzo: mitandao mbalimbali
Pumbaf* huyu mzee. Anaamini yeye tuu ndio mwenye akili Zimbabwe yote.
 
Wanaomsifu Mugabe sijui huwa wanatumia kiungo gani kufikiri.
Ukiwa tu outspoken kuongea hovyo hovyo na kutukana Marekani bila kufanya Kazi yeyote ya msingi waafrica wanakupenda. Leo hii JPM aanze kutukana Marekani kila muda hata asipofanya kitu kingine chochote atapata wafuasi zaidi. Kuiba akili za waafrika kazi rahisi sana
 
Back
Top Bottom