Mzee Jongwe amejifungia nyumbani jana kutwa na leo pia.
Akiwa nyumbani kwake yupo katika simu akiwasiliana na jamaa wa tume ya uchaguzi kuhakikisha kura zinaongezewa kwa ZANU-PF na baadae atamwambia mweyekiti wa tume hio kutangaza matokea hao kwamba Robert Mugabe ndio raisi na kila mtu anendele na shughuli zake.
Mugabe amejifunza kutoka Kenya na amewahi kwa kuwasambaza askari polisi nchi nzima. Kwa hio hakuna mtu wa kuanza kufanza fujo kama pangekuwepo na vacuum hadi leo.
Hii yote sote tunajua kwamba ndio siasa za Afrika.
Mnakumbuka wimbo aloimba Hassan Rehani Bichuka na DDC Mlimani Park, usemao- "Sura ya Zimbabwe inajionesha, siasa za Mugabe zinazidi kung'araa.."
Afrika kiboko!