Mufti Zubeir: Kuna mijitu ilikuwa na kesi za Uhujumu Uchumi, huruma ya Magufuli ikawataka warudishe walizoiba

Unamkumbuka Idd Amin?
Sasa utamfananisha idd Amin na jpm.jpm ni hayati tayari kwa nn madhehebu ya dini,Christian plus Muslim ,wakubaliane kufanya ibada ya pamoja !?,hivi viongozi wote wa dini ni mazwazwa !!?
 
Mufti jifunze lugha ya kistaarabu "mijitu " maana yake nini?
Nadhani mijitu ni watu wasiokuwa na shukrani.

Yani wasioona mema ,wenyewe wanaangalia mabaya ma 2 kwenye mema 98. Hao ndio mijitu, na humu wapopia.

R.I.P Magu.
 
M

Nataka viongozi wa dini waseme mnachotaka kusikia, kile msichotaka kusikia wakisema wanakua sio viongozi wa dini.

Lazima tuwe jamii ya kukubali kusikia tusiotaka kusikia. Sio kila siku kusikia tunayotaka kusikia.

Hao viongozi wa dini ni binadamu, wana hisia, wana mitanzamo yao pia. Tusikilize na mitazamo yao.

Hatuwezi kua tunataka nchi yenye watu wenye mawazo yanayofanana muda wote. Viongozi wote wawe kama Bagonza, haiwezekani, Bagonza ni Bagonza na Mufti simba ni Mufti Simba.
Mkuu hebu twende pamoja. Kiongozi wa Dini kuwaita baadhi ya Waumini wake au Binadamu wenzie MIJITU tena wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwako wewe ni poa tu siyo??
 
Mkuu hebu twende pamoja. Kiongozi wa Dini kuwaita baadhi ya Waumini wake au Binadamu wenzie MIJITU tena wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwako wewe ni poa tu

Acha kujifanya mtakatifu nawewee, kwani ukisikia mijitu we unaelewanini.

Kwangu mimi mijitu niwatu wasionashukrani na mwingine anatafsiriyake, wewe unaelewanini.
 
Vipi tena Sheikh wetu Mkuu anatumia lugha kali ya hukmu kwa washukiwa wa uhujumu vs watuhumiwa wa ugaidi (watu waliobanwa hawapati ufumbuzi) awamu hii ya sita ila kipindi cha awamu ya 5 walikuwa wapole .

Nini kimebadilika Leo hii wanaJF Great Thinkers. Ni kwa kuwa sasa tuna Rais ambaye ni mwanamke tofauti na yule Rais aliyekuwa mwanaume?

Au ni mtizamo wa kiitikadi ya kidini katika kuchambua serikali iliyokuwa chini ya rais wa jinsia tofauti?

Au pia kwa kuwa mwendazake alikuwa mbabe 'hapangiwi' sasa huyu wa awamu ya sita wanamuona si mbabe hivyo wanataka 'kumpangia' ?

BAKWATA hapa wamepotoka kwa kutaka kutumia itikadi kumburuza Rais wa awamu ya sita. ( Kusisitiza uthubutu lazima timu yako ishinde)?
 
M

Nataka viongozi wa dini waseme mnachotaka kusikia, kile msichotaka kusikia wakisema wanakua sio viongozi wa dini.

Lazima tuwe jamii ya kukubali kusikia tusiotaka kusikia. Sio kila siku kusikia tunayotaka kusikia.

Hao viongozi wa dini ni binadamu, wana hisia, wana mitanzamo yao pia. Tusikilize na mitazamo yao.

Hatuwezi kua tunataka nchi yenye watu wenye mawazo yanayofanana muda wote. Viongozi wote wawe kama Bagonza, haiwezekani, Bagonza ni Bagonza na Mufti simba ni Mufti Simba.
Unapotaka kuwa na mitazamo yako ni lazima ujiondoe kwanza kwenye mamlaka yako na uelezee maoni binafsi ila unapokuwa na kofia inayokubeba unaaminiwa kwamba ni maoni ya watu unaowaongoza na sio mitazamo binafsi
 
18 April 2021
Dodoma, Tanzania

RAIS SAMIA AWASHA MOTO - "MNALINGANISHA MAGUFULI NA SAMIA, HAWA WATU NI KITU KIMOJA"

RAIS Samia Suluhu na Rais Hussein Mwinyi, leo Aprili 18, wameshiriki katika kongamano lililoandaliwa na viongozi wa dini Chimwaga, maalum kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Hayati Magufuli.
 
Historia zinaandikwa mkuu hata wanaozaliwa sasa wataambiwa, mnaona Umeme, Reli, Ndege, madaraja namengine mengi kwamba kulikuwa na mtu anaitwa magu ambae alifanya maamuzi magumu katika muda mfupisana chini ya miaka mitano kuliinua taifa, na Rais wa kwanza mwanamke akamalizia kazimnazoniona leo.

Hawa wachumiatumbo wanajaribu tu kumchafua lakini wanajua wazi wana fanya vitendo vya aibu tu.
Walishindwa kumchafua alipokuwa hai, haitowezekana hivi sasa.
Tutayatetea yaliyo mazuri aliyoyafanya kwa Taifa hili wakati wote mpaka siku watakapoacha upumbafu wao.
 
Jizi la kura la liuaji, acha kunajisi neno masiha na malevi ya madaraka.
Kunywa maji upunguze hizo jazba, JPm alikuwa mkombozi wa Taifa hili. Hakuna mtanzania mwenye akili timamu anaweza kushawishika na huo be uzushi wenu.
 
Mkuu hebu twende pamoja. Kiongozi wa Dini kuwaita baadhi ya Waumini wake au Binadamu wenzie MIJITU tena wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwako wewe ni poa tu siyo??
Ni mijitu ndio, watu wa hovyo.

Yesu kristo alienda kwenye nyumba ya ibada akakuta imebadilishwa matumizi alikasirika sana, aliwasema sana.

Watu ambao wanaiba hela ambazo zingekua na manufaa ya watu wengi wakajineemesha wenyewe hakuna jina zuri la kuwaita, hakuna.
 
unapotaka kuwa na mitazamo yako nilazima ujiondoe kwanza kwenye mamlaka yako na uelezee maoni binafsi ila unapokuwa na kofia inayokubeba unaaminiwa kwamba ni maoni ya watu unaowaongoza na sio mitazamo binafsi
Anajiondoaje, aache utumishi wake?

Kina Bagonza mbona hamuwamabii waache dini, shida iwe kwa Mufti kisa kasema ambayo hutaki kusikia? Huo ni unafiki.

Acha aseme anachotaka kusema.
 
Back
Top Bottom