RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ameonya mawaziri wake dhidi ya kuwa na nyumba ndogo, akisema kuwa wanatumia mali zao nyingi katika uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengi wasio wake zao.
Alisema tabia hiyo ndiyo chanzo cha kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi, kwani anawafahamu mawaziri wengi wanaougua ugonjwa huo.
Mugabe ambaye ameiongoza nchi yake tangu ilipojinyakulia uhuru wake mwaka 1980, alitoa matamshi hayo Jumamosi iliyopita wakati wa harusi ya mpwa wake.
Huku akiwasihi wanandoa kuwa waaminifu katika ndoa yao, Rais Mugabe alionya dhidi ya kile alichokitaja kama tabia ya wanaume kuwa na nyumba ndogo nchini Zimbabwe, akisema kuwa mawaziri wake aliowatarajia kuwa watu wenye maadili mema pia walikuwa na tabia ya uasherati.
Kwa mujibu wa jarida la New Zimbabwe, Mugabe alisema kuwa mali waliyonayo baadhi ya waziri ndiyo chanzo cha matatizo kwenye ndoa. Na kwamba nyumba ndogo si jambo jema katika jamii.
Nawasihi muachane na tabia hiyo. Mwanamume mmoja na mke mmoja bila shaka kutafanikisha ndoa zenu,' alisema Mugabe.
Mugabe pia alitoa changamto kwa wanawake kukataa tabia hiyo kwa kutojihusisha na wanaume walio kwenye ndoa.
Wanawake lazima wapigane dhidi ya tabia hii mbovu, lakini wao ndio walioko katika nyumba ndogo, alisema.
Alisisitiza kuwa usawa wa kijinsia haupaswi kumaanisha kutupilia mbali utamaduni na maadili.
Mugabe alisema kwa mzaha kuwa japo hualikwa kwenye harusi nyingi, wakati waume na wake wanapotalikiana huwa hajulishwi.